USHAURI:MENGI AKAAGIWE UWANJA WA TAIFA

USHAURI:MENGI AKAAGIWE UWANJA WA TAIFA

laptop90

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2017
Posts
1,827
Reaction score
2,297
Kutokana na hali halisi na kwa kuzingatia Mengi amegusa watu wengi ktk nchi hii, basi watu wengi wangependa kumuaga kwa makundi tofauti.
Kwa maono yangu Karimjee hapatoshi kuhimili idadi ya watu wataopenda kutoa heshima za mwisho, karimjee kuna hali ya kaubaguzi wa aina ya watu kuingia hivyo kufanya watu wachache waweze kumuaga.
Kwa muktadha huo kamati inayojihusisha na mazishi yake ipeleke mwili uwanja wa taifa ili kila mtu aweze kuaga.
 
Wameshausikia ushauri, maamuzi yapo kwenye fikra zao wahusika kadri watakaloona linafaa.
 
Wazo zuri maana huyo mzee alijiepusha na siasa za majitaka, hivyo watu wengi wako naye.
 
Ni kweli wazo zuri lkn nahisi harufu ya siasa kuingia kwenye haya maombolezo.
 
Wazo zuri maana huyo mzee alijiepusha na siasa za majitaka, hivyo watu wengi wako naye.

Ndo maana nasema aagwe uwanja wa taifa maana hata wasio wanasiasa wataweza kwenda kuaga, watanzania walizoea kumuona mengi kwenye tv ktk maswala ya kijamii na wangependa kwa wingi wakamuage, huku kumuagia karimjee ni ubinafsi
 
Kutokana na hali halisi na kwa kuzingatia Mengi amegusa watu wengi ktk nchi hii, basi watu wengi wangependa kumuaga kwa makundi tofauti.
Kwa maono yangu Karimjee hapatoshi kuhimili idadi ya watu wataopenda kutoa heshima za mwisho, karimjee kuna hali ya kaubaguzi wa aina ya watu kuingia hivyo kufanya watu wachache waweze kumuaga.
Kwa muktadha huo kamati inayojihusisha na mazishi yake ipeleke mwili uwanja wa taifa ili kila mtu aweze kuaga.
Wazo jema, Mkuu. Ngoja tusubiri wahusika watalichukuliaje...
 
Kila nikikumbuka kipindi Cha JK ,ITV ilivyokuwa inaibua taarifa za kina kuhusu awamu ya nne,ukosoaji wa wazi,Mara Mzee Mengi (R.I.P) akaitisha mkutano na waandishi wa habari kuwa usalama wake upo hatarini kisa Kuna kauli flan ilitolewa na kiongozi! Kuingia awamu ya Tano kila kitu kimyaa zaidi nikaja muona na K Lyn! R.I.P Mzee Mengi
 
Back
Top Bottom