Ushauri: Mchumba wangu (mwanamke) anakunywa sana pombe

Ushauri: Mchumba wangu (mwanamke) anakunywa sana pombe

IamPrince George

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2014
Posts
412
Reaction score
168
Wadau habari ya wakati huu,wana JF wenzangu napenda ushauri wenu juu ya hili,

Nina mchumba ambaye tuko nae katika mahusiano kwa muda sasa, tumeshapanga mengi, kilichobaki ni taratibu za kuishi pamoja.Tatizo la huyu mtu wangu (Mwanamke) ni matumizi ya pombe.

Anakunywa sana pombe, na nimemkataza akasema hatarudia lakini karudia tena, ukizingatia mimi situmii pombe na hata nyumbani kwetu wakijua kuwa anakunywa pombe hawataafiki na ninampenda sana zaidi ya sana.

Naombeni ushauri ndugu zangu nifanyeje na hii hali naichukia sana.

Asanteni
 
Aliniambia kuwa anakunywa lakini nikamkataza kunywa na akaniahidi kutokunywa
 
Tafuta maziwa ya kitimoto mchanganyie kwenye ulabu, ataacha kabisaaa, ila atatapika vibaya sana
 
Mpwa huyo wa bia tuachie wenyewe wanyewe wanywaji kwako humuwezi
 
je akinywa pombe anakusumbua ? au anakuwa mkali? ... mtu nayekunywa pombe huwezi mkataza mara moja lazima aache kidogo kidogo.... mimi kama ni mnywaji siyo shida kama ni mlevi kalowea hapo ni shida kama hutaweza kuhandle that mwache atapata wa kufaana nae
 
Watu tunatofautiana....!
Hutaki anywe kwa sababu imani yako hairuhusu au kwa vile wewe hunywi?
 
Ulikuwa unajua kwabisa kwamba anakunywa pombe, pombe ni ngumu kuacha, kama anakunywa kwa faida yake hana madhara wala hakwamishi kitu kwenye mahusiano yenu wewe inakukera nini?
 
kama haimuathiri wala kumfanya aonekane kituko sioni kama ni shida...tatzo ww haunywi ndio maana unaleta shida...na hivi unaongozwa na familia yenu....eti watanionaje kwani anaenda kukaa kwao?kiruuuuuuuu
 
natafuta whey powder kwaajili ya kujenga mwili anayejua inapouzwa aniambie kwa hapa dar
 
Back
Top Bottom