Ushauri: Mama mkwe wangu kaja bila taarifa

Ushauri: Mama mkwe wangu kaja bila taarifa

py thon

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2016
Posts
2,475
Reaction score
4,454
Ndugu zanguni wiki yangu imeanza vibaya nioneeni huruma,

Jumamosi nilipata ugeni wa mama mkwe wangu bila ya kupewa taarifa lakini ugeni huu umekuwa mtihani kwakweli leo nimetumia 10,000 kwa mlo mmoja tu wake yeye nimepiga mahesabu kwa mlo 3 ni 30,000 na mfano akikaa kwa siku 10 nitakuwa nimetumia laki 3 kwa msosi wake yeye tu bado mimi na watoto wangu hapa hatujala,yani leo kanitisha saa 6 hii nimetumia 10,000 kwa chakula chake yeye tu.

Naombeni ushauri nimfukuze, nikimbie nyumba niage nasafiri mpaka pale atakapoondoka, naombeni msaada wa mawazo ndugu zanguni nina mawazo tele hapa huyu mama kaja kunichanganya akili tu hapa.
 
Attachments

  • 1473758155086.jpg
    1473758155086.jpg
    65 KB · Views: 271
Acha ubahiri .
Chuku laki nanusu hemee vyakula vya miezi mingi
Yaani,sukari,kg 20,
Michele kg 30,
Mafuta liter 10,
Unga sembe na dona kg 20/
Maharagwe kg 13:
Hapo utakuwa unabadili Mboga tu.
Huku ukiwa na kg 12 ndani za dagaa nyasa
 
Ndugu zanguni wiki yangu imeanza vibaya nioneeni huruma,

Jumamosi nilipata ugeni wa mama mkwe wangu bila ya kupewa taarifa lakini ugeni huu umekuwa mtihani kwakweli leo nimetumia 10,000 kwa mlo mmoja tu wake yeye nimepiga mahesabu kwa mlo 3 ni 30,000 na mfano akikaa kwa siku 10 nitakuwa nimetumia laki 3 kwa msosi wake yeye tu bado mimi na watoto wangu hapa hatujala,yani leo kanitisha saa 6 hii nimetumia 10,000 kwa chakula chake yeye tu.

Naombeni ushauri nimfukuze, nikimbie nyumba niage nasafiri mpaka pale atakapoondoka, naombeni msaada wa mawazo ndugu zanguni nina mawazo tele hapa huyu mama kaja kunichanganya akili tu hapa.
Elfu 10 amekula nini??? Na kwanini aandaliwe yeye peke yake.
 
Duuuhh kazi kweli kweli.

Unamkimbia adui usie mjua. Tatizo hapo si mama mkwe bali ni hali duni ya maisha inayochangiwa na kipato haba.

MUHIMU : Tafuta mbinu za kujiongezea kipato. Umasikini ni laana hasa UMASKINI unapokuwa wa FIKRA
 
Yaan mtu akilia lia kisa menu especially jinsia yetu hii........
 
Hii chai nayo tena bila viungo.....chakula kitapikwaje cha mtu mmoja nyumba hyo hyo afu nyie chakula kingine
 
Back
Top Bottom