Ushauri Majina ya kwenye cheti cha ndoa na bima ya afya

kibangubangu

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2018
Posts
289
Reaction score
411
Kwenye cheti cha ndoa Mwanaume alitumia jina la kwanza lile la Ubatizo,na siyo lile la kwanza la kiacademic au kiserikali.

Kwa sasa mwanaume anataka kumkatia bima ya afya mke wake kupitia ajira yake ambayo inaruhusu mke kupewa bima ya afya.

Kwakuwa katika cheti cha ndoa jina la mwanaume la kwanza ni tofauti na jina lile la ki academic je itawezekana na kama haiwezekani nini kifanyike.
 
Ofisi za bima wamesemaje?
 
Kiacademic??..jina ni lile la kwenye cheti cha kuzaliwa.
Hapo cha kufanya, nenda mahakamani uapishwe kutumia jina moja tu (utakalochagua kati ya hayo mawili)
Utasaini na utapewa change of name deed poll.
 
Shukrani sana mkuu kuna mtu alinishaur hii kitu b4 ila nikaona si vibaya nikasikiliza na wadau wa jamii wanasemaje...thank u!
 
Nenda ofisi za NHIF. Spouse sasa hivi wanataka cheti cha ndoa pamoja kopi ya kitambulisho cha nida, kura, ama leseni ya udereva.
 
Kiacademic??..jina ni lile la kwenye cheti cha kuzaliwa.
Hapo cha kufanya, nenda mahakamani uapishwe kutumia jina moja tu (utakalochagua kati ya hayo mawili)
Utasaini na utapewa change of name deed poll.
Sasa bro haitaathiri majina yaliyopo kwenye vyeti vya shule?
 
Kwa mfano Jina langu la shule ni shija but la ubatizo ni Shadrach na yote hayo majoina yanaomekana kwenye birth certificate

So madhara gani yatatokea
 
Sasa bro haitaathiri majina yaliyopo kwenye vyeti vya shule?
Yaan kwenye cheti cha kuzaliwa na vyeti vya elimu jina ni hilohilo hakuna tofauti.

Ila katika cheti cha ndoa ndiyo jina lilitumika la ubatizo sio lile la kuzaliwa ambalo ndo la shule.
 
Baki na lile ambalo umelitumia kwenye vyeti vingi. Kwahiyo kesi yako ni vizuri ubaki na hilo ulilotumia kwenye cheti cha kuzaliwa.
Cheti kingine (cha ndoa) unaendelea kukitumia kama kilivyo, ikitokea shaka unawaonesha change of name deed poll.
 
Back
Top Bottom