Niwakati wa kutafiti na kulinganisha hasara na faida ya mabasi ya abiria hasa ya umbali mrefu kama Mwanza-Dar, Musoma/tarime-Dar, Sumbawanga/mpanda- Dar, Mwanza-Mbeya, Arusha- Mbeya, Kigoma- Dar, Bukoba-Dar na zingine nyingi ambazo kwa sasa nilazima kusafiri kwa siku mbili ili kuweza kufika unako elekea kwasababu mabasi yana lala njiani kutokana na kutoruhusiwa kuendelea na safari baada ya saa 5 usiku.
Mosi, tunahitaji kujua faida na hasara ya safari za usiku ukilinganisha na zile za mchana tu (kiuchumi na kiusalama)
Pili, tunahitaji kujifunza kwa jirani zetu mfano Kenya na Zambia juu ya kukabiliana na changamoto za safari za mabasi usiku.
Tatu, niliwahi uliza madereva wa kanda ya ziwa kadhaa juu ya suala hili wao waliniambia usalama ndio changamoto kubwa. (Lakini nikawa najiuliza mwenye jukumu la kuwalinda watanzania na mali zao ni nani? Ukifanya uchunguzi 60% ya polisi huwa hawako kazini nyakati za usiku)
Nne, demand ya watu kusafiri wakati wausiku na mchana kuendelea na shughuri zingine za uzalishaji mali ni mkubwa kwa kuangalia watu wanasafiri na magari ya mizigo na magari yanayosafitishwa kwenda nchi jirani ambayo husafiri kwa wingi wakati wa usiku ni kubwa.
Tano, nimejiridhisha wawelaji wa sera na wasimamizi wa sheria au miongozo hii sii watumiaji wa usafiri huuu kwa kiasi kikubwa, vivyo hivyo adha na karaha za watumiaji wa usafiri huu hawazijui .
Mwisho, ni jambo lisilo pingika moja ya sababu za nauli kwenda sehemu mbalimbali za nchi kuwa juu sio tu kutokana na bei ya mafuta kupanda bali hata utaratibuwa mabasi kusafiri kwa zaidi ya siku mbili umeongeza gharama za nauli kuwa juu