Ushauri kwa wote

Expedito Mduda

JF-Expert Member
Sep 22, 2009
522
240
Duniani kuna miono tofauti kwa kuwa sisi binadamu pia tumeumbwa tofauti!
Tukija kwetu Tanzania na tuchukue makundi tuliyo nayo na kuyalinganisha, tunaweza kuona tofauti hiyo!
Mfano, nimeona kwa sasa kuna tofauti kubwa sana kati ya wakristu na waislam namna wanavyoshughulia mambo yao ili waweze kuendesha maisha yao.
Wakati wakristu wakifanya kazi kubwa kuhakikisha mambo yao yanakwenda kwa mafanikio makubwa bila kukosea sana, waislamu wamekuwa mstari wa mbele kulaumu kuwa mafanikio ya wakristu katika mambo yao ni kwa sababu ya kupendelewa!
Jana nimeona Mwiba analalamika eti muungano una maonezi kwa kuwa watu wa bara na hasa shule za seminari zinaongoza kufaulisha kuliko zile za Zanzibar na hasa kwenye shule za kiislamu. Mtu mwenye akili zake akikaa afikiri, anashangaa sana. Hivi ni nani hajui kuwa Wakristu wanafanya bidii kubwa sana kuhakikisha wanafunzi wanaopita kwenye shule zao wanafaulu vizuri?
Baraza la mitihani linatunga mitihani na wakati wa kusahihisha walimu toka Zanzibar wanaitwa kuja kusahihisha kama ilivyo kwa walimu wa bara. Baraza la mitihani linaingia vipi na huo upendeleo?
Wakati wakristu wakijikita sana kwenye huduma za jamii, wengine wanajikita zaidi kwenye mijadala ambayo haihusiani kabisa na maendeleo ya nchi. Baadaye wanapofungua macho wanafikiri hawa wamependelewa na serikali. HATUTAFIKA!!
Halafu ubunifu nao ni muhimu. Hivi nyie mnaolalamika serikali imependelea wakristu, mliwahi kujiuliza hata maana tu ya ya jina SEMINARI? Maana huwa naona wengi wanafikiri labda shule yoyote ya dini inaitwa seminari na baada ya kutojua maana ya neno hilo na wewe unaita hivyo shule yako!
Mimi nawaambia msipofanya juhudi na kukaa chini mjue kosa liko wapi, mtaishia kulalamika tu!
UKITAKA KUFANIKIWA BWANA MWIBA, FANYA KAZI KWA JUHUDI NA MAARIFA. Nitakushangaa kuniona mimi nina hospitali lakini wewe unanionea wivu wakati hata wewe ukiugua unatibiwa hapohapo!!
 
Back
Top Bottom