Ushauri kwa wizara ya miundombinu kuhusu barabara zinazo ingia Mbezi stendi ya Magufuli.

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,148
7,722
Hakuna ubishi kuwa stendi ya Magufuli iliyoko Mbezi ndio kitovu cha usafirishaji ktk Jiji la DSM,.

Daladala kutoka katika pembe zote za Jiji la DSM zinaingia Mbezi kupeeleka na kuchukua abiria.

Changamoto iliyopo ni Barbara za ushoroba zinazo ingia Mbezi hazitoshelezi.
Utafiti unaonyesha kuwa Barbara zinazopitika ni;
1. Madale/goba hadi Mbezi.

2. Majumba sita/kinyerezi/maramba hadi Mbezi.

3. K.koo/Moro road hadi Mbezi.

Barbara zifuatazo ni muhimu zijengwe kwa kiwango Cha lami ili kurahisisha usafiri kwa wananchi wa maeneo mengine waweze kufika kwa urahisi;

1. Barbara ya mapinga/kidimu/kibaha hadi Mbezi.

2. Barbara ya Kisarawe/makurunge/kiluvya hadi Mbezi.

Barbara hizi ni muhimu zijengwe haraka ili kupungiza adha kwa wananchi wa maeneo hayo.
 
Wazo zuri ila mimi ninapendekeza kituo hiki kifungwe kabisa maana hakifanyi kazi iliyokusudiwa,kituo hiki kilitakiwa kijengwe kati kati ya jiji ili kuwarahisishia abiria kusafiri, na hii miji yote mikuu duniani imefanya hivi,mfano mimi ninasafiri kwa bus kwenda songea nikitokea kigamboni, ni usumbufu mkubwa kwangu niipite ofisi ya bud pale shekilango na niende mbezi!hii ni craze, kituo kijengwe pale pale ubungo au mnazi mmoja ila kujengwe line maalum ya mabus haya along pugu road na Mandela road
 
Kama hujui kwa sasa stendi ya Magufuli ndio katikati ya Jiji la DSM, Mbezi ndio centre ya Jiji la DSM, ndio maana daladala zote kutoka kila Kona ya Jiji zinaelekea Mbezi stendi ya Magufuli.

Kinacho takiwa kwa sasa ni ouboresha miundombinu niliyo ieleza hapo juu ili kutatua changamoto za wanao kaa mbali.
 
Back
Top Bottom