Ushauri kwa Waziri Ndalichako juu ya uundaji wa TCU mpya

pocha2

JF-Expert Member
Sep 23, 2014
890
396
Mh. Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kwa miaka mingi sana TCU imekuwa ina uwakilishi wa mdogo wa taaluma mbali mbali katika ngazi za juu za maamuzi za chombo hiki muhimu, utakapo kuwa unaisuka upya (TCU) tafadhari kumbuka uwakilishi huu, na ili niwe specific, vyuo vya sayansi za tiba vipate uwakilishi.

Vyuo hivi taaluma zake zipo tofauti kidogo kuanzia kwenye mitaala, muda na urefu wa semester, namna ya kufanya elimu kwa vitendo (practical and clinical training), mitihani na grading system.

Tumekuwa tukipata shida kubwa tunapowakilisha maandiko ya kuanzisha programs mbali mbali.

Zaidi ni pale ambapo miongozo ya TCU inaposahau uwepo wa vyuo vya namna hii.

Wadau wengine wanaweza kuchangia namna ya kuboresha na kuleta ufanisi.
 
Ndalichako msikivu ni mwanajamvi humu atapitia hapa aone ushauri.
 
Kwa udhalilishaji aliousema jana juu ya wanafunzi wote wa St Joseph sio vyema kabisa...Nashindwa kupata maana halisi alikuwa na maana gani ya kuwaita wanafunzi kuwa wana UWEZO MDOGO, ni dharau grade A hii, wizara anayosimamaia ilipeleka wanafunzi hapo iweje leo iseme wanauwezo mdogo?
Na ametumia criteria ipi kupima kuwa wanafunzi wote wanauwezo mdogo?
 
Tatizo la St Joseph limetengenezwa na tcu na wizara yenyewe, hivyo si vyema kukipa chuo lawama ama wanafunzi lawama zote..
 
Napatishida kuelewa kwa nini watu wenye elimu kubwa na dhamana kubwa serikalini especially kwenye wizara ya elimu kushindwa kufanya majukumu yao ipasavyo vikiendana na elimu zao walizonazo...
Pesa na kodi za wa Tanzania wengi hupotea kutokana na uzembe wa watu wachache tu..
 
Kwanza nitoe hongera kwa Dr. Ndalichako kwa uamuzi mgumu wa kuvunja bodi.
Pili ningependa kuona tcu ijayo ikitilia mkazo kwenye elimu ya vitendo zaidi ili kumwaandaa graduate kukutana na real world problems. Ni bora ukafundishwa vichache ambavyo vitakuwa na manufaa kuliko kufundishwa mzigo wa mambo ambayo hayana tija kwa mtu binafsi na hata taifa kwa ujumla.
Ni ukweli usiopingika kuwa taifa letu limekosa wasomi WABUNIFU, wenye uwezo wa kutumia resources tulizo nazo kutatua big problems in our locality.
Nashauri tunapo kazania elimu, tukazanie elimu yenye kuambatana na ubunifu, na watu wawe awarded depending on their creativity and high ability of solving critical problems.
Kama vyuo vyetu vikiliweza hili la kuhuisha ubunifu huko mashuleni naamini ndani ya miaka michache Tanzania itakuwa inchi ya mfano
 
Samahani, me nlikua natak nifaham Kwanza hivo vgezo vnavoangaliwa, maana nackia tyu waco na vgezo ila cjajua vgezo vp vnahtajika...
 
vyuo vikuu vingi hasa vya binafsi ni vibovu kama vile kuwa na mitalaa isiyofaa kufundishia, waadhiri wasio na sifa stahiki, miundombinu mibaya kwasababu ya usimamizi mbaya wa TCU, namuomba Prof. Ndalichako afanye mabadiliko makubwa kwenye taasisi hii. naona ni bora nchi yetu iwe na quality universities badala ya quantity universities.
 
Mh. Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kwa miaka mingi sana TCU imekuwa ina uwakilishi wa mdogo wa taaluma mbali mbali katika ngazi za juu za maamuzi za chombo hiki muhimu, utakapo kuwa unaisuka upya (TCU) tafadhari kumbuka uwakilishi huu, na ili niwe specific, vyuo vya sayansi za tiba vipate uwakilishi.

Vyuo hivi taaluma zake zipo tofauti kidogo kuanzia kwenye mitaala, muda na urefu wa semester, namna ya kufanya elimu kwa vitendo (practical and clinical training), mitihani na grading system.

Tumekuwa tukipata shida kubwa tunapowakilisha maandiko ya kuanzisha programs mbali mbali.

Zaidi ni pale ambapo miongozo ya TCU inaposahau uwepo wa vyuo vya namna hii.

Wadau wengine wanaweza kuchangia namna ya kuboresha na kuleta ufanisi.
Samahani, me nlikua natak nifaham Kwanza hivo vgezo vnavoangaliwa, maana nackia tyu waco na vgezo ila cjajua vgezo vp vnahtajika.
 
Back
Top Bottom