Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 34,061
- 79,423
USHAURI KWA WAZEE WANAOANZIA MIAKA 55 KUENDELEA.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.
Kwa heshima na uangalifu Mkubwa nianze kwa kuwapa Shikamoo.
Kwenu nitakuwa muangalifu wa kutupa maneno yangu huku kwa sehemu kubwa nikiacha akiba kubwa ya maneno.
Niwapongeze kwa Mafanikio makubwa ya kufikisha umri huo. Katika maisha ya kiumbe, moja ya mafanikio makubwa ni kuishi umri mrefu. Ni kuuona uzee wake.
Fanikio la pili la kiumbe ni kuacha uzao wake. Uzao ndio Legacy number moja kwa kiumbe yeyote. Kwa sababu ni muendelezo wa uhai na identity yako.
Kufikisha uzee ni baraka.
Uzee huo!
Changamoto za Kimwili;
1. Moja ya changamoto ya uzee ni changamoto za kimwili, nguvu kuisha hasa miguuni.
2. Maumivu ya kiuno, mgongo.
3. Kupoteza usingizi.
4. Magonjwa kama kisukari, presha ambayo mara nyingi huweza kusababisha kifo cha upesi au stroke
Changamoto za kimahusiano;
1. Upweke!
Hii hutokana na kadiri umri unavyokua ndivyo watu wa age yako wanavyozidi kupungua eneo ulilopo.
Na watoto uliowalea wanaanza kuondoka kwenda kuanzisha maisha yao.
Mwenza wako kufariki ni miongoni mwa changamoto za uzee.
2. Mamlaka yako kama Baba/Mama kutetereka. Enzi yako kushuka. Kutokusikilizwa.
3. Mkeo Kukudharau na kukukimbia na kwenda kwa watoto au mumeo kukuolea mke mdogo.
4. Mwanaume shauku ya kupata vibinti vidogo kuongezeka.
Hapa wengine husindwa kabisa na kuamua kuongeza mke mdogo.
5. Kutaka wazazi wako uwaombe Msamaha na uwafanyie Mema ambapo wakati huo wengi wao walishakufa.
6. Kutaka kuunganisha watoto ambapo haitawezekana kwani umoja hauletwi na wazee waliokwisha kupoteza nguvu. Umoja wa familia unaletwa Baba akiwa kijana mwenye nguvu. Watoto wakiwa wadogo.
Kushindwa kuleta umoja ukiwa Mzee itakuongezea huzuni.
Changamoto za kisaikolojia na kisosholojia
1. Kupoteza Kumbukumbu huanza kidogokidogo
2. Kujutia na kuwa na msongo wa mawazo kwa Makosa uliyoyafanya wakati ukiwa kijana.
3. ushauri wako utakuwa Irrelevant kwani mawazo yako yatapishana na kizazi kipya.
Yaani wewe utaona unatoa mawazo ya maana lakini watoto wanaokusikiliza wataona mawazo yako ni irrelevants.
Kufupisha;
Mambo ya Kufanya ukishaukaribia Uzee au ukishakuwa Mzee;
1. Akiba ya Pesa uliyonayo itumie kwaakili.
Itumie kwaajili ya Chakula kizuri cha wazee.
2. Sio Muda wa uwekezaji tena. Hasa kama pesa yako sio nyingi kama mafisadi.
Yaani kama wewe ulikuwa mtumishi wa umma. Mshahara wa kawaida. Usiwaze mambo ya uwekezaji.
Fanya Kilimo na ufugaji. Kilimo na ufugaji wa kawaida.
Uwekezaji wa maskini ni wakati akiwa kijana akiwa na nguvu nyingi.
3. Ukijenga nje ya Mji au kijijini unaadvantage hasa ukiwa na space.
Uzee unahitaji sehemu tulivu, yenye eneo lenye nafasi, na hewa safi.
4. Umri huo ni wakujipa vikazi vya mikono kama kilimo cha bustani, uangalizi wa mifugo, n.k.
Usikae tuu! Na usipendelee kutumia Usafiri labda iwe baiskeli.
Usafiri tumia ukienda Mjini. Au kwenye shughuli zilizombali.
5. Ni wakati wa kuandaa baraka na warithi wako.
Angalia Nani atabeba na kuongoza watoto na ukoo wako.
Mpe majukumu na mfundishe pasipo yeye kujua kuwa ndiye successor plan wako. Mpe uzoefu.
Mrithi wako lazima awe na sifa zifuatazo;
a) Alpha Male.
Mwanaume ambaye ni Mwanaume.
Usikabidhi ukoo wako kwa mwanaume mdhaifu(simp man). Kijana mwenye tabia legelege.
b) Mwenye Akili
c) Mwenye kuweza kuongoza wenzake na kuwaunganisha Lakini mwenye maamuzi magumu ya Haki.
d) Mwenye uwezo na kuwa na familia take.
Usimpe ukoo wako na jina lako lisibebwe na mhuni asiyeweza kuwa na familia au mwenye mawazo ya kutokuwa na familia.
e) Mwenye kuweza kujenga Mahusiano Bora na jamii.
Kwenye urithi na Baraka usiangalie Moyo wako, usiangalie sura ya mtu. Angalia Yule mwenye vigezo.
6. Sio Wakati wa kuzaa. Tena kuzaa na wanawake wengine.
Huko ni kuvuruga familia ambayo tayari upo nayo.
7. Usilazimishe watoto kuungana, kama hukuweza kuwaunganisha ukiwa kijana hutoweza ukiwa Mzee.
8. Watoto Watakaokuheshimu waite wanangu. Wakaidi Achana nao. Usilazimishe wala kuwabembeleza. Wewe ni Baba.
9. Kuwa Makini wanaojiweka karibu na wewe hasa ukiwa na vipesa. Tumia pesa yako kwa tahadhari.
10. Saidia wajukuu wenye kuonyesha kutaka Msaada. Wenye jitihada.
Usitoe pesa kwa shinikizo la mtoto wako. Toa pesa kwa mjukuu mwenye kubebeka.
11. Fanya mazoezi kadiri uwezavyo.
12. Jiunge na vikundi vya kanisani vya Kwaya uimbe uongeze siku za kuishi.
Kama hupendelei kuimba, hakikisha unapewa majukumu kanisani au msikitini na uyasimamie.
Usikae akili ikiwa ipoipo.
13. Andikisha Mali majina ya watoto wako. Mwenye akili MPE zaidi, mwenye maadili mpe zaidi. Mkaidi MPE kidogo.
14. Mke akikimbia kwa Watoto wako, atakayempokea mtoe kwenye urithi na baraka za Baba kwake au umpe kidogo.
Watoto wako wajue Jambo hilo tangu wakiwa wadogo kuwa atakayempokea Mama Yao atakapokukimbia hutombariki.
Na Mkeo ajue hayo mapema.
15. Kama utaoa mke mwingine ukiwa na miaka zaidi ya 60.
Asikae kwenye nyumba kubwa, nyumba yako ya Kwanza uliyoanzisha maisha na mkeo wa Kwanza.
Jenga nyingine sehemu nyingine kisha muweke huyo mkeo. Furahia maisha.
16. Successor wako mtembeze kwenye Mali zako zote. Mara kwa mara uwe naye.
17. Successor wako ajue wapi ukoo wako umetoka na wapi anatakiwa aupeleke.
18. Successor wako utamkabidhi kumbukumbu kama Diary na umfundishe jinsi ya kuandika tawasifu na historia ya Yale uliyomuambia, atakayoyaona na kuweka Sawa kumbukumbu.
19. Kunywa Pombe lakini kwa afya, kwa wale Wanywaji.
20. Ukiwa ikiwa Mumeo amefariki, na umri wako ni zaidi ya 55+ usiolewe tena.
Ikitokea Umeolewa hamia kwenye nyumba ya Mwanaume. Uache Mji wako wa Kwanza kwa Watoto. Huo mji unabeba jina la mumeo na ukoo wako.
21. Usimvulie chupi Kijana mdogo uliyemzidi zaidi ya miaka 5. Kama ni wale wanawake miili yao yenye Moto Sana. Kamwe usitembee na kijana mdogo.
Sio unajidhalilisha bali unawaumiza watoto wako hasa wakoume uliowazaa. Wanaumia Sana.
22. Ikiwa mkeo amekufa, umebaki Mgane.
Ukitaka kuoa Jenga nyumba nyingine ndipo ufanye hivyo. Na huyo mke mpeleke kwenye nyumba hiyo.
23. Ukizaa mtoto wa uzeeni usiwape majukumu watoto kumlea mtoto wako.
Kama utataka jukumu la kulelewa mtoto, utampa atakayelea hao watoto wako vitendea kazi na uwezo wa kufanya hivyo.
24. Ikiwa Mkeo anakusumbua na hataki kukupa huduma zako za msingi. Na unaona Jambo Hilo linakupa stress. Utaoa binti mwingine mdogo, utaanza kwa kumpangia nyumba ndogo kabla ya kumjengea. Ukiona kwa miaka na Miaka binti huyo bado ni mwema na muadilifu kwako, mjengee nyumba.
Kamwe usitumie nguvu zako na jasho lako vibaya kwa MTU asiyestahili.
25. Ikiwa Watoto wataungana na Mama yao kukuangusha na wanakukosea adabu waziwazi. Usiwape baraka wala urithi watoto wajinga na wasio na adabu.
Wewe ni Baba na Mtawala. Usipelekeshwe na yeyote ndani ya familia.
Ambaye anakiuka amri zako mpe adhabu, anayegeuka muasi muondoe kwenye mfumo wako.
Tafuta binti mwingine, zaa naye watoto kisha wape hao hizo baraka na urithi.
Usitietie Huruma!
Kamwe usimbariki mtoto mkaidi, muasi aliyekukosea adabu waziwazi wewe Kama Baba.
Kuwa Alpha Male hata kama umezeeka.
26. Andaa eneo la wewe na wanaokupenda pakuzikwa. Eneo utakalopumzika ni muhimu kulijua na uliandae.
Wewe tayari ni Mzee. Ni aibu watu kutokujua utazikiwa wapi kanakwamba aliyekufa ni kijana tena kwa ghafla.
Ni dalili ya kutojitambua na kukosa busara
Acha nipumzike sasa.
Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam