Ushauri kwa watu wote walioajiriwa

Ushauri kwa watu wote walioajiriwa

The redemeer

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2025
Posts
4,780
Reaction score
8,155
1. Jenga nyumba mapema. Iwe kijijini kwenu au mjini. Kujenga nyumba ukiwa na miaka 50 sio mafanikio. Usizoee nyumba za serikali. Faraja hii ni hatari sana. Hebu familia yako yote iwe na wakati mzuri ktk nyumba yako mwenyewe.

2. Nenda nyumbani. Usiishie kazini mwaka mzima. Wewe si nguzo ya idara yako. Ikiwa utakufa leo, nafasi yako atapewa mwingine bila kuchelewa na shughuli zitaendelea kama kawaida. Ifanye familia yako kuwa kipaumbele.

3. Usifukuzie kupandishwa cheo. Boresha ujuzi wako na uwe bora katika kile unachokifanya. Ikiwa wanataka kukupandisha ni sawa ikiwa hawatafanya hivyo sawa tu, wewe zingatia maendeleo yako binafsi.

4. Epuka porojo za ofisini au kazini. Epuka mambo yanayochafua jina au sifa yako. Usijiunge na genge la kejeli kwa wakuu wako na wenzako. Kaa mbali na mikusanyiko hasi ambayo ajenda yao ni kujadili watu tu.

5. Kamwe usishindane na mabosi zako. Utachoma vidole vyako wala usishindane na wafanyakazi wenzako, utakaanga ubongo wako.

6. Hakikisha una biashara ya kando. Mshahara wako hautakidhi mahitaji yako kwa muda mrefu.

7. Okoa pesa. ruhusu ikatwe moja kwa moja kwenye payslip yako.

8. Kopa mkopo kuwekeza katika biashara au kubadilisha mazingira ya kipato siyo kwa ajili ya kutumia ktk mambo ya anasa. Tumia faida kufanya starehe zako.

9. Hebu fanya maisha yako ya ndoa na familia kuwa ya faragha(siri). Waache wanafamilia wakae mbali na masuala yako ya kazi. Hii ni muhimu sana.

10. Uwe mwaminifu kwako mwenyewe na uamini katika kazi yako. Kukaa karibu sana na bosi wako kutakufitinisha na wenzako na bosi wako hatimaye anaweza kukustukia na kukutenga.

11. Jitahidi kustaafu mapema. Njia bora ya kupanga kuondoka kwako ilikuwa wakati ulipokea barua ya ajira. Wakati mwingine mzuri ni leo. Ktk umri wa miaka 40 hadi 50 uwe umestaafu.

12. Jiunge na Taasisi ya Ustawi wa kazi na uwe mwanachama hai kila wakati. Itakusaidia sana wakati tukio lolote litatokea.

13.Siku za likizo zitumie kwa kuendeleza nyumba au miradi ya siku zijazo, kwa kawaida unachofanya wakati wa siku za likizo ya mwaka huakisi jinsi utakavyoishi baada ya kustaafu. Hii ina maana kuwa kama utatumia muda huo kukaa kizembe kama vile kushinda unatazama tamthilia ktk TV yaani rimoti haitoki mikononi basi usitegemee chochote cha tofauti baada ya kustaafu.

14. Anzisha mradi ukiwa bado unahudumu au unafanya kazi. Hebu mradi wako ufanyike ukiwa kazini na ikiwa haufanyi vizuri, anza mwingine hadi ufanye vizuri kabisa. Wakati mradi wako unaendelea vizuri basi staafu ili kusimamia biashara zako. Watu wengi au wastaafu wanashindwa maisha kwa sababu wanastaafu kuanzisha mradi badala ya kustaafu kuendesha mradi.

15. Pesa ya pensheni si kwa ajili ya kuanzisha mradi au kununua shamba au kujenga nyumba bali ni fedha kwa ajili ya kukutunza au kujitunza katika afya njema. Pesa ya pensheni si ya kulipia karo ya shule au kuoa mke mdogo bali ni kujiangalia wewe mwenyewe na maisha yako ya uzeeni.

16. Kila wakati ukumbuke kuwa, unapostaafu hutakiwi kuwa mfano wa kuishi maisha duni baada ya kustaafu bali uwe mfano wa kuigwa na wenzako kufikiria kustaafu pia.

17. Usistaafu kwa sababu tu umezeeka au sasa wewe ni mzigo kwa kampuni na unasubiri siku yako ya kufa. Staafu ukiwa bado kijana au ukiwa bado una nguvu za kufurahia kuamka kwa kikombe cha kahawa, kufurahia jua, kupokea pesa kutoka kwa biashara yako, tembelea sehemu nzuri ambayo umeikumbuka na kutumia wakati mzuri na familia. Wale wanaostaafu wakiwa wamechelewa, hutumia takriban 95% ya muda wao kazini kuliko kuwa na familia zao na ndiyo maana wanaona ni vigumu kukaa na familia zao wanapostaafu lakini wanaishia kutafuta kazi nyingine hadi wanakufa. Wasipopata kazi nyingine, wanakufa mapema.

18. Staafu ukiwa nyumbani kwako kuliko katika makazi ya serikali ili unapostaafu uweze kufaa katika jamii iliyokulea. Si rahisi kuzoea kuishi katika eneo baada ya kukaa kwa miaka mingi kwenye nyumba ya kampuni au katika nyumba ya serikali.

19. Usiruhusu kamwe faida za ajira yako zikufanye usahau kuhusu kustaafu kwako. Manufaa ya ajira yanakusudiwa tu kukufanya uwe na utulivu.
 
Namba 6 nyongeza, ikiwezekana wafanyakazi wako wasijue biashara unayofanya na wakijua, wasijue Ni wapi ilipo angalau utapunguza kuchukiwa kazini
Hii ni ngumu hasa kwa kazi kama za usafirishaji
 
Kazini unafiki sana , punguza mdomo kwa vitu unavyofanya jadili ujinga ujinga na sio maendeleo watu wanakunja sana ndita za moyoni makazini
Mimi kazini ni kujadili magari mazuri na mpira tu ,stori za maendeleo ni kidogo sana
 
CHifu chukua serengeti lemon 4 nitalipia mwisho wa mwezi
 
Hii mada ni ya siku nyingi sana ila ahsante kwa kutukumbusha
Mimi nina miaka 60.5 ila kila nikitaka kustaafu wananibembeleza na wananiongezea mshahara na bado nina nguvu sasa nifanyeje.
Ila vigezo vyote ulivyovianisha nimevitimiza
Akili yangu ni kwamba ngoja watoto wangu wote waiingie kwenye system nikimanisha wote wako makazini sina wa kusomesha sekondari ila wa mwisho anamalizia chuo sasa nataka nitumie nafasi hii hii nikiwa kwenye hii ofisi nimchomeke halafu na mimi nichomoke.
 
Back
Top Bottom