Ushauri kwa wanaume: Usiahidi ndoa hewa

Ushauri kwa wanaume: Usiahidi ndoa hewa

Kweli mkuu bora kuwa muwazi inakuweka huru zaidi;kwa upande wangu mi huwa nawaambia ukweli nina familia,kama unataka tule maisha poa.lakini sio ndoa.
 
nishajaribu kusema nataka show tu nikaulizwa "unanichukuliaje kwani" nikagundua ukijifanya mkweli hupati kitu
Eeh mzee baba hawa ndugu zetu bila kamba 2 kamba ukijifanya unanyoosha maelezo watakuona siasa zako za maji taka tu!

Lazma uweke kabobo za kutosha ili kuibuka kidedea, ukishaanza kuskia "mmh,,kwelii?" ujue msumari umeshika vizuri kwenye mbao, kazi kwako tu!
 
Eeh mzee baba hawa ndugu zetu bila kamba 2 kamba ukijifanya unanyoosha maelezo watakuona siasa zako za maji taka tu!

Lazma uweke kabobo za kutosha ili kuibuka kidedea, ukishaanza kuskia "mmh,,kwelii?" ujue msumari umeshika vizuri kwenye mbao, kazi kwako tu!
acha tutangaze ndoa tu japo sio kupenda kwetu maana wanatulazimisha wenyewe
 
UKIWA MKWELI UNAKUWA BOYA..MWENDO WA FIKSI..HATA NTAYEMUOA NTAMPIGA FIKSI TU KUWA NIMEWAACHA WA ZAMANI
 
Huyo Malaya ni Muha au wa kanda ya ziwa? Maana wale na watu wa Mbeya haswa Rungwe na Mbozi ndiyo wanaoongoza kwa mazingaombe ya kishenzi ya namna hii.
Muha kudadadeki! Ila nilishafyekelea mbali. Naona maombi yenu yalifanya kazi
 
Muha kudadadeki! Ila nilishafyekelea mbali. Naona maombi yenu yalifanya kazi


Ni bora umemtupilia mbali na kusevu maisha yako maana ungezidi kuwa naye mwisho wa siku ungekuwa zombie wake tu. Waha bwana, si mwanamke si mwanamme yaani hawana afadhali wale....si unamuona Diamond jinsi anavyochezea watoto wa watu na kutembea na nyota zao ila wao hawajijuwi tu wanafikiri wanapendwa kumbe jamaa anawavuna nyota.
 
Sometimes wanawake wanafanya tuwe waongo!.

Nakumbuka kuna demu nilikuwa nikimpa ukweli wa maisha yangu anakataa Na kusema me wakishua!.

Siku alipojua me MASIKINI akaniacha.

Alikuwa Na shoga yake!. Wameshibana
Baada ya shoga yake kujua nineachwa Coz ya Hali yangu
Alinionea huruma Sanaa.so akawa ananipa kampani
Mwisho tukapendanana

Hatimaye tukaoana Na kujenga maisha mazuri!.
Yule Ex wangu mpaka Leo hajaolewa
Kuna kipindi anajuta kwa alilonifanyia

But wanawake MUHIMU kuwa na utulivu!.
Hadithi nzuri hii
 
Shida inaanza pale mwenzako (binti) anapoweka imani na mategemeo makubwa kwako. Yaani anakutambulisha kwa ndg zake, anakuchukulia kama mume mtarajiwa kweli tena kwa unyenyekevu wote. Huyu huwa anaumia sana na ndiye malipo yake yanweza kukupata ukimdanganya si wale malaya wa mjini yaani hata ukimuahidi ndoa haimshughulishi.
Vipi ukigundua huyo aliyeweka matumaini kwako bado ana uhusiano wa kimapenzi na ex wake tena na kidume mwingine zaidi halafu wewe umezaa nae mna mtoto mdogo unachukua uamuzi gani?
emu tatua hili nione hekima yako
 
Habari za mchana ndg zangu!
Jana nimetoa ushauri hapa juu ya dada zangu kuhusu kuwa presentable mbele za wanaume na kuwa na tabia njema katika jamii ili uweze kupata mwenza mwema. Leo nimeona ni vizuri pia nikaongea na kaka na wadogo zangu wanaume ambao hawajaoa ila wanampango huo kwa siku za usoni.

Ndg zangu wanaume kumekuwa na tabia ya sisi kuwa na wapenzi wetu huku tukiwahadaa kwamba tutawaoa. Ni jambo jema kutoa ahadi na kulitimiliza, lakini ni jambo la hatari sana kuweka ahadi ambayo moyoni mwako unajua kabisa unadanganya. Mungu anakataza kabisa juu ya sisi binadamu kuapa kwa jina la Mungu au chochote kilicho juu ya ardhi au chini yake. Lakini biblia pia inakataza kabisa kufunga nadhiri halafu usilikamilishe. Sasa wanadamu wengi wanajua nadhiri katika upande ule wa mtu na Mungu tu ndiyo wenye madhara lakini ukweli ni kwamba nadhiri unaweza kuwa na madhara usipotimilizwa hata kati ya mtu na mtu.

Unapokwenda kwa mtoto wa kike kumtongoza ni vzr kuwa wazi kabisa, kwamba unachotaka ni nini, kama unataka company tu ni vizuri kuweka wazi na kama unataka urafiki wenye malengo ya uchumba au ndoa pia ni vizuri kuweka wazi ili wote muwe na common mind. Kila moja aingie kwenye makubaliano anayoyaelewa ili kuwa tayari kubeba yatokanayo. Lakini hapa pia wasichana wengi wamekosea na wanazidi kukosea hawaulizi kinaga ubaga lengo la mwanaume pale anapotokewa. Wao wanakubali tu halafu mwisho wa siku anapata ujauzito anataka aolewe kumbe mkataba haukuwa wa kuoana. Lakini pia anaweza asipate mimba ila baada ya kuachwa akaanza kulia eti ameachwa kumbe jamaa yeye hakutaka future naye. Ni muhimu wadada nao wakawa makini kujua lengo la mwanaume ili kuepuka lawama za baadaye.

Nikirudi kwenye mada napenda kuwaasa vijana wa kiume kuepuka kutoa ahadi hewa, yaani unaenda kwa binti unamtongoza kwamba muwe wachumba wakati mwingine unamuweka hadi kwako kwa muda kadhaa, binti anakuwa na matumaini makubwa nawe anakutambulisha kwa marafiki zake au ndg zake lakini wewe moyoni unajua kabisa kwamba unafanya usanii na kwamba ama una mke au una mwanamke mwingine ambaye ndiye mchumba wako. Baada ya kuachana na huyu uliyempa matumaini makubwa anabaki analia usiku kucha, wengine hadi wanajaribu kujiua kwa ajili yako. Anashindwa kubeba aibu uliyompa mbele ya marafiki zake, wazazi au ndg zake. Vilio kama hivi hufika kwa Mungu na kwakweli pamoja na kwamba mlifanya uzinzi bado Mungu hawezi kukuacha hivi hivi.

NINI MADHARA YA KUTOA AHADI YA NDOA HEWA.
Madhara yanaweza kuwa ya aina mbali mbali kama ifuatavyo.

Kwanza unaweza kutafutiwa dawa ya kukufanya usiondoke ( dawa ya kumtuliza mume/ mchumba) , haya yanaweza kutokea kama binti amekulia katika jamii za watu wanaoamini katika ushirikina. Binti anaweza kufanya hivi bila kujua madhara ya madawa hayo, mwisho wa siku ukapata madhara na unaweza hata kufa. Kuna mifano kibao katika jamii zetu yanayofanana na haya
Pili unaweza kuuwawa kabisa, yaani binti mwenye roho mbaya anaweza kwenda kwa wafumu wa dunia na kukumaliza kabisa. Lengo hapa ni ili wote wawili wakose, yaani yeye na yule mwingine ambaye hasa ndiye unampenda.

Tatu unaweza kufanywa chochote kishirikina na kupata madhara mengine kama kufanywa nyoka wa kibisa, kufanywa kichaa au kubaribiwa kazi kwa namna za kiganga na kichawi au hata kupewa ugonjwa usiotibika.

Nne sote tunajua what goes around comes around (karma) inaweza kukufuata na kukushughulikia kwa namna ya ajabu sana. Unaweza kujikuta mambo yako hayaendi sawa ukajiuliza ni nini kinatokea kumbe machozi ya wasichana ndiyo yanakutesa.

Lakini jambo lingine, haya mambo yanaweza kufuata uzao wako yaani mabinti zako nao wanweza kujikuta katika taabu hii uliyowapa mabinti za wengine. Ukatesa watoto wako kwa matendo uliyoyatenda wewe huko nyuma.

Jambo la mwisho ni kwamba napenda sana vijana tuwe wa kweli kwa dada zetu maana hata ukikataliwa na huyu kwasababu umesema ukweli yupo atakayekukubalia ambaye yeye hapendi kudanganywa. Hata hivyo madhara ya kusema ukweli ni mdogo sana kulinganisha na madhara ya kusema uongo. Kuwa mkweli hata kama ukweli huo utakugharimu, kumbuka dhambi ni dhambi na usifanye haya ukadhani uko safe.

Nimesema madhara ambayo mengi yameegemea kwenye mambo ya kiafrika kwasababu tunaishi afrika na uchawi ni sehemu ya maisha yetu. Halafu nimeona haya mambo kwa ndg zangu na jamii inayonizunguka watu wakifanywa vibaya na wasichana ambao waliwaacha huku wasichana hao wakilia machozi ya damu.

Mwenye masikio na asikie msije sema hamkuonywa! (tunauguza)

Kindi
Mkuu umemaliza kila kitu. Wa kuskia na askie
 
Back
Top Bottom