Ushauri Kwa Wanaotafuta Kazi

Sir Hemedi

Senior Member
Sep 28, 2016
112
120
Kama unatafuta kazi na umeitwa katika interview au unaandika proposal ili upate kazi, zingatia sana mambo yafuatayo.

1. Usielezee shida zako, jitahidi uonyeshe jinsi gani unaweza kuisaidia kampuni, taasisi au shirika unaloomba kazi katika kufikia malengo yake. Kuna baadhi ya watu wanapoomba kazi huelezea shida zao na kufikiri kuwa watahurumiwa ili wapatiwe kazi, Usifanye hivyo utakosa kazi.

2. Kama unaweka experience za kazi ulizofanya Usiweke nyingi hadi zikamtia wasiwasi mwajiri.
Kwa mfano ndani ya miaka mitano unaweka kuwa umeajiriwa katika taasisi zaidi ya tatu. Hii inaweza kumpa mashaka mwajiri kwani inaashiria kuwa haudumu kazini na hatimaye unaweza kukosa kazi.

3. Jiamini, onyesha kuwa una uwezo wa kufanya kazi unayoiomba, epuka maneno labda, nitajaribu, na mengine yanayofanana na hayo.

Nina hayo machache, yazingatie.
 
5. Zingatia muonekano wako unapoenda kufanya interview eg. Ukienda umenyoa kihuni,suruali modo,umepiga mlegezo jiandae tu kukosa kazi
Hapo kwenye modo wengi watakosa kazi maana siku hizi vijana wengi wanavaa taiti mana hata hizo modo zimepitiliza. Je kwa hali jinsi ilivyo ya uvaaji wa hizo modo tutapata kweli kazi.
 
5. Zingatia muonekano wako unapoenda kufanya interview eg. Ukienda umenyoa kihuni,suruali modo,umepiga mlegezo jiandae tu kukosa kazi
suruali modo dah! siku hiz suruali zile za mtepweto hazipatikani madukani ,kadet zote ni model hapo sijui tufanyeje........
 
Back
Top Bottom