Ushauri kwa wana ndoa hawa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri kwa wana ndoa hawa

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by PEA, Feb 23, 2011.

 1. PEA

  PEA Member

  #1
  Feb 23, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni ndoa changa ina miaka mitano tu, maisha yao mazuri kwa Baba na Mama wote wanafanya kazi nzuri tu na kimsingi ndoa yao ina amani na utulivukwa kiwango kikubwa.
  Tatizo lao kubwa ni moja tu. Mama anataka anataka jina lake lionekane katika kila kitu kikubwa kinachonunuliwa au kumilikiwa na familia mfano hati ya kiwanja iandikwe jina lake badala ya jina la mumewe. Kwa mujibu wa Mama huyo haoni tatizo kwa jina la mumewe kutoonekana mahali popote. Hii kwa kiasi kikubwa imepelekea ugomvi wa hapa na pale ndani ya familia. Ikumbukwe kwamba baadhi ya makubaliano hufanywa na Mkewe pekee jamaa akiwa safari

  Je kuna madhara yoyote kwa jina la mmoja wa wana ndoa kutoonekana katika umiliki wa mali za pamoja?

  Je, kuna logic yoyote kwa mwanamme kutokubaliana na utaratibu huu wa mkewe?

  Je, kwa mila na tamaduni za makabila mbalimbali ya Tanzania nani ni msimamizi au kiongozi wa familia?

  Je, sheria ya ndoa ya mwaka 1971 inafafanua vipi utata uliopo hapa?

  Nawakaribisha kwa maoni, michango na ushauri
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Feb 23, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kwanini wasiweke majina yote mawili kuondoa utatà????
   
 3. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #3
  Feb 23, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Hiyo ndo iko matatani sana ha mwanamke anataka jina lake what do you mean??? Aisee kuna walakini hapo.

  Waandike Julias Maganya and Jane Mtakuja mambo yaishe
   
 4. PEA

  PEA Member

  #4
  Feb 23, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mume anataka iwe kama ulivyoshauri wewe na Lizzy, wanakubaliana ikitokea kasafiri akikrudi anakuta yale yaani owner Jane Mtakuja, kama kunahitajika ushahidi Mumewe ndo anakuwa shahidi
   
 5. papag

  papag JF-Expert Member

  #5
  Feb 23, 2011
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 688
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  nimesahau kunywa thupu....nitarudi baaadaeee
   
 6. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #6
  Feb 23, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kwahiyo mume anataka majina yote mke anataka lake tu???Mbona hapo pagumu...usikute anataka mume akienda siku akirudi akute hamna kitu tena!!Na hatokua na haki ya kudai kama tangu mwanzo vimeandikishwa kama mali za mwanamke!!Atafute mwanasheria waandikishe majina yote mawili....hapahitajiki discussion wala sijui makubaliano!!!
   
 7. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #7
  Feb 23, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Aisee hiyo ndoa inamushkeli lakini huyo mwanaume anamuachiaje mwanamke anunue kila kitu wakati hayupo?? Mkishaoana si mnakuwa mwili mmoja na mnasema "Gari letu, nyumba yetu, shamba letu nk" Au wao kila mtu gari yangu, nyumba yangu, shamba langu.

  Mkioana bana kuna mambo mengi hata kama mwanaume/mwanamke ndo anatoa pesa ya kufanyia jambo mwenzake lazima atachangia hata kwa mawazo, nao ni mchango.
   
 8. t

  the mkerewe JF-Expert Member

  #8
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 232
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tamaa ya mali itawatokea puani waacheni wararuane vizuri kwani hawakusomana kabla ya kuoana?
   
 9. LeopoldByongje

  LeopoldByongje JF-Expert Member

  #9
  Feb 23, 2011
  Joined: Apr 28, 2008
  Messages: 373
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kisingi wanatakiwa wafahamishane kwa kila dili ambayo familia inafanya. Haina tatizo kumuandikisha yeyote baina ya mke au mume. Ila kwa masilahi ya Familia Kumuandikisha Baba mwenye mji ni bora zaidi kwani anaiwakilisha familia nzimayaani Yeye baba, Mkewe na watoto ambao ndiyo familia. Lakini kwa kisa hiki huyo Mwanamke ana agenda ya siri na naona muda si mrefu atamtoa uhai huyo bwana. Mshauri huyo bwana asimushirikishe mkewe kwenye masuala ya msingi, maana mke ameishapoteza uhalali kwa kuingia maelewano na watu wengine bila kumshirikisha mumewe na hasa pale anapoacha muwewe yu safari akafanya mapatano bila hata ya ridhaa ya mumewe. Huyo mama wa kuogopwa kama ukoma. KIFO HICHO CHA MCHUNGULIA HUYO BWANA.
   
 10. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #10
  Feb 23, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Utulivu na amani ya hiyo ndoa ni upi?
   
 11. PEA

  PEA Member

  #11
  Feb 23, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimewasoma waungwana. Hata mimi nimejiuliza sana nikakosa majibu. Labda hapa tunaweza kuwaokoa wenzetu hawa
   
 12. PEA

  PEA Member

  #12
  Feb 23, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimesema kwa kiwango kikubwa, tatizo ni hilo la umiliki wa mali.Japo nakubaliana na wengi kwamba hakuna amani hapo
   
Loading...