Mkuu MAKOLE vipi kuhusu suala la dress code kwa ujumla kuanzia hostel hadi lecture rooms, je pens,raba na open shoes a.k.a masai.
MAKOLE eti ni kweli wireles internet inapatikana had maeneo ya hoshel[ndan ya hostel] and vp kuhus people walifany fresh wanabakishwa kufundish hapo?
Ukiwa class baadhi ya college na baadhi ya wahadhiri hawataki kuona pens wala kapelo. Masai na open shoes ruksa ila ndala mimi sijawahi kuziona na mwenyewe pia huwezi kuvaa ndala kwenye mihadhara na semina. Kwa hostel vaa chochote uwezacho, sio issue. Ila kwa Social usivae hovyo popote pale, ukikutwa ni msala. Dressing code labda wafanye kutoa general ila kwa sasa kila college inazo taratibu zake. Wakati mwingine hata kwenye Pepa au test ukikutwa na pensi wanakusepesha. Kwa Coed, ni marufuku kuvaa t shirt zenye maandishi ukiwa library, na wanawake walikuwa wanazuiwa kuvaa suruali hasa za jeans ukiwa library. Hta hivyo utaratibu huu kwa coed ni mgeni kwa kuwa waliuanzisha mwishoni mwa semesta iliyopita. Nadhani umenielewa mkuu .
nime kuelewa ipasavyo mkuu thanks a lot, mungu akujalie mafanikio zaidi. Nikipata boom ntakugawia kidogo yata ya vocha kwa kupoteza muda wako ili kutusaidia
Makole tunashukuru kwa kutupa feedback za hik chuo,ila ningependa kujua et hii coz ya mining engneering inamdagan tangu ianzishwe hapo chuon na sisi tunaoichukua tutafkia wapo tutakapo fika chuon?naje et maprincples huwa wanaishi maeneo ya chuo au mbal na chuo?nisaidie kaka.
Samahan kaka makole naomba unipe website ya Coed kama ipo niweze kupitia mambo fulan
so ata room mate mnapangwa;;;no choice;;;;;;;
Unaweza kuchagua kukaa na mwenzako, ingawa ni lazima muwe college moja, ila si lazima muwe program moja. Ukiwahi uende kwenye block ulilopangiwa sasa hapo maongezi na mawarden yanahitajika. Hatakubali hivihivi hadi umchomee hindi kidogo ( nadhani unaelewa maana ya kuchoma hindi)
Makole, hivi ATM's zipo karibu na colleges au ndo mpaka kitu cha mjini?
kontena la mama kikwete, uwe muwazi makole, wanafunzi full kusex, full kuoana, full kuachana, full kuumizana moyo, wengine pombe, watu bwana, kuna wakati wajasi walikuwa wakiokota mizoga vichakani. wanaaboti wanaambiwa kwa kutupa hakuna bebeni. Udom kwa asieyeijua ataisikia ni chuo kikuu kikubwa na pale kilipo bado sana.
Makole toa ushauri hapo, nimependa jinsi unavyo asa jamii kizazi kipya udom, na jinsi unavyofloo hata mimi nimeshindwa.. Wewe unafaa kuwa kiongozi...na mungu atakuona mkuu
Kila college inazo ATM za NMB na CRDB, aidha, kuna sehemu zipo bank yz CRDB ikiwa na full operation na nmb ndo wanakamilisha jengo lao, huenda tayari linafanya kazi. Mara kwa mara benk za mjini wanagoma kuhudumia wanachuo kwa madai kuwa wakafanye transaction chuoni.
kwa hiyo kwa ambao hatuna account tunaweza kufungulia ndan ya chuo bila kwenda town?