Ushauri kwa vyama vyote:CCM,CHADEMA,CUF,NCCR,TLP ,UDP,NLD,DP,CCK,ACT na vinginevyo

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Tafadhalini sana someni hapa. Msiishie kuwaandaa makada/makamanda/wanachama wenu kulinda kura. Kila mmoja wenu,kwa nafasi yake, yampasa kufanya kampeni ya kutosha kuhakikisha watanzania wenye sifa stahiki wanajiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura. Uchaguzi utanoga kukiwa na wapigakura wa kutosha.Uchaguzi utanoga na mshindi kuheshimiwa,mamilioni ya watanzania yakipiga kura kuchagua viongozi wao hapo Oktoba. Vyama visitegemee 'simple majority' itakiwayo kwenye Katiba ya sasa.

Viongozi na wanachama tuhamasishane na tuhamasishe wengine kujiandikisha. Hakika nawaambia,kujaza watu wasiopiga kura mikutanoni si kipimo sahihi ha demokrasia. Kusomba na kuswaga washangiliaji pia si kipimo sahihi. Watanzania wajae kwenye Daftari la Kudumu laWapigakura na wamiminike vituo vya kupigiakura Oktoba. Hapo,tutaiona demokrasia na kumchagua tutakaye kama Rais,Mbunge na Diwani bila mawaa. La sivyo,kumi tu watatuchagulia viongozi wetu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Umenena vyema Mzee Tupatupa,ila wape shule na kwenye chama tawala kwamba WIZI wa KURA sasa basi!Tunahitaji HAKI tu,na pia usiache kupitia NEC ya Lubuva mwambie asiuchagulie VIONGOZI..............

Na mwisho kabisa mwambie Shemeji asifanye alichoamua kukifanya ataleta chuki na vurugu.....Atuachie Makanisa yetu,hata kama hayafanyi Auditing,sadaka ni yetu siyo mali ya serikali.Kwani pilipili ya shamba inamuashiani?

Haya tu Mzee wangu.
 
Mzee Tupa Tupa next time ongeza na hili kuwa Kila Chama Cha Siasa kitakachopanda Jukwaani Vihubiri Tanzania kwanza, vitamke wazi wazi kuwa Tanzania kwanza na mengine baadae, Vitamke kwamba rasilimali zote ni za watanzania wote na kwamba Cheo kiwe ni dhamana.

Vitamke kuwa vitatangaza sera na sio kushambulia watu/individuals. Vitamke kwamba vitaelinda Tanzania hata baada ya vyama na ufuasi wa vyama kufika kikomo. Vitamke wazi kuwa haviungi mkono uwindaji haramu wa Wanyama pori na Uuwaji wa Albinos.

Ni hilo tu
 
huyu mzee kwa busara hajambo ivi kwa nini ccm watu Kama hawa wasipendekezwe kugombea urais?

Mkuu jme,Urais una wenyewe.Mimi ni Mzalendo-sina mali!

Mzee Tupatupa
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: jme
Back
Top Bottom