Wabunge wa UKAWA,mara baada ya kula kiapo cha ubunge,kazi yenu ya kwanza na kwa umoja wenu iwe ni kusimamia mambo yafuatayo ndani ya Bunge.
Tume Huru:Hili jambo nawashauri liwe ni agenda yenu ya kudumu ndani ya Bunge na mkiona serikali inasitasita kuleta mswaada wa marekebisho wa undwaji wa Tume hii pelekeni hoja binafsi hata kams itakataliwa.
Matokeo ya uraisi kuhojiwa Mahakamani:Hii nayo iwe ni agenda yenu ya kudumu na msikubali kurudi nyuma.
Sheria ya Uchaguzi:Muitake serikali ilete Bungeni Muswaada wa Marekebisho wa Sheria hii katika kifungu/vipengele vinavyowataja/kuwatambua Wakurugenzi wa Halmashauri na Watendaji wa Kata kama maafisa wa Tume ya Uchaguzi.Hawa watu baadhi yao ni chanzo cha matatizo ya kuvurugika kwa uchaguzi katika maeneo yao.
Serikali ikisita kutekeleza,pelekeni hoja binafsi bungeni mkilenga kuifanyia mabadiliko sheria hiyo hata kama walio wengi watakataa ila mtakuwa mmetimiza wajibu wenu kabla ya kuchukua hatua nyingine nje Bunge kupitia Umoja wa Vyama vyenu(UKAWA).
Viongozi wa UKAWA,endapo mambo haya yatakataliwa,kamwe msikubali kushiriki katika uchaguzi wowote ule ujao kwani inatosha na sasa tuseme "yatosha".
Huu ndio wakati muafaka wa kupigania haya kwani bado watu wana kumbukumbu nzuri za nini kimefanyika katika uchaguzi wa mwaka huu kulikoni kungoja muda upite na watu wakawa wamesahau na hoja zikakosa nguvu.
Mnapaswa kutambua kuwa wafuasi wengi wa mabadiliko wamekatishwa tamaa na huu uchaguzi na bila marekebisho hayo wengi wao hawatapiga kura katika uchaguzi ujao.
Hatari kubwa ya wafuasi wa vyama vya upinzani kukata tamaa ya kupiga kura ni kutoa fursa kwa chama tawala kushinda kirahisi kwani wafuasi wa CCM wao watajitokeza kwa wingi ili hali wa upinzani watapungu na hapo tutakuwa tumeshindwa asubuhi ya siku ya uchaguzi ujao na zingine zitakazofuata.
NB:Uchaguzi si lazima ufanyike kila baada ya miaka 5 kama Katiba inavyoelekeza kwani kuna mambo yakitokea yanaweza kupelekea uchaguzi kufanyika kabla ya muda huo kupita hivyo hakuna muda wa kupoteza kwani hakuna aijue kesho.
Tofauti na hapo,tutaendelea kuwa wapinzani daima.
Hakika kama sheria hii na haya hayatabadilika basi hata mimi nikijaliwa uhai sitapiga tena kura.Ni hali halisi na hujuma nyingi tumeshuhudia ikiwa ni pamoja na masanduku na kura kukamatwa na kupotelea mikononi mwa polisi.Wakurugenzi kufanya figisu nyingi sana na kuhatarisha amani.
Magufuri kaa ukiamnini kuwa umeingia madarakani kwa goli la mkono na utakuja kutambua ubaya wa Goli la mkono huko mbele.
Nina machungu makubwa sana na sheria hii mbovu ya serikali hii.