Ushauri kwa tuliowapa dhamana ya usalama wa Tanzania

UFUNUO WA TANZANIA

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2013
Posts
471
Reaction score
166
Ushauri huu umwendee Rais wangu mpendwa J.M Kikwete, Said Mwema, Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Viongozi wa juu wa Polisi, Magereza, Usalama wa Taifa na taasisi ya Ujasusi Tanzania:

Nimesoma mambo ya usalama kidogo wakati sipo Tanzania na kozi mojawapo ni Psychology of Intelligence Analysis katika kozi hii kuna topic moja nilijifunza ambayo ni Strategies for Analytical Judgement Transending the Limits of Incomplete Information na nyingine ambayo ni Biases in Perception of Cause and Effect.

Dhamira yangu si kusema nimesoma nini bali ni kuweka msingi wa hoja yangu.

Nimetathmini hali inavyoendelea katika nchi yetu na kwa kuwa nina ujuzi katika baadhi ya maeneo naomba nitoe ushauri ambao kama na wenzangu katika safari ya mafunzo yenu mlisoma hizo mada nilizoziainisha mtanielewa vizuri.

SABABU ZA KUTOA USHAURI
1. Kujirudia rudia kwa Matukio ya Kuuawa au/na kuteshwa kwa waandishi wa habari na wananchi wengine wengi wa Kawaida
2. Milipuko ya Mabomu kule Arusha
3. Biashara ya Dawa za Kulevya
4. Kukithiri kwa Rushwa na Ufisadi (e.g utata wa Kifo cha Balali)
5. Uwajibikaji mdogo wa Viongozi wa Serikali

USHAURI NI KAMA UFUATAVYO:
Najua wahusika mna taaluma na maeneo mnayoyaongoza lakini sitaki kuamini kuwa imeshindikana kutumia taaluma zenu kuwahudumia waTanzania ipasavyo. Najua wengi huenda wamezolewa na upepo wa mafisadi na wala rushwa wakubwa wa nchi hii na hivyo kukaribia kuwa bendera kufuata upepo ingawa sitaki kuamini kuwa hili limetokea.
1. Naomba viongozi wa Usalama tuwe wakweli kwa waTZ kama hatujathibitisha taarifa fulani za kiusalama si vyema kuwataarifu wa TZ. Ukweli nusu ni sumu kali sana tukiwa wawazi juu ya maendeleo ya uchunguzi fulani tutajenga imani kwa wananchi wetu Lakini kwa sasa tumeipoteza kwa kiwango kikubwa.
2. Naomba tusipindishe ukweli kama viapo vyetu vinavyotuagiza. Hata kama kwa kufanya hivyo tutaharibu maslahi ya watu wachache tuweke taifa kwanza na tuseme kweli daima
3. Tutumie weledi wetu katika utaalamu tuliosomea. Tusiendeshwe na watu wachache ambao wanataka kujinufaisha kwa maslahi yao, familia zao na marafiki zao.

Haya matatu yakizingatiwa kwa umakini angalau tutabadilika namna ya kufanya kazi. Najua miongoni mwa viongozi hawa tayari wametumbukia kwenye lindi la sababu za ushauri huu lakini wapo pia ambao bado ni wasafi na kilio chao ni kuitetea Tanzania.
Naomba vyombo vya usalama tujisahihishe bado hatujachelewa.

cc: Mangula, Nape, Mwigulu, Slaa, Mbowe
Bc: Mkapa, Wassira, Sefue, Lowassa, Chenge
 
wewe inaonekana umesomea mitaani hiyo taaluma na acha kupotosha watu kwa kujifanya unafahamu masuala ya ulinzi. Upi weledi wako hapo? TATIZO WATU WENGI MNAONGOZWA NA HISIA BADALA YA UHALISIA. Pole sana.
 
Mkuu hapo ni nini kilicho kuudhi?...mbona nyinyi hamtoi ushauri wowote chanya pamoja na kuwa mmesomeshwa kwa fedha za taifa hili na kupewa dhamana kubwa?.....Mtaendelea kushabikia na kuwapigia makofi watu wanaoliweka taifa hili katika mashaka kwa kuwa tu nyie mashabiki wa ccm.
Mkuu kuwa mtulivu lete hoja sio kutoa maPOVU
 
Kwanza ni usalama wa taifa, Kuna haja haraka sana kuangalia lengo kuu la chombo hiki, kijutathmini na kuboresha. kama ni kweli chombu hiki kimethubutu kutumiwa kisiasa basi kuna hatari kubwa ya taifa hili kukosa amani huko mbeleni. We dont need to reinvent the wheel, kuna vyo vingi tu duniani ambavyo vinafanya kazi kwa uzalendo wa hali ya juu, bila kujali itikadi yeyote na vina ufanisi mkubwa sana. Umesema kitu muhumu sana, mfano biased surveillance report, inaweza kumyumbisha hata Raisi wa nchi. Kuweni makini na tumikieni watanzania, sio kundi la watu fulani.
 
Ushauri huu umwendee Rais wangu mpendwa J.M Kikwete, Said Mwema, Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Viongozi wa juu wa Polisi, Magereza, Usalama wa Taifa na taasisi ya Ujasusi Tanzania:

Nimesoma mambo ya usalama kidogo wakati sipo Tanzania na kozi mojawapo ni Psychology of Intelligence Analysis katika kozi hii kuna topic moja nilijifunza ambayo ni Strategies for Analytical Judgement Transending the Limits of Incomplete Information na nyingine ambayo ni Biases in Perception of Cause and Effect.

Dhamira yangu si kusema nimesoma nini bali ni kuweka msingi wa hoja yangu.

Nimetathmini hali inavyoendelea katika nchi yetu na kwa kuwa nina ujuzi katika baadhi ya maeneo naomba nitoe ushauri ambao kama na wenzangu katika safari ya mafunzo yenu mlisoma hizo mada nilizoziainisha mtanielewa vizuri.

SABABU ZA KUTOA USHAURI
1. Kujirudia rudia kwa Matukio ya Kuuawa au/na kuteshwa kwa waandishi wa habari na wananchi wengine wengi wa Kawaida
2. Milipuko ya Mabomu kule Arusha
3. Biashara ya Dawa za Kulevya
4. Kukithiri kwa Rushwa na Ufisadi (e.g utata wa Kifo cha Balali)
5. Uwajibikaji mdogo wa Viongozi wa Serikali

USHAURI NI KAMA UFUATAVYO:
Najua wahusika mna taaluma na maeneo mnayoyaongoza lakini sitaki kuamini kuwa imeshindikana kutumia taaluma zenu kuwahudumia waTanzania ipasavyo. Najua wengi huenda wamezolewa na upepo wa mafisadi na wala rushwa wakubwa wa nchi hii na hivyo kukaribia kuwa bendera kufuata upepo ingawa sitaki kuamini kuwa hili limetokea.
1. Naomba viongozi wa Usalama tuwe wakweli kwa waTZ kama hatujathibitisha taarifa fulani za kiusalama si vyema kuwataarifu wa TZ. Ukweli nusu ni sumu kali sana tukiwa wawazi juu ya maendeleo ya uchunguzi fulani tutajenga imani kwa wananchi wetu Lakini kwa sasa tumeipoteza kwa kiwango kikubwa.
2. Naomba tusipindishe ukweli kama viapo vyetu vinavyotuagiza. Hata kama kwa kufanya hivyo tutaharibu maslahi ya watu wachache tuweke taifa kwanza na tuseme kweli daima
3. Tutumie weledi wetu katika utaalamu tuliosomea. Tusiendeshwe na watu wachache ambao wanataka kujinufaisha kwa maslahi yao, familia zao na marafiki zao.

Haya matatu yakizingatiwa kwa umakini angalau tutabadilika namna ya kufanya kazi. Najua miongoni mwa viongozi hawa tayari wametumbukia kwenye lindi la sababu za ushauri huu lakini wapo pia ambao bado ni wasafi na kilio chao ni kuitetea Tanzania.
Naomba vyombo vya usalama tujisahihishe bado hatujachelewa.

cc: Mangula, Nape, Mwigulu, Slaa, Mbowe
Bc: Mkapa, Wassira, Sefue, Lowassa, Chenge

hapa kilichokukera nini hasa mbona unatokwa povu bila sababu.
 
Kaa ukifahamu ndugu kwamba penye ufisadi na rushwa iliyokolea, professionalism na ethics zake zote hutupwa baharini.Unalosema, vijana wa mtaani huita:"Kumpigia mbuzi gitaa"
 
Back
Top Bottom