Hotuba ya Mh Sumaye imejaa maneno yenye busara sana na ukomavu mkubwa wa kisiasa. Tunahitaji chama chenye Demokrasia pana chenye muundo wa kitaasisi na ambacho ni mbadala wa CCM ambao wananchi watakiamini na kukiona mbadala wa CCM.
Hivi vilivyopo sasa ni mali za watu na vingine ni mashamba darasa na vingine ni vijiwe vya kuganga njaa. Siasa inaathiri maisha ya watu hatuwezi acha yakawa mashamba darasa wala vihenge vya watu. Tunahitaji corporate bodies zitakazo shindana na CCM.
Tanzania na dunia ya sasa haihitaji wanasiasa wa kukimbizana na FFU wakuchimbana mikwara na dola. Tunataka chama chenye kushauri panapohitaji maboresho, kuonya palipo na mapungufu na kukemea palipo na maovu. Lakini kisifu na kutia moyo mema yanapofanyika. Kiwe chama chenye uwezo na nia ya dhati ya kupokea kijiti mkimbiaji wa awali anapohitimisha ngwe yake.
Mh Sumaye ili kuleta uhai katika siasa za zetu na kukamilisha nia yako njema ni vyema ukaanzisha chama kipya cha siasa chenye maono na malengo uliyokusudia.