Ushauri kwa Simba, kama inatwaka itwae kombe la CAF iwekeze kwenye beki na kipa wa ukweli.. Good defence = championship

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
8,822
33,526
Habari wadau..

Nimesikia simba wanamtaka morrisson.. nikashangaa sana.. simba imesajili watu wengi wazuri mbele ila bado inahangaika..


Kwa uzoefu wangu wa kutazama caf champions league nimejifunza mengi sana..

Mpira wa africa una tofauti kubwa na wa ulaya.. ushindani wa caf champions league ni mkubwa kuliko hata wa uefa champions league... sema africa hakuna hela tu ila timu zinatwaa taji hilo kwa mbinde sana.. africa kushinda ama kupata sare ukiwa away ni kazi kubwa kweli kweli.. timu zinazotoa hata sare ugenini ndio zinazotwaa mataji..

Simba imebarikiwa tajiri mwenye hela kuamua kuwekeza hela zake. Hiyo ni bahati kubwa sana..

Kama simba inataka itwae taji hilo nguvu kubwa iwe kwenye beki line ya ukweli.. na kipa wa uhakika maana game za mtoano away lazima ushambuliwe sana hata uwe na timu kali vipi.. na watakaokusaidia usitolewe ni mabeki wa ukweli na kipa wa ukweli...kuna msemo unasema good offence win matches but good defence win championships

Naonaga mamelodi dennis onyango anachomwaga mpaka masindano ya ganzi ili game za away akae yeye golini.. maana wanajua mziki ni mnene ukiwa ugenini africa hawa makipa na mabeki miili midogo midogo, wenye uzembe wa kijinga na maboko mengi hawafai
 
Tanzania bado sana kwenye mpira wa miguu ,hizo timu zote wamewekeza kwenye siasa mimi nitaanza kuwa mshabiki 2099
 
Beki simba tatizo kama sio uwezo binafsi wa Manula pia simba watafute kocha

Simba hakuna beki ya kuwazuia mazembe wasipate goli lubumbashi, simba hakuna beki wa kumzuia waydad asipate goli mjini casablanca, navyosema beki za ukweli inabidi uelewe.. usiongelee beki za kuzuia mashambulizi ya yanga au ya kagera sugar.. caf champions league ukiwa away huwa unashambuliwa kama mwizi.. sasa beki za kuunga unga lazima zichoke jasho jingiii... unajikuta unapigwa magoli.. tazama mazembe ama mamelodi wakiwa ugenini jinsi beki zake na kipa wanavyokaza

Simba isajili mabeki wenye miili mikubwa.. warefu na football iq ya hali ya juu... wakiwa ugenini wawe wanakichafua kweli kweli.. angalau simba iwe ina uhakika wa kupata hata sare away kwenye mtoano
 
Tatizo mabeki wa hivyo dau lao $400K na kuendelea..mshahara $20,000 per month Mo anaweza kutoa hizo pesa???
 
Back
Top Bottom