Ushauri kwa serikali yangu

Ushauri kwa serikali yangu

Chato tena

Member
Joined
Jan 17, 2021
Posts
24
Reaction score
50
Pongezi kubwa kwa mhe Rais wetu kujenga kilometa nyingi bila kufanya maonyesho ya bila mimi msingepata barabara.
pia pongezi nyingi kwa Raisi aliyepo kwa kundelea kuchapa kazi ambayo matunda yake yameonekanana yanaendelea kuonekana. Pamoja na yote hayo hatuwezi kukosa changamoto.

Kuna maswali mengi sana nimejiuliza jinsi ya viongozi wetu wanapokabidhiana Nchi pindi ya kiongozi anapokamilisha awamu yake ya uongozi. Mfano katika makabidhiano lazima mkabidhiane kila kitu. Mfano miradi iliyokamilika katika awamu yako na pia inayoendelea, kwa bahati nzuri nimefika katika mkoa wa kigoma nimekuta miradi alioiacha the best president in Tanzania Mr Jakaya kikwete.

Imetelekezwa mfano ujenzi wa bandari ya nchi kavu katosho umesimama na sijui kama utaendelea tena, upanduzi wa bandari ya kigoma upande wa kibirizi nao wameishia kuweka mabati na na kuzungushia uzio hakuna chochote kinachofanyika.

Umaliziaji wa barabara ya kigoma tabora kuna vipande kama vitatu havijakamilika.Maajabu ya serikali inayochapa kazi.Mfano 45km za kutoka Urambo kwenda kaliua imejengwa kwa muda wa miaka zaidi ya 6 yaani kuanzia 2015 mpaka leo 2021 na bado ujenzi unaendelea.Kandarasi alipewa mzawa SAMOTA ujenzi unaendelea lakini baada ya miaka 5 ijayo barabara iyo itakuwa hoi kwani inajengwa chini ya kiwango sijui Tanrods mkoa wamellala au ndo mambo ya bahasha yakaki zinatembea.

Pia kuna kipandea cha kutoka sawima mpaka unakaribia maeneo ya nguruka.Huko ndio ni hatari sijajua kama halimashahuri ya kaliua na uvinza zinajua hilo kwani barabara ina makorongo ya kutosha barabara ni mbovu na hizi halmashauri 2 zimelala zimewaachia watu wa mabasi hususani kuchonga barabara wanajichanga wamiliki wa mabasi kisha wanachongesha.Lakini ni sehemu inayoongoza kwa kuwa na mageti kuna mkandarasi yuko pale anazaidi ya miaka 4. Haja tengeneza hata robo kilometa ya rami.Nahisi nae yule atakuwa mzawa kama samota.

Kutoka uvinza kwenda mpk malagarasi nalo ni hatari kama unaharisha inatakiwa uweke pamba kwenye sehemu ya kupimia korona ( kwa mujibu wa kipimo kipya) hii ndio sehemu mbaya zaidi kutoka uvinza kwenda malagarasi kwani hapa kuna mlima mkubwa na njia ni nyembamba. Magari hayawezi kupishana nani sehemu ndefu.

Mfano siku niliopita hapo natoka kigoma tulikaaa zaidi ya maasaaa manne tukisubiri gari liloaribika mbele yetu na ikumbukwe hapa kuna mteremko mkali, basi kama hata serikali inayochapa kazi basi ipatanue angalau hata gari ziweze kupishana hapana Tanrods mkoa wakigoma wanatakiwa kulaumiwa mojakwa moja kwa kukosa kuwa wabunifu katika hili.

Swali ambalo ninalojiuza hivi viongozi wetu wakuu wanapokabidhiana hivi hakuna sehemu ambayo inambana kiongozi kuanzisha miladi mipya kabla ya kumaliza miradi ilioachwa na mtangulizi wake.barabara ya uvinza na malagarasi
 
Mkuu umesahau maneno ya jiwe. Msikilize tena hapa.

Huwa nikisikiliza sauti na maneno ya huyu mtu nabaki najiuliza "hivi 2015 watanzania tulipatwa na mkosi ama laana?
 
Pongezi kubwa kwa mhe Rais wetu kujenga kilometa nyingi bila kufanya maonyesho ya bila mimi msingepata barabara, pia pongezi nyingi kwa Raisi aliyepo kwa kundelea kuchapa kazi ambayo matunda yake yameonekanana yanaendelea kuonekana...
Dah! Sawa. Ujumbe umefika. Ila ujitahidi kuweka maandishi yako katika paragraph. Tumeelewana Mheshimiwa Chato tena?
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Back
Top Bottom