Ushauri kwa serikali ya tano kuhusu elimu yetu

Ushauri kwa serikali ya tano kuhusu elimu yetu

KENZY

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
36,516
Reaction score
89,013
wanafunzi-Tanzania.jpg

Tukianzia awamu iliyopita wamejitahidi kwa kiwango chao ktk swala zima la ujenzi wa shule mbalimbali hapa nchini,hii nikutokana na kwa wkt huo kuwa na uhaba wa shule kwa wkt huo lkn kwa sasa jambo hilo limepungua kwa kiasi chake..
Hivyo ningependelea awamu hii ijikite ktk kuhamasisha utoaji wa elimu bora.. bila hivyo kutakuwa hakuna maana nzima ya majengo yaliyojengwa na yale yote yanayofanyika kuhusu elimu yetu!
tatizo sio kuwa na shule nyingi tu hapana bali kuwa na watu waliokuwa na elimu bora maana hiki ndio msingi mzima wa neno elimu means kuelimika..
hata kama ni kukazia kuwa na shule lkn kwasasa sidhani kama hili linatakiwa kushikwa tena kwa kasi sana ila kinachotakiwa sasa ni kutolewa kwa elimu bora hili ndilo lengo haswa.
nibora kuwa na siraha moja ambayo itakulinda kwa uhakika kuliko kuwa na siraha elfu moja ambazo haziwezi kumdhuru adui! hata sifa ya kuitwa siraha zitakuwa zimepoteza.
 
serekali inachofanya ni kuua elimu

yani goli ni la mita moja wakiona mchezaji kashindwa funga wanaliongeza ukubwa hii inasabàbisha kuwà na vilaza mashuleni mtoto anafaulu kwa kushedi hadi hesabu si usengerema huo angalia na matokeo ya kidato cha pili 2012 walifeli ikabidi wapanue goli mwaka 2013 kutoka 30 mpk 21 kama sio kuzalisha vilaza ñi nini hiko joice ndalichako
 
Hujaeleza namna elimu bora itakavyotolewa ili ionekane ni bora.
 
elimu bora labda raisi atakayekuja ila sio huyu.... vitisho tu ndo anavyoviweza!
 
Hujaeleza namna elimu bora itakavyotolewa ili ionekane ni bora.
sidhani kama maprofesa,wenye phd zao,walimu n.k watashindwa kutokujua ni namna gani elimu bora inavyotolewa ni aibu kushindwa na private schools ila hatuoni sababu lile shipa la aibu limeshakatika!
 
Serikari ya awamu ya tano wanazan mtoto kusoma bure ni elimu bora. Elimu bora inaanza kwa kumthamini mwalimu, kutengeneza mitaala inayokidhi mahtaji ya sasa. Hayo yote yamepuuzwa na wamejikita kutengneza madawat meng na elimu bure afu wanajicfu kwenye media kwamb wanatoa elimu bora.
 
kwa awamu hii kinachoendelea kwenye elimu ni majanga.kwa mfano badala ya serikali kuajiri walimu wa kutosha wa shule za msingi na mtaani wapo. serikali inapanga kuchukua walimu wa sekondari
na kuwapeleka shule za misingi kinyume na wslichojifunza vyuoni. binafsi nawalaumu sana wabunge wetu kwa kutotimiza wajibu wao ipasavyo. pia serikali imeshindwa kuboresha maslahi ya walimu kama kupandisha madaraja yao na kusingizia mafunzo na kinyume na ilivyozoeleka. tumeshuhudia wabunge wakimpongeza waziri kairuki kwa kweli ni bora bunge lingefutwa tu...
 
Niliwaelewa sana Mkapa na JK kwa pamoja na EL wao!!!

Zamani, kwenda sekondari ilikuwa ni kama kushinda Bingo kutokana na uhaba wa shule ambao tulikuwa nao! Ilikuwa ni kawaida kukuta mkoa mzima una shule chini ya 10!!

So, Mkapa na JK hawakuwa na namna zaidi ya kutoa kipaumbele kwenye ujenzi wa shule nyingi zaidi kwa sababu; isingewezekana kuanza kudahiri walimu wengi zaidi na kuwatupa mitaani kwa kuwa hapakuwa na shule za kutosha!!

They did good cuz' baada ya kusambaza mashule nchi mzima; JK akageukia kwenye kudahiri walimu wengi zaidi kwa kuipandisha hadhi Chang'ombe kuwa University na Mkwawa kuwa University College! SUA ambayo ilionekana ni chuo cha kilimo nayo ikapewa hiyo kazi kwa ajili ya Walimu wa Sayansi!!

Tanzania tuna tatizo la msingi... tunakwepa sana masomo ya sayansi hata kama mtoto anasoma shule yenye kila kitu!! O-Level nilisoma shule yenye kila kitu but still out of mikondo 6; ni mikondo miwili tu ndio walikuwa wanasoma Sayansi!!!

Baada ya kuhangaika sana kudahiri walimu wa Sayansi; ndipo ikaja ile special advanced diploma! Bado ikadunda kwavile bado hapakuwa na watu! Ikaja program ya kuajiri wastaafu (walimu wa sayansi); walijitokeza 92 tu Tanzania mzima!

Hapo hapakuwa na namna ndipo ikaanzishwa ile Special Diploma pale UDOM!!

Alipoingia mheshimiwa sana akasema wote hao wana Div IV na hawana sifa ya kuwa chuo kikuu as if pale UDOM walikuwa wanasoma Bachelor!!

Watu tukaone anyway labda ana plan!!!

Ni takribani mwaka sasa umepita tangu Special Diploma in Science Subjects ipigwe nyundo lakini sijasikia ikiwa kuna alternative iliyofanyika hadi sasa!!!

Zile maabara zilizojengwa Tanzania mzima sidhani kama zitakuwa na maana tena!!!

Leo hii wanaona raha kuwahamisha walimu wa sekondari kwenda kufundisha primary kwa vile ni wengi sana!! Wanadhani hao walimu wa arts walishuka toka mbinguni kama mvua bila kufahamu wenzake walikuwa na mipango na ndio maana walizalishwa walimu wengi zaidi kiasi cha kuzidi mahitaji!!!

Haidhuru, tunaambiwa huyu ndie Malaika wetu!!!!!
 
elimu bora labda raisi atakayekuja ila sio huyu.... vitisho tu ndo anavyoviweza!
Huyu ,muheshimiwa hana habari kabisa na elimu yaani kaigeuzia kisogo anacho waza ni kupunguza watumish ili pesa zisitumike nyingi na ni hulka ya kabila lake hupenda kuziona pesa tu zikiwepo hata kama hazifanyi chochote,

kuna uhaba wa walimu wao wanaona dawa kuwashusha wa sekondari wakati mifumo ya ufundishaji ni tofauti sana tena sana na bado huko wanako toa walimu bado kutakuwa na Mapungufu tena maana miaka hii miwili inaonesha idadi ya wanafunzi wanao jiunga sekondari ni kubwa mara mbili ya awali na inazid kuongezeka na bado hata walimu hao wa art ni wachache kwa shule za vijijini , sijui wanafkirije hawa viumbe wa mungu huwa hata siwaelewi huwa hawana uwezo wa kufikiria mbali zaid wao wanafikiri hapo hapo walipo tu

Shule iliyo kuwa na wanafunzi 300 kwa sasa idadi imepanda hadi 487 wakati idadi ya walimu ileile na unaambiwa watakao maliza darasa la saba mwaka huu ni wengi zaid maana yake idadi itaongezeka zaid halafu wao bila akili hawaja fikiria ya mbeleni kweli tanzania tuna laana sisi wananchi na viongozi wetu kwa ujumla.
 
Serikali haina muda na elimu
kama haina muda na elimu hivyo viwanda vitaendeshwaje..?
unajua kila kitu huwa nadhumuni lake na dhumuni kuu ndilo lenye mantik zaidi... dhumuni la kuwepo kwa shule ni ili kujifunza na kupata elimu sasa nikiangalia kwenye nchi yetu naona tuko nyuma! kama mtoto anafika mpk la saba hajui kuandika na kusoma nini dhumuni la kuwepo kwa shule..?
dhumuni la nyumba ni makazi na kuhifadhi vitu lkn itakuwa haina maana kama nyumba hiyo haitakuwa ikikaliwa na mtu wala kuhifadhi vitu.
bila hata kukwepesha elimu ni msingi mkubwa sana ktk nchi ndio maana huwa nasema wazungu hawatuzalau kwaajili ya ngozi yetu,wanatuzalau kwasababu ya ujinga wetu.
 
Back
Top Bottom