Ushauri kwa Saed Kubenea kuhusu kiwanja chenye utata

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,760
Reaction score
165,320
Mh.Kubenea,nakushauri swala hili lisiishie Bungeni tu bali uende pia kwenye Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma kuona kama kiwanja hicho kimeorodheshwa kama mali halali ya huyo unaemtuhumu.

Bila shaka ikithibitika kuwa ni mali yake na taarifa za umiliki wa kiwanja hicho hajaziwasilisha katika Tume hiyo,hilo linaweza kuwa ni kosa lingine na hapa sheria itambana zaidi tofauti na adhabu za kibunge.

Navyofahamu mimi sheria inaruhusu mwananchi yeyote kupewa taarifa juu ya mali za viongozi isipokuwa huruhusiwa kuzifanya taarifa hizo kuwa public.

 
Ushauri mzuri sana na hilo litakuwa ni fundisho kwa watawala
 
Reactions: BAK
Ushauri mzuri ila hi kesi itapinduliwa na nyeupe kuwa nyeusi
Yaani anatakiwa kesho afike ofisi za Tume hiyo maana akikuta taarifa hiyo ameiorodhesha pia itakuwa ni ushahidi mwingine na hata akikuta hajaorodhesha na ikaja ikathibitika kiwanja ni chake bado atakuwa yuko hatiani.Dawa asichelewe.
 
Wana jamvi
Kama mjuavyo Kubenea atatakiwa kwenda mbele ya Kamati kuthibisha tuhuma dhidi ya JWTZ na Mh Mwinyi(MB)

Mbunge wetu amekwepa kujibu hoja au kuthibitisha tuhuma alizo toa bungeni na amekwenda kwenye vyombo vya habari makusudi kupotosha alicho takiwa kuthibitisha!

Mbunge Kubenea anataka akapewa adhabu ionekane kaonewa wakati kiukweli hajathibitisha tuhuma alizo zitoa bungeni dhidi ya Mwinyi na JWTZ
Kwa hisani ya mdau wa Jf tunawakumbusha wananchi na kubenea kuwa!

Ushahidi wa Kubenea hauhusiani na hoja aliyoshtakiwa na mwinyi. Hapa kawapumbuza watu ameacha jambo la msingi ili baadae akihukumiwa ionekane alionewa. alitakiwa kuthibitisha tuhuma dhidi ya JWTZ wakishirikiana na Waziri Mwinyi kuwa ilitoa ardhi kwa kampuni ya Hennang Guiging Industry Investiment kwa ajili ya kufanya ujenzi wa nyumba kwa miaka 40 na si kuhusiana na Mwinyi kumiliki kiwanja. Athibitishe pasipo na shaka ukweli huo .

Karibuni wana jamvi!
 
Ushahidi unaotakiwa no kuhusu JWTZ haya mengine ni kujaribu kutoka kwenye key point ya tuhuma
 
Na ikithibitika sio chake unamshauri nini mkuu?
 
kubenea athibitishe asithibitishe adhabu iko palepale. ile ni kamati ya ccm wala sio ya bunge...
 
Huyu mbunge ni kilaza ukiona anayoeleza hayana uhusiano Na hoja ya msingi anayoshitakiwa nayo
 
Ushahidi unaotakiwa no kuhusu JWTZ haya mengine ni kujaribu kutoka kwenye key point ya tuhuma
Kubenea alitoa tuhuma nyingi lakini waziri Mwinyi alikanusha zote kwa kusema hazina chembe ya ukweli kulingana na maelezo haya ya kubenea kwenye hii clip.

Hii maana yake(kwa uelewa wangu) ni kuwa, madai ya kubenea kuwa anamiliki hicho kiwanja yalikuwa ya uongo pia maana hakukiri kuwa kiwanja ni chake bali alisema madai yote ya kubenea(kulingana na hii clip) hayana hata chembe ya ukweli akimanisha hata umiliki wa hicho kiwanja.Je,ni kweli hata hicho kiwanja si chake?
 
Kubenea hajajibu mashitaka yake. Shitaka kuu lilikuwa kusema uongo kwamba Mwinyi anajengewa nyumba kwenye hicho kiwanja sio kuwa na kiwanja.
 
Watanzania wengi ni mbuzi!! Siasa zimetawala maisha yao kuliko uhalisia wa kitu!!

Mtu ana documents na Plot No na ww umekazania Hoja ya Bungeni!! Kwahiyo hoja ikiachwa, ww kwako ni haki Waziri wa ulinzi kujitwalia sehemu/eneo ya JWZT?
 
Hiyo inaitwa kukaba mpaka penati kudadeki !
 
Watanzania wengi ni mbuzi!! Siasa zimetawala maisha yao kuliko uhalisia wa kitu!!

Mtu ana documents na Plot No na ww umekazania Hoja ya Bungeni!! Kwahiyo hoja ikiachwa, ww kwako ni haki Waziri wa ulinzi kujitwalia sehemu/eneo ya JWZT?
Wewe hujaelewa,kuna watu wanapinga hizo document hivyo cha kwanza ni kuthibitisha hizo document na baada ya hapo kosa la kujitwalia eneo la Jeshi litafuata baada ya kuthibitika kuwa ni kweli ana hicho kiwanja katika eneo la Jeshi.Mi si mtetezi wa hawa jamaa hata kidogo na ninaamini Kubena ataibuka mshindi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…