Ushauri kwa Rais Samia Suluhu

Taifa lipo katika maombolezo makubwa ila kwa wakati huo huo maisha yanapaswa kuendelea.

Ni ushauri tu kwa Mh. Samia endapo ataamua kufanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri, wa kwanza kumtoa awe Waziri wa Afya, Dr. Gwajima. Huyu mama amekuwa kituko kikubwa katika wizara na serikali.

Huyu ndio Waziri wa Afya wa kwanza aliefanya kazi kwa sifa zisizokuwa na tija yeyote katika wizara yake. Alidiriki mpaka kutuonyesha maisha yake ya binafsi wakilishana matunda na mumewe. Ni swala la wakati angetuonyeshea hata ya zaidi yasiyofaa.

Ana kauli za kuhemkwa akiwa anaongea kama vile kila jambo ni ugomvi. Hata akiwa anatoa speech unamuona kabisa kuwa hajatulia kutafakari anachosoma.

Endapo kungekuwa na Wizara ya miti shamba na uganga wa kienyeji, basi hakika ingemfaa hasa lakini sio Wizara ya Afya.
Asiwaache
1. Mwigulu nchemba(hafai,hakufaa wakati wote)
2. Kabudi
3. Jaffo(anafanyakazi kwa kujipendekeza na siyo wajibu)
 
Back
Top Bottom