Ushauri kwa Rais Samia Suluhu

Ushauri kwa Rais Samia Suluhu

Mr Sir1

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2018
Posts
1,787
Reaction score
8,115
Taifa lipo katika maombolezo makubwa ila kwa wakati huo huo maisha yanapaswa kuendelea.

Ni ushauri tu kwa Mh. Samia endapo ataamua kufanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri, wa kwanza kumtoa awe Waziri wa Afya, Dr. Gwajima. Huyu mama amekuwa kituko kikubwa katika wizara na serikali.

Huyu ndio Waziri wa Afya wa kwanza aliefanya kazi kwa sifa zisizokuwa na tija yeyote katika wizara yake. Alidiriki mpaka kutuonyesha maisha yake ya binafsi wakilishana matunda na mumewe. Ni swala la wakati angetuonyeshea hata ya zaidi yasiyofaa.

Ana kauli za kuhemkwa akiwa anaongea kama vile kila jambo ni ugomvi. Hata akiwa anatoa speech unamuona kabisa kuwa hajatulia kutafakari anachosoma.

Endapo kungekuwa na Wizara ya miti shamba na uganga wa kienyeji, basi hakika ingemfaa hasa lakini sio Wizara ya Afya.
 
mama mbabe sana. kakaa kishari shari saa zote
Huyu mama amefanya hii wizara watu wajione kama wamevaapampas kwa kweli mtu wa kusumanha watumishi kila kona mara majambazi mara utateseka kwa kwa utumishi wako uliobakia
 
Kubwa zaidi ni kushindwa kuishauri vyema Serikali kuhusu hatua sahihi za kuchukua dhidi ya janga la COVID-19; ona sasa lilivyomaliza viongozi na wapendwa wetu. Kama alishauri hakusikilizwa alipaswa kujiuzulu!
 
Ninamuombea huyu mama awe jasiri na awe na uthubutu. Asichekee manyang'au.


YESU NI BWANA
... kabisa; akatende ndani ya wigo wa kikatiba na kisheria vikamuongoze katika utendaji wake. Ateue washauri wazuri kuanzia waziri wa katiba na sheria, mwanasheria mkuu wa serikali, na maeneo mengine.
 
Mimi namshauri asitende kama yule aliyesema "nilisukumiwa huko nikawa raisi"
 
... kubwa zaidi ni kushindwa kuishauri vyema Serikali kuhusu hatua sahihi za kuchukua dhidi ya janga la COVID-19; ona sasa lilivyomaliza viongozi na wapendwa wetu. Kama alishauri hakusikilizwa alipaswa kujiuzulu!
alitoa ushauri kuwa watu wafanye mazoezi, wale matunda na kujifukiza. Kama vile haitoshi, akajipiga blanket na mumewe mbele ya kamera za waandishi wa habari ili dunia yote ione. In short huyu mama amepwaya kwenye hiyo wizara kupita maelezo.
Yani kila alichokikosa kwenye utendaji alikifidia na maneno ya shombo na kutaka kumfurahisha aliyemteua, kusahau ya kwamba ana wajibu kwa wananchi wote wa Tz.
 
alitoa ushauri kuwa watu wafanye mazoezi, wale matunda na kujifukiza. Kama vile haitoshi, akajipiga blanket na mumewe mbele ya kamera za waandishi wa habari ili dunia yote ione. In short huyu mama amepwaya kwenye hiyo wizara kupita maelezo.
Yani kila alichokikosa kwenye utendaji alikifidia na maneno ya shombo na kutaka kumfurahisha aliyemteua, kusahau ya kwamba ana wajibu kwa wananchi wote wa Tz.
... huyu alitakiwa afukuzwe muda uleule akiwa ndani ya blanket na mumewe wakionesha dunia ujinga wao! That's not a professional way to combat COVID-19!
 
Arudishwe Ummy wizara ya afya alikuwa serious kukabiliana na corona mpaka ikapotea.
Ni kweli kabisa. Ummy hakuwahi kuwa na mhemko alipokuwa akitoa report, akitembelea sehemu. Lakini huyu mama kila sehemu anayokwenda nusu saa nzima hutumika katika kutishia watu kuwa yeye ana akili zaidi. Anauliza swali kabla hajajibiwa anajijibu mwenyewe. Ni swala la wakati tu, ipo siku ataruka sarakasi kama Bruce Lee ili tu ku prove point kuwa yeye ni Field Marshall.
 
Back
Top Bottom