Ushauri kwa Rais Dkt. Hussein Mwinyi

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,214
3,587
Rais, Kijiolojia na kama muungano utadumu, Zanzibar ina kila sababu ya kupewa ardhi bara ili isipotee na ikipotea basi hakuna muungano tena maana Zanzibar haitakuwepo kwenye atlas ya dunia, itabidi Tanganyika irejeshwe.

Rais, Wanajiolojia na wanameteorolojia wameridhika kwamba ifikapo mwaka 2100 visiwa vyote vya Zanzibar na Mafia vitazama (vitaliwa na maji na kwisha kabisa), bado miaka 77 tu ambayo ni muda mfupi sana kuanzia hapa 2023.

Rais, Kujipanga na tukio hilo lililo karibu sana kutukia na kukata mzizi wa mgogoro kuhusu ardhi kati ya Zanzibar na bara (Makurunge RAZABA) napendekeza serikali ya SMZ izindue mpango mkakati maalum wa land fill au ocean reclamation ambao umeokoa UAE iliyoelemewa na idadi kubwa ya watu.

Rais, SMZ itafute uwezo wa kutekeleza mradi huu wa land fill na ikibidi iombe UN iiongezee eneo la bahari ya kimataifa ili kutanua mpaka wake.

Rais, kwa njia hii, mgogoro unaodhaniwa kuwepo wa Zanzibar kuchukuwa ardhi ya bara utaisha asilani na hata Wabara wengi watahamia Zanzibar kununua hiyo ardhi ya land fill.

Nawasilisha kwa heshima, taadhima na adhama.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Muungano udumu tuwe na serikali Moja hii ya kuwa na serikali mbili lazima Tanganyika watadai serikali Yao na pia ardhi yao
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom