neha mimi
JF-Expert Member
- Aug 19, 2014
- 344
- 152
Habari zenu wapendwa, binafsi ni mzima kiasi coz kichwa kinaniuma.
Jana nilikuwa nastorisha na rafiki yangu fulani hivi akawa ananielezea baadhi ya matatizo yake na mpenzi wake ni hivi; huyo mpenzi wa rafiki yangu anamlazimisha abebe mimba yani wazae mtoto lakini rafiki akakataa kwa madai kwamba hana kazi kwahiyo hawezi kubeba mimba kabla hajaolewa au kupata kazi lakini mwanaume amekuwa mkali na kununa ,kutokana na hali hiyo wamekuwa na migogoro ya hapa na pale na mawasiliano yamepungua sio kama mwanzo.
Wana uhusiano karibia mwaka sasa msichana anapajua kwa mpenzi wake na huwa anaenda mara nyingi anawafahamu baadhi ya ndugu zake na marafiki pia lakini huyo mwanaume hajui mpenzi wake anaishi wapi zaidi ya kufahamu tu jina la hiyo sehemu hamfahamu hata rafiki yake mmoja.
Rafiki yupo njia panda mpenzi anampenda ila kubeba mimba hayupo tayari ila anatami abebe ili alinde penzi,waungwana ushauri kwa rafiki yupo njia panda.
Pole kwa uandishi wangu mbaya.