Ushauri kwa mheshimiwa mwenyekiti wa CCM taifa

Ngamanya Kitangalala

JF-Expert Member
Sep 24, 2012
501
1,214
Napenda kuchukua fursa hii kumpongeza kwa dhati ndugu Dr Bashiru Ally Kakurwa kwa kuteuliwa na kuwa katibu mkuu wa chama cha mapinduzi taifa

Kwa uteuzi huu ni dhahiri pasipo shaka mh mwenyekiti taifa, amedhamiria kwa dhati kukifanya chama cha mapinduzi kiweze kujiendesha chenyewe kiuchumi, pasipo kutegemea ruzuku ama michango kutoka kwa wafanyabiashara kama ilivyokuwa siku za nyuma

Binafsi naamini jina la Dr Bashiru Ally kuwa katibu mkuu,lilikuwepo kwenye mawazo ya mwenyekiti taifa kwa muda kidogo, kwani lilikuwa likitajwa mara nyingi kama mrithi sahihi wa Comrade Kinana, hata kuteuliwa kwake kuwa mwenyekiti wa kamati ya kuhakiki mali za CCM ulifanywa kwa makusudi kabisa, ili aweze kupata fursa ya kufahamu ni kwa namna gani mali za chama zimekuwa zikitumika isivyo na kuwanufahisha baadhi ya watu wachache na si chama kama yalivyo makusudi yake

Hivyo basi kwa kuteuliwa kwake kuwa katibu mkuu CCM, itampa fursa nzuri zaidi ya kuhakikisha mali hizo zinarudi mikononi mwa chama na kukinufaisha chama, ni hatua nzuri sana ya kizalendo na ya kupongezwa iliyochukuliwa na mwenyekiti CCM taifa

Lakini binafsi kama ningekuwa kwenye nafasi ya kumshauri mh mwenyekiti au katibu mkuu mpya, ningewashauri hatua hii ya kurudisha mali za CCM, tuanzie hapa tulipo sasa, kwa maana ya kuwaomba wale wote waliojitwalia mali za chama kuzirudisha pasipo kwenda hatua zaidi za kuwataja hadharani ama kuwachukulia hatua za kisheria

Kwa nini nasema hivyo, lazima tukumbuke wale wote wanaodaiwa kuchukua mali za chama wengi ni wale wanaojiona ni CCM asilia( CCM maslahi), kundi hili ni kundi kubwa na lenye watu wengi wenye uzoefu katika siasa za nchi hii, wenye kujua fitna za siasa,

Kundi hili kama litapelekwa kwenye mikono ya sheria, litazidi kujenga chuki kubwa dhidi ya CCM mpya, kwani wengi wao katika kundi hili wanajiona wametengwa na CCM mpya

Kundi hili la CCM maslahi( CCM asilia) si la kupuuza hata kidogo, kwani ni dhahiri kwa kutumia izoefu wao katika siasa za nchi hii, wanaweza kuleta shida sana katika uchaguzi wa ndani wa CCM 2022, kwa vyevyote vile watakuwa wanajipanga kuandaa mgombea wao 2025 kama ilivyo kawaiida yao, pia ni lazima tukumbuke baada ya uchaguzi 2020, kundi hili hawatakuwa na nidhamu ya uoga tena kwa mwenyekiti kama waliyonayo sasa

Kundi hili linahitaji uangalifu wa hali ya juu katika kuwashughulikia
 
Nadhani sasa hii ni CCM ya wote, siyo tena ya wenyewe! Juhudi za kuiboresha CCM ziungwe mkono! Hongereni viongozi na wanachama wote wa CCM kwa ushirikiano wa kuimarisha Chama hasa hili la kukidhi takwa muhimu la uwepo wa chama hiki.
 
Nichukue fursa hii kumpongeza Katibu Mkuu mpya wa CCM.
Hata hivyo, Mwenyekiti amerahisha kazi na malengo yake. Aliyeandaa ripoti na mapendekezo ataifanyia kazi mwenyewe. Hiki kitakuwa kipimo kizuri cha ufanisi kwa Katibu Mkuu huyo.
.
 
wa
Napenda kuchukua fursa hii kumpongeza kwa dhati ndugu Dr Bashiru Ally Kakurwa kwa kuteuliwa na kuwa katibu mkuu wa chama cha mapinduzi taifa

Kwa uteuzi huu ni dhahiri pasipo shaka mh mwenyekiti taifa, amedhamiria kwa dhati kukifanya chama cha mapinduzi kiweze kujiendesha chenyewe kiuchumi, pasipo kutegemea ruzuku ama michango kutoka kwa wafanyabiashara kama ilivyokuwa siku za nyuma

Binafsi naamini jina la Dr Bashiru Ally kuwa katibu mkuu,lilikuwepo kwenye mawazo ya mwenyekiti taifa kwa muda kidogo, kwani lilikuwa likitajwa mara nyingi kama mrithi sahihi wa Comrade Kinana, hata kuteuliwa kwake kuwa mwenyekiti wa kamati ya kuhakiki mali za CCM ulifanywa kwa makusudi kabisa, ili aweze kupata fursa ya kufahamu ni kwa namna gani mali za chama zimekuwa zikitumika isivyo na kuwanufahisha baadhi ya watu wachache na si chama kama yalivyo makusudi yake

Hivyo basi kwa kuteuliwa kwake kuwa katibu mkuu COM, itampa fursa nzuri zaidi ya kuhakikisha mali hizo zinarudi mikononi mwa chama na kukinufaisha chama, ni hatua nzuri sana ya kizalendo na ya kupongezwa iliyochukuliwa na mwenyekiti CCM taifa

Lakini binafsi kama ningekuwa kwenye nafasi ya kumshauri mh mwenyekiti au katibu mkuu mpya, ningewashauri hatua hii ya kurudisha mali za CCM, tuanzie hapa tulipo sasa, kwa maana ya kuwaomba wale wote waliojitwalia mali za chama kuzirudisha pasipo kwenda hatua zaidi za kuwataja hadharani ama kuwachukulia hatua za kisheria

Kwa nini nasema hivyo, lazima tukumbuke wale wote wanaodaiwa kuchukua mali za chama wengi ni wale wanaojiona ni CCM asilia( CCM maslahi), kundi hili ni kundi kubwa na lenye watu wengi wenye uzoefu katika siasa za nchi hii, wenye kujua fitna za siasa,

Kundi hili kama litapelekwa kwenye mikono ya sheria, litazidi kujenga chuki kubwa dhidi ya CCM mpya, kwani wengi wao katika kundi hili wanajiona wametengwa na CCM mpya

Kundi hili la CCM maslahi( CCM asilia) si la kupuuza hata kidogo, kwani ni dhahiri kwa kutumia izoefu wao katika siasa za nchi hii, wanaweza kuleta shida sana katika uchaguzi wa ndani wa CCM 2022, kwa vyevyote vile watakuwa wanajipanga kuandaa mgombea wao 2025 kama ilivyo kawaiida yao, pia ni lazima tukumbuke baada ya uchaguzi 2020, kundi hili hawatakuwa na nidhamu ya uoga tena kwa mwenyekiti kama waliyonayo sasa

Kundi hili linahitaji uangalifu wa hali ya juu katika kuwashughulikia
Wasalaam , natumai sitakua nimekosea japo leo nami kuchangia kidogo. Nimerudia mara tatu kuusoma ushauri wako kiasi flani nimekuelewa nadhani umesahau kidogo tu kwamba CCM sio mtu au kikundi cha watu flan, CCM ni taasisi hakuna mtu au watu kikundi wenye uwezo wa kuwa juu au maarufu zaidi ya taasisi. na vile vile mwizi au fisadi ni mwizi tu au fisadi tu, hakuna mwizi maarufu kiasi kwamba aonewe aibu kuwajibishwa inapodhibitika ametenda kweli, binafsi nilisubiri sana kipindi kama hiki kifike , natamani sana kuona na wao wakionja uchungu wa jasho la watanzania na wana CCM walilofaidi kwa miaka mingi, NASEMA TENA MWENYEKITI BADO NI MPOLE SANA LAITI ....... wangekiona cha mtema kuni. Niishie tu hapa nisije andika mengne yasiyofaa

Ushauri tu kwa ndugu zetu wale wengine nadhani watatfute tu shughuli nyingine za kujiingizia kipato maana ule muda wa kujipatia kipato kupitia siasa za vyama vingi unakaribia kufikia ukingoni. niwakumbushe tu hiki ni CHAMA CHA MAPINDUZI kama wanaelewa maana ya neno MAPINDUZI basi wafanyie kazi neno hilo.

WASAAALAAM
 
Haya mambo yakuoneana huruma ndio yataturudisha nyuma.

Kwani hamna adhabu za ndani ya chama?
 
Back
Top Bottom