Kwa mara ya kwanza wana JF wamenena kiustaarabu na kiutanzania zaidi. Nadhani ni vyema hili likaendelea.Napenda kumshauri ndugu yangu SLAVE kuwa wauza ubuyu ndiyo wenye nchi hivyo alivyowataja ni kama amewadharau kama si binadamu wa kawaida au hawafikirii!!!!
Naamini Kamanda Lema akijitathmini vyema atakugundua wapi alikojikwaa maana Bosi wake Mh. Mbowe, pia kadinali Pengo na Shhe Mkuu wa Dar es Salaam wamenena kinyume nae kabisa tena Pengo ameenda mbali kusema haoni udini mahali ambapo hata waliokamatwa wengi ni wakristo, hivyo ni vyema uchunguzi wa kina ukafanyika.
Nikumbushe kuwa haya mambo yanafanywa au watu hutimiza azma yao pale penye mwanya; kwa mfano, kama kuna mwanya wa udini watu wanafanya mambo yao ili tu Arusha ishuke kiutalii utalii uhamie Kenya nani anajua???? Au mtu mwenye uchu wa kuona nchi haitawaliki ili tu Tanzania ionekane si sehemu salama ya watalii au mashirika ya kimataifa kuwepo, au siasa uchwara za hapa nchini au kama za obote za fanya lolote ili ikiwezekana wananchi waichukie serikali uchaguzi uitishwe upya au tufanye mapinduzi.
Mwisho, nashauri tuache kuzungumzia mambo yetu ya usalama hasa ya siri bila kujali mipaka. Hii ni hatari kubwa sana. Na huo ni ushauri wangu kwa Lema maana CHADEMA ikichukua nchi kwa kadiri ya mazungumzo ya Kiwia na wenje pale Mwanza ndiye atakua waziri wa Mambo ya ndani.