Ushauri kwa Makamanda: Kuhusu kususia chaguzi

Ushauri kwa Makamanda: Kuhusu kususia chaguzi

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
97,155
Reaction score
137,166
People’s.....

Ama baada ya salaam, ngoja tu niwape ushauri ingawa huwa hampendi kushauriwa wala kukosolewa.

Ni mara kadhaa sasa humu nimekuwa nikiwaasa kususia chaguzi na mmekuwa mkinibeza.

Baada ya kisago cha jana ndo mmeanza kuzinduka na kuona umuhimu wa huo ushauri wangu.

Sasa basi, kwanza poleni sana maana mmeshindwa vibaya mno. Pili, muwe mnakubali kukosolewa hususan ukosoo unaolenga katika kuwajenga.

Siyo kila anayewakosoa ni CCM au sijui kanunuliwa na CCM.

Hamjachelewa sana...mnaweza kabisa kubadilika. Kwa hiyo badilikeni kabla hamjachelewa.
 
Ujumbe huu kwa hisani ya Lumumba
 
Acha hizo wewe, hakuna anasiyekubali kukosolewa ila ukikosoa kinafiki lazima upewe ukweli wako. Wewe sema ukipewa ukweli wako unakwazika. Tuje kwenye ushauri wako, hiyo mbinu ya kususia uchaguzi ni sawa, je baada ya kususia ni hatima yake? Tuliona uchaguzi wa ZnZ Cuf walisusia, ni kipi walifanikiwa? Mkuu ukija na wazo tupe na mafanikio ya wazo lako na ukiwa na mifano itapendeza.
 
ushauri wangu kwa makamanda,cha muhimu sana kabla ya uchaguzi wa 2020 ni kupigania katiba mpya ya wananchi,bila yakatiba mpya nchi hii ipo chini ya himaya ya ufalme na sio democrasy,tuache siasa za kitoto za kushindana na wenye nguvu bila ya katiba mpya mwenye nguvu ndio atakuwa mshindi katika kila kitu,na mwishoe ikiwa hakuna tamaa ya kupata katiba watu dhaifu wote watampigia magoti mwenye nguvu, kama hao waliohama chama hivi karibuni,wote wamesalim amri
 
Nasisisitiza mafunzo ya kujilinda kwa makamanda..... hasa against haya ya kupigwa mapanga kipuuzi....
 
Ili watume ujumbe kwa matendo kuwa hawana imani na chombo kinachoendesha chaguzi nchini.
Kisha huo ujumbe itasaidia kitu gani chini ya serikali hii? Kususia siyo solution hata kidogo. Halafu ujuwe wanapewa pesa za kugombea kutoka kwenye vyama kwa ajili ya kampeni kiasi flani. Kwahiyo wanakuwa wameshajiandaa kabla hata sababu za kususia hazijaibuka
 
Kilichotokea Zanzibar na recently Kenya ni fundisho tosha kuhusiana na 'siasa za kususia chaguzi'

Kuna tofauti kati kususia na kujitoa kwenye uchaguzi. Dawa ni kutoshiriki kabisa tokea mwanzo kwa masharti mpaka kuwe na Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi
 
People’s.....

Ama baada ya salaam, ngoja tu niwape ushauri ingawa huwa hampendi kushauriwa wala kukosolewa.

Ni mara kadhaa sasa humu nimekuwa nikiwaasa kususia chaguzi na mmekuwa mkinibeza.

Baada ya kisago cha jana ndo mmeanza kuzinduka na kuona umuhimu wa huo ushauri wangu.

Sasa basi, kwanza poleni sana maana mmeshindwa vibaya mno. Pili, muwe mnakubali kukosolewa hususan ukosoo unaolenga katika kuwajenga.

Siyo kila anayewakosoa ni CCM au sijui kanunuliwa na CCM.

Hamjachelewa sana...mnaweza kabisa kubadilika. Kwa hiyo badilikeni kabla hamjachelewa.

mijitu mikubwa na akili zao eti inaenda kwenye uchaguzi huku ikijua kabisa Tume ya uchaguzi ni ya CCM

ukiwashauri wanatukana, beza, matusi bila hata kuangalia mantiki ya mtoa ushauri

cha kufanya

1. waache kila kitu wapiganie tume huru na taratibu za uchaguzi

2. waache chuki, zinawapofua! upuuzi wa kumpenda uhuru kisa raila ni rafiki wa magufuli that was stupidity of the highest order! leo wana nguvu gani ya kulaumu maana haya ndio yale ya uhuru kenya

3. viongozi wao sio miungu, ni watu wanaopaswa kukosoreka, kushauriwa na ukiona hawaeleweki tambaa

4. waache kujipa matumaini yasiyokuwepo KUONGEA KWA MSISITIZO KWA VITISHO AU SAUTI kubwa havikufanyi kukubalika kwa watu, sana sana wanakuogopa na kuwa wanafiki..kumbuka KURA INATOKA MOYONI! unatakiwa kuingia kwenye mioyo ya watu na sio kwenye vichwa vya watu, moyoni hauingiia kwa violance you shuld be trusted first

5. sio kila kitu kupinga, issue za madini, maknikia na tumbua tumbua chadema walipaswa kuvikubali vyote , hata kwa kwa kinafiki ili kupata MASS support ambayo ina msupport magufuli na kisha KUONGEA POLITELY how they will it better than magufuli kwa kuleta utofauti wenye lengo lile lile!! upuuzi aliokuwa anauongea Lissu bila heshima na kujali hisia za wengine na hasa za kiongozi wa taifa hazikupaswa kuwepo, unapomdhalilisha kiongozi wa kitaia haumii yeye tu, wanaumie wengi pia! hili ni somo pana sana, mniite kwa two days seminar how innocent souls that they love president zinaumia wanapoona rais anaumia, na hawa innocent soul ndo wapiga kura!......mtatukana tena

6. Toeni ushauri mbadala kwa kila tatizo! kuwe na writeups kuwa chadema walisema watafanya haya, KUKOSOA RUKSA, tumia lugha nzuri na kisha ELEZEA MBADALA wake, ambao unajua utaingia kwa wananchi over time, days, years even decades!

mwaka wa 20 sasa tunabaki tunatukanana watu wenye lengo moja kutaka mabadiliko ila njia na mawazo tofauti! personally nataka CCM waondoke hata leo hii, ila sio kwa upinzani huu, sio kwa wahuni kama Mbowe, Mbowe huwa najua kabisa hata ukimpa urais hatautaka, atakachotaka ni pesa tu, ni mafia tapeli na anayetoa false hopes....kuna wakati unawaza ni sehemu ya ccm ya kuwadanganya wanachadema na mabadiliko feki ambayo yeye hana mpango nayo

Hivi kwa akili za kawaida kabisa kabisa mkiwa na makende yenu, tume ya uchaguzi kweli iko huru mpaka mpeleke suruali zenu kupiga kura???, halafu mkishindwa mnalalamika, mna tofauti gani na mbwa ambaye analalwa na madume kumi kila mwaka na anazaa tu! akimaliza tena analalwa kwa uchungu, kisha mwakani anarudia, hata baba wa watoto hajui! sasa mpe ushauri mbowe na chadema uone!! watakomaa hivyo hivyo kana kwamba wanaotea vile

ebu amkeni bana, priority ni Tume huru ya uchaguzi kelele zingine mnajipotezea muda

sio mara ya kwanza

Mwongozo wa JF: What should start Tume Huru ya Uchaguzi au Katiba?
 
Kuna tofauti kati kususia na kujitoa kwenye uchaguzi. Dawa ni kutoshiriki kabisa tokea mwanzo kwa masharti mpaka kuwe na Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi
Kenya walikuwa na katiba mpya na tume huru pia...imesaidia nini? Mbona bado Uhuru alichakachua? Kwanini hatujifunzi jamani?
 
Back
Top Bottom