Ushauri kwa KIKWETE na NEC/ Makame | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri kwa KIKWETE na NEC/ Makame

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MkamaP, Nov 2, 2010.

 1. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #1
  Nov 2, 2010
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Natumai nyote mko salama.

  Ushauri wangu kama raia mwema kwenda kwako Rais Kikwete, Nakushauri kwa nia njema kabisa , tafadhali jaribu kuangalia mbali kidogo kutoka ktk pua.

  Ushauri wenyewe
  Tangazeni matokeo kama yalivyo hakuna haja kuyabana bana. Hata kama umeshindwa jaribu kumkabidhi ofsi aliyeshinda kwa amani na tabasamu.Hakika ukifanya hivyo utaishi kwa amani.

  Angalizo
  Ukichakachua matokeo, naamini watanzania watamezea na utaendelea kuwa rais kwa miaka mingine mitano. Lakini kama ukiangalia mbali ya pua , utaona bayana kabisa 2015 hutakuweza kuchakachua matokeo maana kura kwenda kwa upinzani zitakuwa nyingi ambazo hazichakachuliki. Hapo hapo Rais atayeingia atakuwa na MACHUNGU nawe na atakutia ndani na wenda na hiyo pesheni ya URAIS hadi kifo hutopewa.

  ADVANTAGE
  Kama umeshindwa na ukikubali kuachia kiungwana, UTAHESHIMIKA, kimataifa utakua mfano wa kuingwa na TANZANIA utaipeleka juu ktk uso wa dunia.

  Kama umeshindwa na hutaki maono rahisi kama haya ENDELEA KUCHAKACHUA.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Nov 2, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,711
  Trophy Points: 280
  Hapo ndipo ulipofunga mjadala lakini JK anaamini kuwa NEC itaendelea na mfumo uliopo hadi hapo watanzania watakapoleta machafuko kama yale ya Kenya na hapo ndipo NEC itaundwa upya na kuwa huru na haki..............................hii ndiyo akili finyu ya viongozi uchwara tulionao hapa nchini na ndiyo maana kamwe nchi hii haiwezi kuendelea.tutabaki na umasikini wetu milele............hadi hapo tutakapoanza kuheshimu haki ya wapigakura kujichagulia viongozi wao wenyewe..................................................
   
 3. N

  Njimba Nsalilwe JF-Expert Member

  #3
  Nov 2, 2010
  Joined: Mar 23, 2008
  Messages: 251
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Heshima kwako MkamaP!

  Tatizo watu kama akina Kikwete hawana uwezo wa kuona mbali vile vile hajijui. Kama angekuwa anajijua vizuri nina imani hata urais asinge gombea kwa mara ya kwanza. Wanafikiri leo tu, aliingia madarakani hata hajui matatizo ya watanzania hivyo hakuwa na lengo lolote lile alichotaka kuwa rais wa nchi. Sio ajabu alipoulizwa kwa nini Tanzania bado masikini mpaka leo alisema hajui.

  Nina imani kwa sasa anajua moyoni mwake kuwa nchi imemshinda na hana jipya lakini yupo kwa sababu anataka aitwe rais wa Tanzania, kwa hiyo sio rahis kwake kukubali matokeo kwa sababu hana uwezo wa kuchanganua mambo. Anaelewa kuwa kuna mikoa akienda watu hawamtaki kabisa lakini anjifanya halioni hilo.

  Mungu ibariki Tanzania;

  Njimba
   
 4. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #4
  Nov 2, 2010
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Mkamap:

  Kwa uchaguzi wa rais CCM wameshinda. Tena wameshinda kihalali. Matatizo yanayokuja je walioshindwa watakubali matokeo?
   
 5. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #5
  Nov 2, 2010
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Sasa kama wameshinda kwa mbali kwanini wanajiumauma kuweka mambo hadharani?
   
 6. C

  Chesty JF-Expert Member

  #6
  Nov 2, 2010
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 2,350
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  Wewe ndio unaesema hivyo, na kama anashinda kihalali ni vema tu ila kama anachakachua ili ashinde kwa kishindo ajue kuwa baadae yatajulikana tu na ikitokea kaingia presidaa say wa upinzani mambo yanaweza kumuwia magumu sana hata akajuka kwa nini aliwahi kuwa presidaa

  Hii dunia haiko static hata siku moja. Ni bora utende haki kuliko ukajutia maisha yako yote ya uzeeni.
   
 7. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #7
  Nov 2, 2010
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Je upo tayari kukubali matokeo?
   
 8. Avanti

  Avanti JF-Expert Member

  #8
  Nov 2, 2010
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 1,209
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135

  Kama kawaida yako!
   
 9. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #9
  Nov 2, 2010
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Chesty:

  Numbers don't lie. Sehemu ambazo CCM wameshinda ubunge, wameshinda pia kiti cha urais.. So why don't you use your own brain.
   
 10. Avanti

  Avanti JF-Expert Member

  #10
  Nov 2, 2010
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 1,209
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Kuweka hadharani kama?
   
 11. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #11
  Nov 2, 2010
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Mkuu,
  Wayatangaze hayo matokeo, maana hata kama ccm imeshinda na kuendelea kuyakalia kunaleta taswira ya ndiyo sivyo. Mbona seif kakubali kiungwana, naamini haki ikitendeka kwa mda muafaka hakuna atakayebisha, lakini, haki ikitendeka kwa mda usio mwafaka watu watabisha.

  Namuomba tena Raisa KIKWETE atangaze matokeo ni maombi tu.
   
 12. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #12
  Nov 2, 2010
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Uungawana upo pande zote mbili. Hivi kwa kuangalia trend ya matokeo kuna ubaya gani kiongozi wa upinzani concede defeat. Kwani CHADEMA hawaoni matokeo yanavyokuja?
   
 13. C

  Chesty JF-Expert Member

  #13
  Nov 2, 2010
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 2,350
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  Wala sipo hapa kubishana na wewe ila natoa angalizo, matokeo yatoke kama yalivyo na in fact hayakutakiwa kuchelewa cos ni kujumlisha tu. My point ni kuwa iwapo Kikwete atashinda wote tutampongeza ila kama kuna kura hata moja imeibiwa itajulikana tu iwe ni kesho au anytime in future.

  Na if that is the case future ya mchakachuaji ipo at stake. Hii dunia ya leo si ya lele mama, akina Chiluba wanaelewa zaidi.
   
 14. C

  Chesty JF-Expert Member

  #14
  Nov 2, 2010
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 2,350
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  Matokeo yanakuja mshindi hajatangazwa na referee halafu unakubali kushindwa, are you serious? O yeah you must be very serious. Kumbe tactic ilikuwa tuanze sehemu tulizoshinda ili wakiona waconcede defeat! Hapana kuna majimbo yenye wapiga kura wengi watu wanayasubiria na sio ya Zenji ya watu laki 3.
   
 15. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #15
  Nov 2, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Hii ni kweli kabisa, ila Kikwete ana upeo huo wa kutafakari unachosema? Yeye anaona raha anapopita anapigiwa ving'ora na saluti basi roho yake kwatu!
   
 16. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #16
  Nov 3, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Watu wengine wanamtindio wa ubongo. Sitayari mna matokeo mikononi mwenu yaliyosainiwa na mawakala wenu, kwani suala nikujumlisha tu, kwanini msijumulishe halafu mseme kuwa nyinyi mnaongoza, nijuavyo mimi, hata kama mngepata robo tu ya kura alizopata jk pangekuwa hapatoshi, kwani jinsi mlivyo watu wa shari hata askari wetu wangetumia nguvu. Bora mungu amewaepushia mbali. Sasa mmebaki kutapata tu wakati matokeo yote mnayo mikononi mweni. Poleni sana. See you again 2015, lakini muache ukabila na udini. Pia msiwatumie watu wengine kama ngazi ili kutimiza malengo yenu binafsi. I trust slaa, lakini wengi wa watu waliopo nyuma yake, no please.
   
 17. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #17
  Nov 3, 2010
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  I am very serious. MaCain conceded kabla kura hawajamaliza kuzihesabu. Na kuhusu majimbo yenye wapiga kura wengi naona unaendeleza ushabiki usio na mpango. Majimbo ya uchaguzi yanapangwa kutokana na idadi ya watu. Hivyo karibu majimbo yote yana idadi ya watu sawa. Kwa mtaji huo ukiangalia trend tu, utajua nani kashinda.
   
 18. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #18
  Nov 3, 2010
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,596
  Likes Received: 6,757
  Trophy Points: 280
  Wewe Zakumi, unasema CCM wameshinda uraisi, nani kakwambia. hata 20 percent ya matokeo hayajatoka wewe unadai wameshinda, wapi vidhibitisho?
   
 19. M

  MJM JF-Expert Member

  #19
  Nov 3, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 461
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Kama haujui kitu kaa kimya utaonekana una busara sana kuliko kuropoka. No research no right to speek hapa simaanishi ile research ya kitaalamu zaidi ila naomba usikilize matokeo yakitangazwa leo au usome sehemu yoyote utapata majibu ya hiyo nyekundu
   
 20. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #20
  Nov 3, 2010
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Wameshinda kabla ya matokeo? unafanya propaganda au unazungumzia uhalisia?
   
Loading...