Uchaguzi 2020 Ushauri kwa kampeni ya Urais ya CHADEMA

mwimbule

JF-Expert Member
Feb 25, 2009
585
288
USHAURI KWA KAMPENI YA URAISI YA CHADEMA

NDUGU
wanachadema wenzangu, Ni siku sita sasa zimeisha tangu kampeni ya uraisi ianze, Na kwa kweli niseme wazi kabisa CDM tumeanza vizuri sana katika kampeni hii, na tumepiga hatua kubwa sana, katika harakati hizi za kampeni,

Pamoja na yyote naomba kutoa ushauri kwa Uongozi wa Kampeni ya Urais ya Tundu Lissu, naomba mambo kadhaa yaboreshwe

Naomba kuwe na Mzungamzaji mmoja anaweza kuwa kiongozi wa Chama kwa maana ya Mwenyekiti Au Katibu Mkuu wa Chama,,

Mzungumzaji huyu ajikite katika mambo manne,, Awe anawaomba msaada Watanzania kujitolea ili kupambana na CCM,,,Na kujitolea kwenyewe kuwe katika maeneo yasipungua manne

La Kwanza ni kuomba RASILIMALI FEDHA ili kupambana na CCM,, Na kwa hili nimeona uongozi umeliona na umekuwa ukilitekeleza kwa uzito mkubwa,, kwa hili napongeza sana. Kwa sababu rasilimali fedha ndizo zitaweza kutufikisha katika kila kona ya nchi hii. Kwa hili heko na hongera kwa kulitambua na kulitekeleza. Na hili liwe kwa wote wenye muda na wasio na muda,,. Lakini kama huna muda kabisa basi jitahidi kutoa rasilimali pesa kuwezesha mchakato.

La pili, kuomba wananchi wajitoe VOLUNTEER, pia wananchi waombwe kujitolea, ku volunteer angalau kila mmoja aweze kushawishi watu kumi kwa kuomba kura zao,, na hii inaweza kuwa kwa majirani zake, inaweza kuwa ni majirani wake, marafiki zake, kwa ndugu zake, kwa waumini wenzake.Na pia wajihusishe sana na kampeni,,,,,watumie muda wao kushiriki huu mchakato wa kuiondoa CCM madarakani. Ikichukuliwa kwamba kwa miaka mitano CCM wamekuwa wakifanya siasa peke yao. Na hii itakuwa kwa wale wenye muda wa kutosha au wanoweza kutenga muda wao ili kutekeleza haya.

La tatu, naomba pia mzungumzaji aweze kuomba MSAADA WA MAWAZO (IDEAS) wale wote wenye mawazo ya kuboresha au kuonyesha nini kifanyike ili mkakati wa kuiondoa CCM ufanyike,,, Kuwe na namba maalumu za WHATSUP, ambazo zitumike kupokea mawzo hayo ni pia kutuma hayo mawzo kwa viongozi. Tukumbuke watu wana mawazo very constructive ya kusaidia process nzima ya kampeni hadi matokea ya Uchaguzi. Kuwe na kitengo maalumu ndani ya chama kitakachochambua haya maoni na kuona namna gani yanafanyiwa kazi.

La nne naomba pia Viongozi au Kiongozi aombe Msaada wa WATAALAMU WA KUJITOLEA, Na hawa wataalum wanaweza kugawanywa kwenye kanda zote za chama, wafanye kazi ndani ya chama kwa kusaidia utaalamu wao, pili wataalamu hawa wanaweza kutumika kudesign mpango mkakati wa kupeleka taarifa zote .

Na mwisho naomba wale WALIOFANYIWA MADHILA NA SERIKALI, WAJITOKEZE KWENYE MIKUTANO,, au wapewe segment za kusema,, kwa mfano kuna watu waliobomolewa mmoja wapo aje azungumze kwenye mkutano,, kwa kupewa nini aseme,, au yule jamaa alifungwa na Lissu kujitolea anaweza kwenda kwenye mkutano na kusema namna gani alivyosaidiwa hadi akatoka jela,, au mtu alidhulimiwa korosho zake mtwara,, Naye anaweza kupewa script akasema,, au kwa wale wanaogopa, wanaweza kuwa recorded na kisha record zao ziwe prayed katika mikutano kabla ya mgombea Uraisi.

Ni Mimi Kamanda Mwimbule,
 
Ushauri mjarabu Sana tatizo Lissu ana mission yake special toka ughaibuni ,
 
Back
Top Bottom