Ushauri kwa huyu ex-wangu

BEST ONE BOY

JF-Expert Member
Mar 21, 2017
309
221
HABARI za mda huu usiku tulivu
Naomba niende direct kwenye mada
Mimi ni kijana mwanzoni kipindi nipo
O level niliwahi kuwa na uhusiano na msichana mmoja ila yeye alikua anasoma shule ya jirani lakini baada ya kumaliza masomo ya o level Mimi nilifanikiwa kwenda advanced yeye hakufanikiwa hivyoo alibaki mtaani na wazazi wake walimwambia ngoja wajipange ili waje wamsomeshe mwaka mmoja baadae kipindi nipo likizo baada ya muhula wa kwanza wa advance nilimwambia
Mpenzi wangu kuwa naomba MUNGU akijalia tuwe wanandoa mbeleni akakubali na alifurahi sana na hapo mahusiano yalikolea sana na hadi ikafikia hatua ya kunitambulisha
KWA wadogo zake kuwa huyu shemeji yenu
Nilipokuwa form six mwishoni nilipata taarifa kwa mmoja kwa marafiki zangu kuwa mpenzi wangu kuna jamaa mmoja dereva wa TRA anafukuzia mpenzi wako nilipopata taarifa hizo nilikua kimyaaa nafanya utafiti na kimya kimya bila ya kumuuliza mpenzi wangu mana
Nilitaka kuthibitisha jambo hiloo

Baada ya kumaliza paper ya form six narudi tuu home mpenzi wangu mapokezi yake hayakuwa na furaha sana alinipokea kawaidaaa tuu kama nimetoka sokoni ila nilipiga moyo konde kusema labda kwa kuwa tumezoeana

Si unajua siku hizi mifumo ya serikali lazima kupitia jkt kwa form six nami jina langu lilikuwepo basi nilimpa taarifa mpenzi wangu kuwa baada ya week moja na nusu ntaondoka
Kwenda jkt akasema sawa

Kumbe yeye wakati huo mapenzi yapo motomoto na dereva wake wa TRA na alimuahidi kuja kumtolea mahali mwezi wa saba wakati Mimi mwezi wa Sita ndio naenda jkt

Zimebakia siku tatu jioni napata sms kuwa" boyfriend wangu niilikupenda sana ila nimepata mwanaume natolewa mahali mwezi ujao ila mimi siwezi kukuacha mana nimekuozea ila kuvumilia mpaka uje kumaliza masomo ndio kumenishindaa"niliumia sana nikaja kujua ukweli juu ya taarifa ambayo rafiki yangu alinipa lakini nilipitia wakati mgumu sana ila kwa kuwa nilikua nipo depo hisia zilikata na nikawa nipo kimyaaa


Baadae nipo chuo sasa naendelea na masomo yangu siku nilipata sms habari yako

Wakati huo nilipata taarifa kuwa ex wako tayari mjamzito jamaa kaishamjaza na life Lao NI la kawaidaa na mwanaume kabadilishwa kituo cha kazi kutoa mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine
Basi nilienda kipindi cha DINI na nilitoka nikapiga namba Ile kumbe alikuwa ex wangu akapokea simu kwa kuanza kuomba misamaha mkubwa sana Mimi nilishakusamehe ila naomba utambue KUWA wewe ni mkewa mtu akanijibu kuwa ndio ila nimekwama sana hivyoo naomba unisaidie kama utaweza hela kama laki moja kwa kuwa nipo nasoma na Nina shughuli zangu zingine za kibiashara hapa mjini nikaona sio mbaya nilimpa akanishukuru sana

Kuanzia pale nilibadili line ila alinitafuta tena akiwa na mimba ya miezi saba kuwa anaomba hela ya mana ameambiwa aende hospital kubwa mana ndio mimba ya kwanza kwa check up zaidi mana anaumwa mara kwa mara nilimsaidia ila sikupendakuwasiliana naye mana mkewa mtu

Kuanzia mwezi uliopita kaachana na bean yake na karudi kwao sasa hapo simu kila siku kwangu na kaisha tuma watu wamsaidie kuomba msamaha kwangu anataka kurudiana na Mimi naomba ushauri wenu wadau wa jf kwa kijana mwenzenu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom