Matuja umeandika vzr, maoni mazuri sana..tuko na matatizo nchi yetu kwanza kama mmoja mmoja, lkn pia kama watanzania..la kwanza kama mmoja mmoja ni attitude, kwamba usomi wangu unanijengea tabia ya kujiona najua kila kitu, wivu, ubinafsi na wakati mwingine dharau pia, zaidi wengi walio ndani ya mfumo wa serikali wao kupata hizo nafasi ni kama wamefika anachojua kufanya ni kuwa KEEPER wa yale yaliyopo hana muda na hahitaji kuwa na jambo jipya, la nini kwake wakati mwisho wa mwezi mshahara wake uko pale pale??..kama watanzania au nchi, mfumo wa serikali ulivyo hauna mlango kuruhusu mambo mazuri nje ya mfumo wa serikali kuingia kwenye mfumo wa serikali, sijui pengine kwa kuamini kwamba wale waliomo ndani ya mfumo wa serikali ni bora sana kuliko wote walio nje ya mfumo wa serikali, which is wrong!!!
Mambo mawili yanaweza saidia kuwa na watu wenye maoni kama ya Matuja ndani ya serikali au hata wakiwa nje ya serikali maoni yao yatapata nafasi kutekelezwa na serikali..
1. Ajira za kada ya kufanya maamuzi ndani ya serikali, pamoja na mambo mengine zipime utendaji wa wahusika kwa kuangalia mambo mapya mangapi wameanzisha, wametoa majibu(solutions) ngapi kwa changamoto walizozikuta..haya yakikosekana, ajira inaishia hapo anatafutwa mtu mwingine.kwa maana hiyo kuwa na mfumo wa ajira za kudumu uondolewe.
2. Taratibu za uajiri na hasa kwenye usaili wahusika waulizwe philosophical questions, sio vyeti na grades, philosophical questions zinasaidia ku-reveal uwezon wa muhusika kutenda, brain energy kusolve matatizo, ubunifu nk itasaidia kupata right people na sio KEEPERS!
3. Tufikirie kuwa na kongamano la kitaifa linaloalika kila mwenye jambo zuri kusikilizwa na kuulizwa maswali ya hicho anachodhani ni kizuri kwa nchi yetu na akithibitisha na kukitetea kichukuliwe kifanyiwe kazi hasa kwenye sekta muhimu zinazoathiriwa na mabadiliko ya kidunia, Elimu, afya, uchumi, ulinzi na usalama, teknolojia, biashara na uwekezaji, kilimo,ufugaji na uvuvi pia.
Vinginevyo bado tutaendelea na udumavu huu kwa miongo kadhaa ijayo..!