Ushauri kwa chadema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri kwa chadema

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MWANA WA UFALME, Oct 20, 2010.

 1. MWANA WA UFALME

  MWANA WA UFALME JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2010
  Joined: Sep 10, 2010
  Messages: 578
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nasema ushauri kwa chadema maana ndicho chama hapa bara ambacho kinawatia wasiwasi cccm na kinawindwa kila kukicha,


  taarifa za tetesi nyingi zilizokwisha fikishwa hadi sasa juu ya hujuma za ccm wakishirikiana na vyombo vya dola si za kupuuza.

  nasema si za kupuuza maana tayari baadhi ya hizo tetesi tunaona zikitokea, mfano juu ya kuingizwa kwa kura feki toka south africa, na kwamba kura hazikutengenezewa uk bali south etc,

  tetesi nyingine zilizokwisha wasilishwa hapa ni juu ya uchakachuaji wa matokea kwa kutumia teknologia, wizi etc, kura feki kuwasili kwenye vituao kuanzia tarehe 25 mwezi huu, kufanyika kwa fujo kwenye vituo kwa lengo la kupitisha kura feki ndani ya vituo, huku polisi wakitumika kuwahoji mawakala pembeni kwa lengo kutoa mwanya wa shughuli hiyo. Tetesi za mwanzoni mwa kampeni zilikuwa kwamba ccm inapanga kutumia maisha binafsi ya silaha na kisingizio cha udini, hili tumeliona. Nyingine ilisema redet wanataka kutoa taarifa kuonesha kuwa ccm inakubalika kwa kiwango kikubwa, hili nalo tumeliona.

  hata hivyo hizi tetesi nyingi zinaharufu ya ukweli ndani yake baada ya kuona nec ikiwataarifu mawakala mapema kwamba hata wasipotia saini form haiwezi kubadili chochote, kutishia wanachi wasikae karibu na vituo vya uchaguzi kusubiria n.k.

  huku tukiwa tunasubiria kama kweli haya ndiyo yanayoendelea, nataka kushauri chadema wazichukulie kwa umakini tetesi kama hizi. Hatua ya kwanza ni kuwataarifu waangalizi wa kimataifa kuwa wanahisi haya yatatokea, na yatakapotokea ieleweka kwamba hawakuwachongea bali ndivyo yalivyokuwa yamepangwa.

  la pili ni kutumika kwa nguvu ya ziada ya kulinda kura toka kwenye vituo hadi kwenye majumuisho yake. Kuwe na independent committe pia ya chadema ya kujumlisha matokeo yatakayokuwa pia yakitumwa kwa njia ya simu na mawakala wao, na sio kusubiria ya nec ambayo yanaweza kuwa yamekwisha kuchakachuliwa na computer.


  mawakala hapa watatakiwa wale kiapo cha kutoasi, na waonyeshe ujasiri wa kuhakikisha kuwa kila kituo wanakagua hadi daarini kama lipo dari, maana wanaweza kuweka vitu huko kwenye madari pia.

  kuangusha utawala wa kimabavu, kunahitajika juhudi za ziada.
   
 2. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #2
  Oct 20, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,090
  Trophy Points: 280
  Nimepitia tovuti ya Chadema sasa hivi haraka haraka na kushindwa kupata idadi ya wanachama wao. Sasa nawaomba mfanye kama msemo huu unavyosema "mtoto wako mkabidhi kwa mchawi"/ "Zimwi likujuwalo halikuli likakumaliza". Vituo viko vya kupigia kura viko karibu 52,000. Hivyo mawakala 52,000 wawe wanachama wa Chadema. Pia kuwe na mawakala mbadala 52,000 standby nao vile vile wawe wanachama. Msijindanganye kuwa ambako hamjasimamisha mgombea ubunge kusiwe na mawakala wenu, kumbukeni kura za Urais, Dr. Slaa.

  Mawakala wawepo muda wote wakati wa kufungua kituo, kupiga kura, kuhesabu kura, kubandika matokeo na kupata nakala ya matokeo na kuiwasilisha kwenye chama; mawasiliano ya simu yawe muhimu sana hasa kwenye kujua matokeo ya kila kituo [wakala ampatie matokeo ya kituo kiongozi wa kata au jimbo wa chama kama yupo kama hayupo basi awekwe mtu wa kufanya kazi hiyo ambaye atajumlisha matokeo yote ya jimbo katika ngazi ya Urais, Ubunge na kata]; chakula kiwe cha safari na kitoke sehemu maalum yenye usalama; mawakala watakao choka au kupata dharura watoe taarifa mapema hili wale mbadala wachukue nafasi; wawe na maji ya kunywa ya kutosha; wasikubaliane na kutokuwepo kituoni au shughuli ya kura kusimama kwa kisingizio cha break ya kwenda kula (hasa baada ya kituo kufungwa yaani wapiga kura kumaliza kupiga kura).

  Kwa kweli nimeimba sana kuhusu ili, na nafikiri Chadema wameliona na kusoma na kuelewa.
   
 3. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #3
  Oct 20, 2010
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Nadhani wamekupata.. umewaandikia maoni haya maan a ktk website yao kuna sehemu ya maoni. Ikiwezekana wapigie simu si unajua wako ktk Kampeni?
   
 4. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #4
  Oct 20, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  muda wa kutoa ushari mtupu hapa kwenye jf umekwisha, sasa ni wakati wa kila mtu kujitoa kupiga na kusimamia kura katika vituo. Kama tutabaki kutoa ushauri tuu, ni wazi kuwa kura hizi zitakuwa hazina waangalizi. Na ccm watapita kwa kishindo. Kila mmoja wetu anafahamu kuwa kutokana na mazingira ya kifisadi yaliyojengeka hapa nchini kulinda kura ni moja ya tasks ngumu sana. Zinzhitaji watu wenye uelewa, elimu, upeo na kujitolea kwa kiwango mcha juu kabisa.

  Kama kweli tunataka ccm iondoke madarakani basi twende tukajiorodheshe kuwa mawakala wa chadema, kusaidia katika surveillance ya mtirirko mzima wa wizi wa kura n.k
   
 5. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #5
  Oct 20, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mapinduzi hayafanywi na mtu mmoja Dr Slaa pekee yake,hataweza haki ya mungu,
  Mapinduzi yanataka umoja na nguvu.Kuelewana na kuvumiliana.
  Nawaombeni watanzania wenzangu mlioko hapo karibu mjaribu kuweka maslahi ya walio wengi ili tuweze kurejesha hadhi ya Tanzania kama ilivyokuwa hapo awali.
  Kulinda Kura ni kazi ya kila mwanachama wa chama husika,kama ni CHADEMA mwanachama wake awe pale full time.Ukitoka tu umeliwa.
   
 6. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #6
  Oct 20, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  mm mmoja nataka uwakala wa chadema
   
 7. W

  WAMURUBHERE JF-Expert Member

  #7
  Oct 20, 2010
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  umesomeka mkuu ni utekelezaji umebaki!
   
 8. semango

  semango JF-Expert Member

  #8
  Oct 20, 2010
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 532
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  asante sana mkuu kwa umakini wako.keep up the good work
   
 9. PAS

  PAS JF-Expert Member

  #9
  Oct 20, 2010
  Joined: May 3, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  una uhakika unacho kinena????
   
Loading...