Ushauri kwa CHADEMA na UKAWA

Brigedia Chan-ocha

JF-Expert Member
Mar 7, 2014
1,353
2,842
Kwa kuwa Serikali ya awamu ya Tano imeonesha wazi wazi kutotaka mfumo wa vyama vingi kwa namna yoyote ile ile halali au haramu.

Na kwa kuwa mazingira yote yanaonesha kuwa huko mbeleni hasa uchaguzi wa mwakani na wa 2020 mauaji kwa raia yatakuwa mabaya sana.

Na kwa kuwa hakuna dalili yoyote ya serikali kujirekebisha kwa vitendo vyake vya kutotaka hata wabunge wachache wa upinzani waliopo bungeni waendelee kuwepo kwa gharama yoyote ile iwe halali au haramu.

Hivyo basi, napendekeza wabunge wote wa upinzani, madiwani wote na wenyeviti wote wa serikali za mitaa wajiuzulu nafasi zao ili wawaachie Bunge na halmashauri na mitaa hicho chama, maana naona ndicho wanachokitaka, wanataka wabaki peke yao watawale peke yao, hata kama mtaamua kubaki uchaguzi kama mazingira ndio haya na kama hayatabadilika hali itakuwa mbaya sana huko mbeleni.

Kumbukeni mlimpa tahadhari Rais juu ya kuteua wakurugenzi makada wa CCM lakini hakusikia, walichowafanyia mlikiona na mmekiona juzi Kinondoni na Siha, hivi mnadhani hata kama mngeshinda kweli mngetangazwa? RC, DC na Kamanda wa kanda maalumu ya Dar wamo ndani ya jengo la kujumlishia kura unadhani wangekubali mtangazwe?

Mmeona wenyewe jinsi Tume ya uchaguzi ilichowafanyia na majibu iliyowapa bado mna imani yoyote? Mbowe chukua hatua mapema, jiondoeni wote muachie Bunge lao, dunia itaona.
 
hivyo basi, napendekeza wabunge wote wa upinzani, madiwani wote na wenyeviti wote wa serikali za mitaa wajiuzulu nafasi zao ili wawaachie Bunge na halmashauri na mitaa hicho chama, maana naona ndicho wanachokitaka, wanataka wabaki peke yao watawale peke yao, hata kama mtaamua kubaki uchaguzi kama mazingira ndio haya na kama hayatabadilika hali itakuwa mbaya sana huko mbeleni.
Acha utani na ugali wa watu wewe unaweza kujiuzulu ubunge bila ya uhakika wa kupata kazi ingine?
 
Hakuna sababu ya kupotezeana muda wakati wa chaguzi zozote zile! Ikiwa hali inaendelea hivi, ni bora ubaki mfumo wa chama kimoja.
 
Kwa kuwa Serikali ya awamu ya Tano imeonesha wazi wazi kutotaka mfumo wa vyama vingi kwa namna yoyote ile ile halali au haramu.

Na kwa kuwa mazingira yote yanaonesha kuwa huko mbeleni hasa uchaguzi wa mwakani na wa 2020 mauaji kwa raia yatakuwa mabaya sana.

Na kwa kuwa hakuna dalili yoyote ya serikali kujirekebisha kwa vitendo vyake vya kutotaka hata wabunge wachache wa upinzani waliopo bungeni waendelee kuwepo kwa gharama yoyote ile iwe halali au haramu.

Hivyo basi, napendekeza wabunge wote wa upinzani, madiwani wote na wenyeviti wote wa serikali za mitaa wajiuzulu nafasi zao ili wawaachie Bunge na halmashauri na mitaa hicho chama, maana naona ndicho wanachokitaka, wanataka wabaki peke yao watawale peke yao, hata kama mtaamua kubaki uchaguzi kama mazingira ndio haya na kama hayatabadilika hali itakuwa mbaya sana huko mbeleni.

Kumbukeni mlimpa tahadhari Rais juu ya kuteua wakurugenzi makada wa CCM lakini hakusikia, walichowafanyia mlikiona na mmekiona juzi Kinondoni na Siha, hivi mnadhani hata kama mngeshinda kweli mngetangazwa? RC, DC na Kamanda wa kanda maalumu ya Dar wamo ndani ya jengo la kujumlishia kura unadhani wangekubali mtangazwe?

Mmeona wenyewe jinsi Tume ya uchaguzi ilichowafanyia na majibu iliyowapa bado mna imani yoyote? Mbowe chukua hatua mapema, jiondoeni wote muachie Bunge lao, dunia itaona.

Duh mkuu ni wewe?
 
Back
Top Bottom