Wanabodi,
Kama kawa, kila nipatapo fursa
Kufuatia tishio la matamshi yenye viashiria vya uhaini dhidi ya serikali ya JMT kwa baadhi ya watu, na watu hao kushikiliwa na vyombo vya dola, waneibuka watu, mashirika, wanaharakati kupigia kelele kuna kesi ya uhaini, na hadi baadhi ya taasisi za kimataifa kutaka kuingilia kati mambo yetu ya ndani!, hivyo kufuatia mwandishi wa makala hizi kuwa pia ni mwanasheria na wakili wa kujitegemea, naomba kuitumia makala ya leo, kuanza mfululizo wa makala elimishi kuelimisha umma kuhusu katiba, sheria, haki na wajibu kwa jicho la mtunga katiba.
Naomba nianze na elimu fupi kuhusu makosa mawili makubwa kuliko makosa yote kwenye katiba yetu. Makosa haya ni kosa la kuua, (murder), na kosa la uhaini, (treason), ambayo yote adhabu yake ni kifo, au "capital punishment", na kwa Tanzania adhabu hii inatekelezwa kwa kunyongwa hadi kufa, kwa nchi yetu tuna gereza moja tuu la kunyongea ni gereza la Isanga, liko Dodoma.
Uhaini ni nini? Uhaini umetajwa kwenye sura ya Saba kifungu cha 39 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, yaani penal code kinasema Kifungu cha 39 ( 1 ) cha kanuni za adhabu kinasema kuwa mtu yeyote ambaye yumo ndani ya Jamhuri ya Muungano au popote, kujaribu kumuua Rais, kuanzisha vita dhidi ya Jamhuri ya Muungano, kusababisha, kuwezesha, kuchochea, kushawishi, kushauri kuhusu kifo, kumlemaza, kumzuia, kufungwa kwa Rais.
Kwa mujibu wa sheria tuliofundishwa darasani, uhaini ni vitendo na sio kauli ni uchochezi!. Kwa vile mpaka sasa hakuna mashitaka yoyote ya uhaini yaliyofunguliwa katika Mahakama yoyote, nawaombeni Watanzania wenzangu tusishabikie uzushi wa uhaini, hili sio jambo la kheri hata kidogo.
Vivyo hivyo kwenye jinai ya uhaini, sio kila matamshi ya uhaini ni uhaini, ili kuwepo kwa jinai ya uhaini, lazima kuwepo kwa zile sifa kuu mbili, actus reus na mens rea ya kupanga kufanya uhaini. Kitendo cha mtu ameghafilika tuu na hoja za Club House, akaanza kuhororoja kutoa matamshi ya kupindua serikali, haimaanishi ni uhaini wa kupindua kweli serikali, lakini matamshi hayo yanaweza kuwa ni matamshi ya uchochezi hivyo kusababisha watu wapange kweli kupindua serikali, lakini matamshi tuu kama matamshi bila ya kuwepo means rea ya kupindua serikali, watu hao watakuwa wamefanya kosa la sedition na sio treason.
Wasalaam
Paskali