Ushauri kwa CDM MPs Bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri kwa CDM MPs Bungeni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Inkoskaz, Jun 9, 2011.

 1. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #1
  Jun 9, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Kikao hiki ni muhimu sana katika ratiba ya vikao vya bunge kila mwaka hivyo na kwa kuwa wawakilishi wetu japo sio wote lakini wengi ni wageni mjengoni sio vibaya tukishare mawazo mbalimbali humu mitandaoni kwa faida yenu nyinyi wenye mic huko bungeni
  1.Mjenge utaratibu wa kusoma kwa makini vijitabu vya bajeti,kutafakari na kuweza kuibua hoja pale panapohitajika marekebisho

  2.Muwe na vikao vyenu vya marejeo na majumuisho ya mliyojadili na mtakayojadili kila mwishoni mwa wiki japo na ninyi mnahitaji kupumzisha akili kule mnadani

  3.Kutofautiana hoja mbalimbali isiwe sababu ya kuwabomoa,wekeni namna ya kuzijadili hoja binafsi na kukubaliana kabla hazijawakilishwa na mhusika

  4.Wanachama,wapenzi na wafuasi wa CDM wapo wametapakaa kila kona na humu mitandaoni wapo,msisite kuwaomba ushauri na pia kusikiliza maoni yao kwa kila bajeti husika i.e Miundombinu-Engineers,Katiba na Sheria-Lawyers,Afya-Doctors,Elimu-Walimu,nishati na Madini-Consultants,Kilimo,ufugaji,uvuvui,watoto,kazi,mambo ya ndani kote kuna wataalam etc..etc..

  5.Pingeni kwa nguvu ule utaratibu wa kupiga kura kwa kujibu ndiyo au hapana,uwepo utaratibu wa siri(kumbuka hata wabunge CCM wanaweza kuwa na support kwenu lakini kwenye kura ya kusimama na kujibu akakionea chama chake aibu akajibu kinyume na nafsi yake) refer ule muswada wa sheria za mahakama kikao kilichopita.
  Technology imekuwa sana,unaweza hapo kwenye meza yako ukapress button ya yes or no na rekodi ya kura yako ikaingia na kujumlishwa bila kuchakachuliwa

  6.Maswali ya Nyongeza is a must yale ndio muhimu kwani majibu ya awali huwa ni uwongo uliokwishaandaliwa,sasa mkiwa na maswali mazuri ya nyongeza tuna hakika ya kujua waziri alichojibu anakielewa au alikesha 84

  7.Nidhamu ya kikao,Mahudhurio ya vikao vyote bila kukosa labda kwa udhuru maalumu na kujali muda wa kuanza vikao,waacheni hao wanaosema wana majukumu ya uwaziri nk,nyinyi pigeni mzigo matokeo mtayaona

  Najua wenzangu nao wana mengi waliyonayo watawaeleza hivyo mkipata wasaa japo chungulieni humu mtapata hazina ya mawazo yao
  Nawatakia kikao chema na motomoto
   
 2. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #2
  Jun 9, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,001
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  nafikiri hayo ndio wabunge wa CDM wanayoyafanya walau kwa 90%
   
 3. T

  Taifa_Kwanza JF-Expert Member

  #3
  Jun 9, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 443
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Good Mind
   
 4. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #4
  Jun 9, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Ushauri mzuri sana. Napenda kusisitiza la mahudhurio na kura. Hudhurieni vikao vyote bila kukosa. Acheni kuruka ruka hapa Dodma kama wehu, iweni na utaratibu si kuishi kama mbuzi walioachiwa shambani. Nidhamu ni muhimu sana, hasa nidhamu ya kuiheshimu miili yetu yaani kuipatia wakati wa kutosha wa mapumziko, kulala mapema.
  Pingeni kwa njia zozote utaratibu wa kupiga kura kwa kusema ndiyo na siyo, njia hii ni njia ya mbovu kabisa kwani wale wasio na kitu mara nyingi ndiyo huvuma zaidi. Hata waswahili wamesema, "Debe tupu haliachi kuvuma."
   
 5. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #5
  Jun 9, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Ni kweli mkuu....mapumziko ni muhimu sana..yatawafanya waamke fresh na nguvu za kupambana na wazee wa mipasho
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  Jun 9, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Wawe makini sana na watumie vyema ile quality yao ya information sharing 24/7..... kama wana swali au hoja warushe kwa timu zao za nje,

  ikiwezekana wapunguze vikao vya jioni ili kujiandaa na mtihani huu muhimu wa mwaka
   
 7. L

  Luiz JF-Expert Member

  #7
  Jun 9, 2011
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 342
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimependa ushauri wako wewe ndio mwanajf wa ukweli naomba ushauri uwe kwa wabunge wote wenye nia nzuri na nchi hii tusiwe kama wale wanaopiga makofi mda wote mradi siku iende "the time will come".
   
 8. S

  Smallnick Member

  #8
  Jun 9, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I like that. Wabunge wetu wa chadema kumbukeni kua taifa linawaangalia tena linategemea sana michango yenu ili kuweka taifa letu mahali tunapopataka. Japo mpo wachache ila watanzania tupo wengi muamin kua sauti zenu ndio sauti za watanzania.
   
 9. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #9
  Jun 9, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  True buddy
  watu wapo every corner of this universe na wana ideas nzuri
   
 10. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #10
  Jun 9, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Chief Whip tunakutegemea usiyumbishwe na yule mama mburuzaji wa kanuni
   
Loading...