Adharusi
JF-Expert Member
- Jan 22, 2012
- 14,497
- 7,426
Kwanza, nikipongeze Chama cha Mapinduzi kwa mchakato wa kura ya maoni kwa wagombea ubunge na madiwani wa majimbo (uteuzi kwenye vyombo vya dola).
Nakipongeza sana Chama cha Mapinduzi kwa kurudisha utaratibu huu wa kura ya maoni kupigwa kwenye kata kwa wajumbe wote wa matawi mpaka mabalozi. Kihalisia fulani umepunguza sana matumizi ya rushwa. Chama kifanye tafiti kitaona. Kwa sababu utaratibu wa mikutano mikuu ya wilaya na taifa una mpenyo mkubwa sana wa matumizi ya rushwa — rejea mikutano mikuu ya mikoa na taifa ya uchaguzi wa UWT, UVCCM, Jumuiya ya Wazazi — namna ilivyokuwa kama soko la ulanguzi. Wagombea wamezimwaga kweli kweli. Ukiongea na wajumbe watakuambia ukweli.
Ushauri wangu kwa CCM: kuanzia 2030, majina yasiyozidi matano ya wagombea urais kutoka kwenye Kamati Kuu yarudishwe katika kata kupigiwa kura za maoni Tanzania nzima ndani ya chama, kama wanavyopigiwa kura wabunge wa majimbo.
Vilevile, wagombea viti maalum — baada ya uteuzi wa Kamati Kuu — majina yaliyoteuliwa yapigiwe kura ya maoni na matawi ya mkoa mzima. Kila mgombea kwenye mkoa anakotokea. Tutapunguza sana matumizi ya hela. Na kwa madiwani, hivyo hivyo wa viti maalum.
Baada ya kupigiwa kura, vikao vya uteuzi vitakaa kuteua mgombea wa urais na wabunge. Itasaidia kukijenga Chama cha Mapinduzi. Mchakato huu una faida kubwa:
Mosi, unapunguza rushwa.
Pili, unaongeza ushiriki wa wanachama kuchagua wagombea wao.
Tatu, unakisogeza chama kwa wanachama karibu zaidi kwa kushiriki kwao kupiga kura za maoni za urais.
Mwisho, inasaidia mgombea atakayeteuliwa kutotumia nguvu kubwa kumnadi.
Ahsante kwa kunisoma.
NB: Ushauri wa Watanzania kuhusu uchaguzi mkuu wa 2025 uzingatiwe kabla hatujafika mbali. Nchi ni yetu sote, vyama visitugawe.
Namaliza na neno:
"Usiwanyime watu mema yaliyo haki yao, ikiwa katika uwezo wa mkono wako kuyatenda."
Mithali 3:27