Ushauri kwa CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri kwa CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Joblube, Mar 17, 2011.

 1. J

  Joblube JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 367
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Sisi Watanzania na mimi nikiwa mmojawapo hatuichukii CCM kama CCM bali matendo ya wengi wenu angalau wangekuwa waovu wachache mmekuwa wengi mno. Mmeshashindwa kuongoza nchi na sasa hata kusimamia yale mambo ya msingi yaliokuwa yanatuunganisha wa TZ kama kutojadili upuzi wa kidini na kikabila mmeshindwa badala yake mmeanzisha nyinyi petrol hii ya kuingamiza TZ kwa maslahi ya uongozi kweli mmefikia ukingoni na watu wamewachoka, mmepoteza dira kwa sababu ya kuwa na watu wengi wasio na maono. Hivi mpaka imefikia watu wanaweza kuliwekea gari la kiongozi wa nchi mafuta yaliochakachuliwa kweli kuna kitu tena hapo. Mkumbukeni Mwalimu alisema serikali corupt inatumikishwa na wafanyabiashara nawasihi tusifike huko kama dalili zinavyoonyesha. Ushauri wangu ni huu mmepoteza mwelekeo na dalili zinaonyesha si rahisi kurudi kwenye mstari ni vema hasa rais akaanza kuweka mazingira ya upendo na vyama vingine na kuwaandaa watu wa chama chake kisakologia kuwa CCM si lazima itawale milele ili hata ikatokea CCM ikashindwa kwenye uchaguzi ujao uondoke na heshima na kuliachia taifa amani. Tujitofautishe na kenya na Zimbabwe hili linawezekana tukiamua kwa kuwa alama za nyakati zimeshaonyesha mtapinga tuu kwa sababu sikio la kufa halisikii dawa lakini ukweli ni huo kila ukipita hata wazee waliokuwa wanawaunga mkono wamewachoka kwa sasa. Jamani uongozi ni dhamana mmepewa tuu kwa muda tafakarini na mchukue hatua kwani mkiwa kama sisi mnotuongoza kwa sasa kuna ubaya gani au sisi mnatuona kama tuko jela ndio mkatae kuja huku?.
   
Loading...