Ushauri kwa Askofu Gwajima

Mangwea1900

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2025
Posts
2,485
Reaction score
3,224
Siku ulipoanza kusimama katika majukwaa ya kisiasa ndipo nilipopata shida moyoni kuhusu mahusiano yako na Mungu. Siasa na imani za dini ni sawa na mafuta na maji. Dini lengo lake kuu ni kuwaelekeza watu kufika mwisho mwema baada ya maisha ya hapa duniani.

Unachokifanya kwa sasa unaendelea kujiharibia kwa wenye kujua neno.

1. Mtumishi hatakiwi kuwa mwanaharakati.

2. Mtumishi wa Mungu hapaswi kuwa mwanasiasa.

3. Mtumishi wa Mungu vita vyake ni vya kiroho sio mwilini.

4. Mtumishi wa Mungu huongozwa na roho wa Mungu peke yake katika kila anachokifanya.

Katika video zako YouTube Askofu Gwajima inaonekana unajipendekeza au kujificha kwa kujidai unatetea maslahi yao ili hali wapo waajiriwa wa kada za chini wana changamoto kuliko ukianzia kwa vibarua katika viwanda na makampuni binafsi ukiachilia mbali walimu wauza visheti.

Hotuba zako unaongea kiswaenglish huku kwetu uswazi tunaona unajidai na unalenga daraja fulani la wananchi.
Askofu Gwajima, tubu dhambi zako kwa kumsikiliza roho wa Mungu na urudi kufanya kazi madhabahuni umeingia mtegoni ;"Nitampiga mchungaji, na kondoo wa kundi watatawanyika."— Mathayo 26:31/Zekaria 13:7

Yoeli 2:12-13
“Lakini hata sasa, asema Bwana, nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, kwa kufunga, na kwa kulia, na kwa kuomboleza; rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, mkamrudie Bwana, Mungu wenu; kwa kuwa yeye ni mwenye neema na rehema, si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa fadhili, naye hughairi mabaya.”
Aliye na masikio na asikie
 
Mtumishi hatakiwi kuwa mwanaharakati.
Niwapi ulisoma mtumishi wa Mungu hatakiwi kuwa mwanaharakati?

Au nini maana ya mwanaharakati?

Musa alifanya nini kwa farao?

Una hoja dhaifu sana mkuu.

Mtumishi wa Mungu wa kweli lazima serikali aikemee na kuionya inapoenda kinyume na Mungu mfano utekaji,Rushwa na mauaji.

Pitia maandiko haya kwa uchache kama ulivyoorodhesha.

1. Musa mbele ya Farao (Kutoka 5–12)
Musa alimkabili Farao akimtaka aachie Waisraeli. Alisimama kinyume na amri ya kifalme iliyokuwa ya kinyonyaji na dhalimu.


2. Nabii Nathani kwa Mfalme Daudi (2 Samweli 12:1–14)
Baada ya Daudi kumchukua Bathsheba na kupanga kifo cha Uria, Nathani alimkemea mfalme moja kwa moja.


3. Eliya kwa Mfalme Ahabu na Malkia Yezebeli (1 Wafalme 18; 21:17–24)
Eliya alimkosoa Ahabu kwa kuacha maagizo ya Mungu na kuabudu sanamu, pia kwa kupora shamba la Nabothi.


4. Yohana Mbatizaji kwa Mfalme Herode (Marko 6:17–18)
Yohana alimwambia Herode waziwazi kuwa si halali kwake kumchukua mke wa ndugu yake, jambo lililompelekea kufungwa na hatimaye kuuawa.


5. Mitume mbele ya Baraza la Wayahudi (Matendo 4:18–20; 5:27–29)
Waliambiwa wasihubiri kwa jina la Yesu, lakini walijibu: “Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu.” Hii ilikuwa changamoto ya moja kwa moja kwa mamlaka ya kidini na ya kisiasa.
 
Mtume paulo hakufumbia macho udharimu kwa watawala

Mtume Paulo

Alihoji mamlaka ya kumchapa bila hukumu akiwa raia wa Kirumi (Matendo 22:25–29).

Alimwambia Gavana Feliksi kuhusu haki, kiasi, na hukumu (Matendo 24:24–25).

Yesu Kristo Kristo mwenyewe hakukubali dhuruma.

Aliwaita viongozi wa kidini wanafiki (Mathayo 23:13–33).

DANIELI ALIMUONYA MFALME BILA WOGA WOWOTE.
Nabii Danieli
alimwambia Mfalme Nebukadneza atubu dhambi zake na kufanya haki (Danieli 4:27).

Nabii Amosi alikemea viongozi kwa kuwakandamiza maskini (Amosi 5:10–15).

Nabii Nathani alimkemea Mfalme Daudi kwa uzinzi na mauaji (2 Samweli 12:1–14).

Nabii Isaya aliwalaumu viongozi waliopotoka waliopendelea rushwa (Isaya 1:23; 10:1–2).

Hapo ndo mapre na maaskofu aroma wanabaki kuwa na uhalali wa kuwa wasomi na wenye akili zaidi.
 
Huo utumishi wa kutafuta riziki.

Ufu 3:15-16​

Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.
 
UONGO SIO KWELI
1.Mtumishi wa Mungu wa kweli na nabii wa Mungu wa kweli, Anakemea maovu...kama YOHANA mbatizaji alivyomkemea mfalme HERODE waziwazi.

Kama YONA alivyotumwa nchi ya NINAWI kuionya iache maovu Mungu ataiangamiza,

Kama NUHU alivyo onya

Kama mitume na manabii wengi kina ISAYA ,paulo na wengine wengi sana,hakuna kuhani,au mitume au manabii wa mwanzo ambao hawakukemea ukiukwaji wa haki,hakuna ambao walikuwa MACHAWA.
zaidi ya yote wengi walichukiwa na wafalme wasiotenda haki,wengine walifungwa magerezani,na wengine waliteswa na kuuwawa kwa KUKEMEA MAOVU...nabii wa kweli wa Mungu mara nyingi hapendwi na viongozi wafalme wasiotenda HAKI/waovu.
Ukiona kiongozi wa dini ni anapendwa sana na kusifiwa na kiongozi au mfalme asiyetenda HAKI ujue huyo ni nabii au mtume au kiongozi feki..wa mchongonwa uongo.

Naamini kiongozi Gwajima anaongozwa na roho wa Mungu.

Sio kweli kwamba mtumishi wa Mungu hapaswi kuwa mwanasiasa ,wafalme wote walikuwa wanasiasa mfalme DAUDI,SULEIMANI,hata Musa,yusufu tena walikuwa maraisi au wafalme kabisa..sio ubunge ..akina DANIELI..akina YUSUFU yosefu joseph walikuwa waziri mkuu nchi ya MISRI n.k

UNASOMA BIBLIA GANI.??

View: https://youtu.be/d8Z2Pki-9kE?si=vmfSZOjwkc3chy-B
 
1. Yohana mbatizaji alikatwa kichwa na hata alipowekwa ndani Yesu hakuenda kumtembelea
2. Wote uliowataja walionya watu kuhusu adhabu ya Mungu kutokana na dhambi. Kwenye siasa hakuna dhambi bali jinai, nk.
3. Daudi alikuwa ni mfalme na hakuwa mtumishi wa Mungu Moja kwa Moja wa madhabahuni ndio maana alipopiga chabo na kumchukua mke wa mfanyakazi wake Mungu alimtuma nabii
Unajua kazi ya askofu mkuu?
Askofu Gwajima anaonya Nini? Umesahau wakati anaanza kuonya alikuwa ni mbunge?
 
Wewe unaoona anayosema Askofu Gwajima ni kuonya kama walivyoonya wengine au anaongea umbea?
Kuna utofauti gani katika ya Askofu Gwajima na Mange Kimambi au Polepole?
 
Utawala wa kifalme enzi hizo ni tofauti na ilivyo sasa. Sasa hivi tunapiga kura lakini kwa wafalme walipatikana tofauti na manabii walikuwepo kama jicho na sikio la Mungu kwa wafalme.
2 Timotheo 2:24-"Tena mtumishi wa Bwana haitakiwi kuwa mtu wa kushindana, bali awe mpole kwa watu wote, ajuaye kufundisha, mvumilivu."
 
Gwajima ni tapeli fulani wa mjini aneyetapeli kwa mgongo wa kanisa,hukumu yake ni bakora nyingi zisizo idadi.
 
Gwajima ni tapeli fulani wa mjini aneyetapeli kwa mgongo wa kanisa,hukumu yake ni bakora nyingi zisizo idadi.
Mungu atamhukumu asipotubu na sio bakora za kibinadamu
 
Kuna wakati unaweza sema Mungu alifanya dhambi kumuumba mtu mweusi.
Untaka yeye awe anakema mapepo tu yasio onekana.
Halafu akae kimya kwa mafisadi, wala rushwa na wauaji anao wajua?

Eti vita vyetu si vya kiroho, kwani wakaloni mlipambana nao kwa maombi?
 
1.Yohana alikatwa kichwa kwa kukemea maovu,YESU alisema katika wanadamu hakuna aliye mkuu kushinda yohana mbatizaji,Yesu hakwenda kumuona kimwili ila alimtumia ujumbe kuwa sasa vipofu wanaona na viwete wanatembea watu wanafungulia na roho ya BWANA ilikuwa na YOHANA..sijaelewa point yako unaposema Yesu hakwenda kumuona Yohana mbatizaji gerezani..una maanisha ?hakuwa mtumishi wa Mungu au ??

2.wote niliowataja walionya kuhusu adhabu ya Mungu ,si ndicho Gwajima anachokisema Mungu atahukumu kwa HAKI watu wanaomba na kufunga novena wanaomba Mungu ,JINAI na sheria za nchi si ndicho anachosema GWAJIMA amefuatulia vyombo vya sheria ,anazungushwa tu,siasa ni koti tu ila binadamu mbele za Mungu anasimama kama binadamu hata awe mfalme na Mungu anamuhukumu kwa kadiri ya dhambi zake kwa HAKI,HUKUMUNZA MUNGU ...MENE MENE TEKELI NA PERESI...hata ufalme anaweza kuupokonya kuukomesha akampa mwingine,na adhabu za Mungu ni za haki,mfalme nebucchadnezzer si alipewa adhabu ya kutupwa porini kama mnyama.
3.DAUDI HAKUWA MTUMISHI WA MUNGU REALLY?? mpakwa mafuta wa BWANA ,nini maana ya mtumishi wa Mungu kwa tafsiri yako??hata TINDU LISU ni mtumishi wa Mungu kuliko hata maaskofu wengi wa mchongo..mtumoshi wa Mungu ni nani??sio lazima usimame madhabahuni??
 
1.Daudi hakuwa nabii bali mfalme. Soma vizuri biblia utaelewa tofauti na majukumu yao. Zaidi fuatilia sababu ya uwepo wa wafalme, manabii na waamuzi na baada ya Yesu kuja hawakuwepo tena.
2. Mkuu kila mtumishi wa Mungu ana mission yake. Mfuatilie Mwalimu Mwakasege na Askofu Kulola (RIP) utajua naongea nini.
Tuache ushabiki na tusimamie kweli. Kwa kusikiliza maneno anayoongea Askofu Gwajima ni mazuri masikioni na kwenye mwili wa hisia za ushabiki lakini kiroho haiko sawa
 
La Mungu litasimama tu,
Sisi ni watazamaji na waombea nchi yetu.
Tunasubiri majibu yatakayokuja kutokana na jitihada za Gwajima na haya maneno yako.
 
1.YESU alisema katika wanadamu wote HAKUNA aliye mkubwa kuliko YOHANA MBATIZAJI,
unaposema Yesu hakwenda kumuona una maanisha nini kwamba Yohana mbatizaji hakuwa mtumishi wa Mungu au alikuwa mdogo kiroho au??
tena Yesu alimtumia ujumbe tazama vipofu wanaona,viziwi wanafunguliwa wanasikia ,viwete wanatembea..alimtumia ujumbe akiwa getezani..1) pointi yako kuhusu yohana mbatizaji ni ipi??

2.ndicho GWAJIMA anachokifanya kuonya juu ya adhabu ya Mungu, na Gwajima anasema alifuata taratibu zaa kisheria za vyombo vyetu vya haki...AKAZUNGUSHWA ZUNGUSHWA hata BARUA RASMI hawajapewa zaidi ya taarifa za mitandao,amefuatillia mamlakaa zote ngazi zote za kisheria hakuna jibu ndio akaamua kumshitakia Mungu,na RC wakafunga na kumuomba Mungu..Mungu haangalii cheo cha kisiasa ila anahukumu binadamu kutokana na dhambi hata awe mfalme...MENE MENE TEKELI NA PERESI...reffet mfalme Nebucchadnezzer.. BABELI

3.DAUDI HAKUWA MTUMISHI WA MUNGU REALLY ?you cant be serious ?DAUDI mpakwa mafuta wa Mungu,ameandika sehemu kubwa ya biblia,ametembea na Mungu ,labda kwa tafsiri yako nini MAANA YA MTUMISHI WA MUNGU??
Tindu Lisu mwenyewe ni mtumishi wa Mungu kuliko hata maaskofu wa mchongo tulionao machawa.?sio lazima uvae kanzu na usimame madhabahuni uwetumishi wa Mungu,kiasili binadamu wote ni waja ibada wa mwenyezi Mungu ninwatumishi wa Mungu kama isingekuwa SHETANI kuwapotosha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…