Ushauri kwa ambao hawajaoa au kuolewa

John Joba

JF-Expert Member
Jul 25, 2018
343
500
Kabla ya KUONA au KUCHAGUA mchumba mwombe Mungu kwanza kuwa "unamuhitaji mchumba ambaye utamwoa au atakuoa na kutengeneza ndoa pamoja naye kwa utukufu wa Mungu".

Pia mwambie Mungu kwamba, "Mungu katika ndoa utakayotupatia ujitwalie watumishi wako", maana neno la Mungu linasema, "Mavuno ni mengi lakini watenda kazi ni wachache". Kwa maombi hayo na matamanio hayo utakuwa umeinusuru ndoa na familia yako kutoka mikononi mwa Shetani.

Hapo Mungu atakusikia na atakubariki wewe na mke au mume wako na watoto wenu.

HITIMISHO: Maombi ni ufunguo. Unapomwomba Mungu akupe mke au mume anakupa kwa sababu anakuwa na makusudi na ndoa yenu.

Mwanzo 24: 13-17 "Niko hapa kando ya kisima ambapo binti za wenyeji wa mji huja kuteka maji. Basi, msichana nitakayemwambia atue mtungi wake wa maji anipatie maji ninywe, naye akanipa mimi pamoja na kuwanywesha ngamia wangu, na awe ndiye uliyemchagulia mtumishi wako Isaka.
Jambo hilo litanionesha kwamba umemfadhili bwana wangu. Kabla hajamaliza kuomba, mara Rebeka, binti Bethueli, mwana wa Milka, mkewe Nohari, ndugu yake Abrahamu, akafika amebeba mtungi wake begani. Msichana huyo alikuwa na sura ya kuvutia sana, na bikira ambaye hakuwa amelala na mwanaume yeyote. Basi akateremka kisimani, akaujaza mtungi wake maji na kupanda. Ndipo yule mtumishi akaharakisha kukutana naye, akamwambia, "Tafadhali, nipatie maji ya kunywa kutoka mtungi wako."


Mungu akubariki sana katika safari yako ya maisha.
 

John Joba

JF-Expert Member
Jul 25, 2018
343
500
Kweli kabisa yanahitaji hekima kubwa na baraka za Mwenyezi Mungu. Bila hivyo ni changamoto.
 

jipu

JF-Expert Member
Apr 20, 2015
1,893
2,000
Kweli kabisa yanahitaji hekima kubwa na baraka za Mwenyezi Mungu. Bila hivyo ni changamoto.
Watu wawili waliokua katika malezi na tamaduni tofauti kuishi pamoja ni changamoto Mungu atusaidie.

"Typed with my thumbs."
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom