Uchaguzi 2020 Ushauri kwa ACT - Wazalendo juu ya kampeni za Uchaguzi

MANILABHONA

JF-Expert Member
Apr 1, 2015
462
350
Habari wenye chama chenu, naamini mnafuatilia mikutano ya Mgombea wenu wa Urais kama mimi nifanyavyo kwa wagombea wa vyama vitatu maarufu. Nilitamani kuongea na kiongozi wa Chama mara baada ya uzinduzi wa kampeni, bahati mbaya simu yake ilikuwa bize haikupokelewa.

Niliyoyaona kwenye hotuba ya mgombea Bernard Membe:

1. Hajaichambua vizuri katiba ya ACT Na ilani yake: Kwa wakati tulio nao hakuna katiba bora kama ya ACT, hata ilani yake ni nzuri. Ingawa kwenye ilani hapa kidogo ya CCM ni nzuri zaidi.

2. Ushauri wangu afanye hivyo haraka iwezekanavyo, kwani nyota njema huonekena asubuhi. ajikite kwenye sera zaidi.

3. Ajikite katika kuelezea matatizo ya wananchi na namna atakavyoyatatua, kitaifa zaidi.

4. Akwepe kuongea kwa mlengo wa maeneo, kanda ya kusini n.k, inamfanya aonekane ana mawazo kama ya wenzake ya ukanda,ukabila

5. Asisahau mapungufu ya washindani wake:

Haya ayaweke mbele na bayana na yeye atafanya vipi tofauti na wenzake:

Mfano
a) Kuondolewa utu na heshima ya mtu, tena hadharani

b) Uongozi kukosa maadili hasa kwa wazee na kuongea lugha yenye kufedhehesha/ matusi.

c) Kutetereka kwa umoja wa kitaifa, ukanda,ukabila kudhihiri katika teuzi na uongozi

d) Maendeleo kuwabaguaa baadhi ya wananchi/ maeneo Mikoa ya pembezoni: Lindi, Mtwara, Ruvuma, Rukwa, Kigoma, Manyara, n.k Cha ajabu maendeleo kulazimishwa kijijini Chatto, MWANZA, GEITA na maeneo yanayofanana nayo

e) Kuuawa, kupotea, kutekwa au kutishiwa/kupigwa risasi kwa Watanzania kunakofanywa na watu wasiojulikana

Kwa leo yangu ni hayo machache, mkipenda mengi naweza kuwashauri

Mkiona mazuri chukueni, mkiona mabaya yapuuzeni/yaacheni
Wasalaamu,

Mwanachama halisi wa CCM ya JK Nyerere, sio hii ya kisasa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom