Ushauri: Kupoteza dira/mwelekeo...

Itoye

JF-Expert Member
Sep 29, 2017
531
1,024
Wakuu, Salaam.

Mtu aliyepoteza dira/mwelekeo ktk maisha, kazi au biashara, sifa au tabia zake ni zipi? Au ni vitu gani vinaonekana kwa mtu huyo vinavyoashiria kuwa hayuko kwenye right track?

Thanks in advance kwa elimu nitakayoipata hapa.

Naomba kuwasilisha
 
-Pesa haipati kama mwanzo!

-Amedumaa katika uchumi. Juzi alikuwa na Gari, ameuza, amenunua Pikipiki, ameiuza, amenunua Baiskeli, Mwisho hata hiyo Baiskeli ameiuza.
Sasa yupo yupo tu.
Huo ni mfano tu nimetoa.
 
1.Kila mtu anamchukulia kama adui yake.
2.Anakuwa hapendi mafaniakio ya wengine
3.kila analoanzisha halifanikiwi
4Mda wote anaponda wenzake.
5.Ni mwepesi kupanic
 
Kama alikua na mke sasahivi yupo single
Kama alikua na gari sasahivi litakua limepaki garage,kawekeza kwa mtu au ameshaliuza
Kama alikua wa kupendeza sasahivi anavaa nguo siku3 hadi4 hajabadilisha
Hapendi maendeleo wala mafanikio ya wengine
Muda wote yeye ni kukosoa tu pia anakua mtu wa kupanic kwa mambo madogo
Anajitenga na marafiki zake wa zamani
Wengine wanajifunza kunywa pombe anakua anashinda bar kama mdangaji baadae anaaza kushinda kilabuni kwenye mataptap
 
Mkuu asante kwa hii elimu. Mtu wa namna hii anasaidikaje?
 
-Pesa haipati kama mwanzo!

-Amedumaa katika uchumi. Juzi alikuwa na Gari, ameuza, amenunua Pikipiki, ameiuza, amenunua Baiskeli, Mwisho hata hiyo Baiskeli ameiuza.
Sasa yupo yupo tu.
Huo ni mfano tu nimetoa.
Mkuu huu nauita mfano hai, asante sana.
 
1.Kila mtu anamchukulia kama adui yake.
2.Anakuwa hapendi mafaniakio ya wengine
3.kila analoanzisha halifanikiwi
4Mda wote anaponda wenzake.
5.Ni mwepesi kupanic
Shukrani mkuu moesy kwa haya madini, wakati mwingine mtu unaweza ukadhani uko sawa kumbe kitambo ulishatoka kwenye reli.
 
Mkuu asante kwa hii elimu. Mtu wa namna hii anasaidikaje?

Mtu wa kwanza kumsaidia ni partner wake,amueleze ukweli hali halisi pia ampe nguvu ya ushawishi ya kuanza upya,maana kuanza upya sio ujinga.

Wazazi pia wananguvu ya ushawishi wanaweza kuongea na mtoto wao kuhusu hali halisi ya maisha ya mtoto wao na changamoto za maisha kiujumla..hapa jamaa anaweza kujubali matokeo na kunyooaha mikono juu na kuanza upya..

Mwisho ni yeye mwenyewe kukubali kwamba uwezo wake umefikia hapo sasa awe tayari kuanza upya
 
Back
Top Bottom