Ushauri kuhusu Subara legacy wagon 2006

nickag

Member
Jan 2, 2016
64
29
Mimi ni kijana muangaikaji hapa town mepata gari aina ya subaru legacy wagon sasa nikua nauliza hii gari inadumu hasa upande wa engine maana ni turbo chargred engine na fuel consumption ikoje..
 
Subaru Legacy Wagon ya mwaka gani?? Japo kwa kijana muhangaikaji hili siyo aina ya gari unalo hitaji..
 
Mkuu Hongera kwa kupata Subaru... Me sina hiyo Legacy.. Nina forester hivyo kwa uzoefu wa forester nilio nao in kwamba... Subaru haitaki magumashi, si kila fundi anaweza kutengeneza tu, service on time na oil nzuri, spea zake ziko juu sana Ila zinadumu, ni nzuri sana kwa Safari ndefu.. Kuhusu mafuta inategemea na uendeshaji wako na ukubwa wa engine, ukiwa mtu wa kurotate sana yaani unaenda 3,4,5 utaingiliwa tu hamna namna... Challenge iliyopo kwenye Subaru drivers ni kwamba tunapenda ligi na kusikiliza mnyama anapounguruma na kucheua, ukiendesha kawaida mafuta nayo yanakua kawaida Kama Magari mengine tu.
 
subaru ni gari nzuri na imara sana.Kwa masafa utaipenda ina stability nzuri sana barabarani.Ila tu spare zale zipo juu kidogo japo mpaka uharibu subaru inachukua muda sana.
 
Mimi ni kijana muangaikaji hapa town mepata gari aina ya subaru legacy wagon sasa nikua nauliza hii gari inadumu hasa upande wa engine maana ni turbo chargred engine na fuel consumption ikoje..
Jiandae kulipa faini sana kwa mwendo kasi wake,tengeneza urafiki mapema na matrafiki
 
Mimi ni kijana muangaikaji hapa town mepata gari aina ya subaru legacy wagon sasa nikua nauliza hii gari inadumu hasa upande wa engine maana ni turbo chargred engine na fuel consumption ikoje..
Mkuu hongera kwa kuwa na gari nzuri. Hata mimi namiliki gari kama hiyo hiyo ila ya 2005. Kwa ujumla ni gari nzuri sana katika mambo haya
1. Ulaji mafuta
Kama alivyoandika mtangulizi mmojawapo hapo juu. Ukiwa mtu wa mara RPM ipo kwenye 3 mara 5 mara umerudi 2 lazima utaona inakula sana mafuta. Inataka nidhamu ya uendeshaji kama dreva anaejua gari na sio uendeshaji wa ujana hapa na hapa umevuta mafuta n.k
2. Spare na mafundi
Ni kweli hizi gari hazitaki mafundi wababaishaji na vipuri vile vile vipo lakini bei ipo juu kidogo ila ni 'genuine'. Kwa mfano oil filter inaweza kuwa kati ya Tsh 30,000 ya kawaida hadi Tshs 70,000 genuine, kufanya service ya gearbox inafika hadi laki 5 kwa ufundi, gearbox hydrolic ya subaru maalum lakini unabadilisha baada ya km laki 1.
3. Mwendo
Ipo poa sana kwani ni gari yenye balansi, nguvu na utulivu barabarani.
 
Back
Top Bottom