Ushauri kuhusu sim card na micro-sd

Ushauri kuhusu sim card na micro-sd

Serena

Senior Member
Joined
Apr 4, 2014
Posts
124
Reaction score
125
Naomba kuuliza kwa wale wataalam wetu wa mambo ya simu au yeyote mwenye ufahamu naomba anisaidie katika hili. Ninasimu yangu inatumia Micro-SD na nilikuwa naishi nje ya nchi lakini sasa nataka kurejea TZ na kwa msingi huo nitahitaji kutumia laini zetu za kawaida za Voda, Tigo, n.k. Sasa swali langu ni kwamba, vipi hizo laine za simu za hapo Tanzania naweza kupata Micro-sd nitakayoweza kutumia kwenye simu yangu??? Kwani simu yangu ina sehemu ndogo cha line kiasi kwamba hizo normal lines za Vodacom, Tigo, n.k za hapo TZ haziwezi kuingia. Au kuna utaalam wowote wa kukata hizo kadi na kuwa micro ili iweze kuingia kwenye simu isiyotumia laini zenye ukubwa wa kawaida?

Naombeni ushauri katika hilo.
Ahsanteni na Kristmas njema kwa wote mtakaosoma uzi huu.
 
Zinakatwa na kueneza/kufit fresh kabisa.
Mashine za kukata zipo zinazokata mini na micro so ni wewe mwenyewe.

Karibu
 
Mkuu SERENA, hivi hujui utandawazi wewe? Hata hapa kijijini kwetu Nakapanya Ntwara wanakata kwa machine hizo micro sim card!!
 
Watu wa majuu hao wanaulizia nyumbani kwao kama teknolojia hii imefika
 
Mkuu kukujulisha.....ni kwamba hata huko kwenye micro sd tushatoka tupo kwenye nano sim......na mimi nipo Yaeda.......sasa sijui mkuu ulikuwa una mtazamo gani labda.........
 
Mkuu kukujulisha.....ni kwamba hata huko kwenye micro sd tushatoka tupo kwenye nano sim......na mimi nipo Yaeda.......sasa sijui mkuu ulikuwa una mtazamo gani labda.........
inaonekana mkuu umeadvance,hiyo imenipita kushoto
 
Nunua line mpya inakuja imekatwa kabisa au renew uliyonayo kwa Tsh 500 utapata mpya iliyokatwa
 
Back
Top Bottom