Ushauri kuhusu Nissan Dualis

Bila kuwachosha, niende kwenye mada.

Nimetokea kuipenda sana hii gari, na ninataka kuinunua.

Lakini kabla 'sijajilipua', ningeomba mawili matatu kuhusiana nayo kutoka kwa wataalam wa magari au watu waliowahi kumiliki Nissan Dualis.

Je, ni kweli ENGINE na GEARBOX za hii gari ni PASUA KICHWA SANA..?!

Vipi uhimilivu wake kwenye ROUGH ROADS..?
Manake ITAPAMBANA na kilometa 25 za rough road kabla ya kugusa lami mara 3 kwa wiki!

Vijiweni maneno ni mengi, nimekuja humu nakiamini kuna WAJUZI na WATAALAM!

Natanguliza shukrani zangu kwenu.

Cc: Extrovert RRONDO Offshore Seamen JituMirabaMinne Boeing 747 chilubi
Binafsi napenda Nissan kuliko Toyota. Engene zao ni imara zaidi ya za Toyota kama unafuata matakwa yake ya service hasa oil. Na ukizingatia hutogusa hiyo engine miaka mingi. Haitumii hii mikanda ya mpira(timing belt) inakwenda kwa minyororo(chain kama za baiskeli) na ndiyo inahitaji oil safi kwa kulainishwa muda wote.
 
Toleo gani na ulinunua kwa bei gani ?

Umenunua na kuitumia muda gani?!

Wewe ndie uliinunua na kutumia kwanza ama ulichukua mikononi mwa mtumiaji aliyeinunua, yaani swali langu ni gari imepita mikononi mwa watu wangapi kabla yako tokea iwe imported?!

Nipe history fupi ya service ya hiyo Nissan Dualis yako, ni lini ulianza experience shida ya gear box?!

Umefanya vipi diagnosis na kujua inashida?!

Ni muda gani umepita tokea ugundue tatizo na ni hatua gani umechukua hadi sasa?!
Gearbox yake ni mbovu kishenzi.

Whether umenunua mpya au used.

Whether umefanya service kwa makini.

Whether umefanya diagnosis.

Haijalishi.
 
Umemuuliza maswali magumu sana!

Akikujibu nishtue... niko nimekaa paleee!!!
 
Binafsi napenda Nissan kuliko Toyota. Engene zao ni imara zaidi ya za Toyota kama unafuata matakwa yake ya service hasa oil. Na ukizingatia hutogusa hiyo engine miaka mingi. Haitumii hii mikanda ya mpira(timing belt) inakwenda kwa minyororo(chain kama za baiskeli) na ndiyo inahitaji oil safi kwa kulainishwa muda wote.
Watu wote mje muisome hii comment hapa...
na muisome kwa sauti!!
 
Gearbox yake ni mbovu kishenzi.

Whether umenunua mpya au used.

Whether umefanya service kwa makini.

Whether umefanya diagnosis.

Haijalishi.
Sio kweli. Unaposema gear box yake ni mbovu basi hizi zote zilizopo barabarani muda huu zisingekuwapo. Na mimi hadi muda huu nakaribia kufunga miaka miwili na zaidi sijakutana na shida yoyote.

Wewe unaongea from what source of experience. Maana ukisikiliza mafundi waongo na wamiliki wazembe watatu ni inatosha kabisa kukuharibu mtazamo kuhusu gari fulani.

Kiukweli hiki ulichosema hakina ushahidi na umetunga. Hizi gari kwasasa zinaanza kufanana na IST kwa kuonekana kwa wingi barabarani. Sasa ingekuwa ni mbovu tusingeona namba E ya hizi gari. Na kama haujui hizi gari zimeanza kuingia na namba B zimetembea na C D na sasa Zinaingia na E. Gari zenye usumbufu huwa zinapotea mapema sana sokoni.

So hebu acha kupotosha mkuu.
 
Kweli kabisa hao wajuaji uchwara na utakuta hata hajawai kumiliki gari zaid ya story za vijiweni tu
 
Nikagari kazuri sana nakatumia mwaka wa nne. Miaka miwili nimekitumia location ya milimani na barabara ni mbovu, kipindi cha mvua ndo yenyewe ilikuwa inapandisha kijijini tuu. Usikose kwenye service tuu ambayo ni simple Kwa gari mpya ukiagiza inakuwa ni kumwaga oil na kubadili filter. Make sure unatumia oil iliyoandikwa kwenye kitabu chake. Huta jutia. Kwenye oil sijui ya gear box usimuachie fundi akwambie ubadili inakaa hata km 200,000 huko na ukibadili weka yakwake special iliyoandikwa kwenye kitabu. Sijawahi badili kitu kingine kwenye gari na haligongi gongi chini.
Kabda sijasahau petrol nayo linachagua hakikisha unaweka ya total hizi stetion Za mafuta nyingine Changamoto mafuta yanakuwaga machafu Mara nyingi. Gari ndo naitumia kila siku na safari inapiga boda tu boda wakati wowote. Wanaoaribugi magari ni mafundi wetu wa mchongo.

Ushauri wa muhimu niliowahi pewa ni kuwa na Fundi wauhakika mmoja anayeijua gari yako na mapungufu Kama yapo.
Ni gari nzuri sana halafu zimekaa kishua sana binafsi naipenda sana na ndo ilikua gari ya ndoto yangu baada ya kuchoshwa na vitz
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom