Ushauri kuhusu Nissan Dualis

Naomba ufafanuzi kwanini nisiichukue wakati UMEISIFU ni nzuri..?

Kuhusu gearbox, huku vijiweni kwetu wanasema gearbox yake ni CVT ambayo wanasema ina kama 'maruhani!'
CVT ni gear box ambazo hazitaki kuchanganyiwa oil. Oil zake ni specific. Kuna CVT oil kwaajiri ya Toyota brands kama Toyota Lumion, Vits, Wish, Vanguard etc. Na ipo CVT ya Nissan Dualis, Nissan Xtrail, etc ambayo ipo specific kwaajiri ya gari husika.

Sasa zingatia kutochanganya oil ili uwe salama.
 
Hii gari ni nzuri na ipo comfortable, na hata kwenye njia mbovu inapita.
Sema kikubwa ni service, usizidishe mda. Na unapofanya service uwepo kumsimamia fundi.

Kwa upande wangu nilipata taarifa za kimakosa mtandaoni kuwa usibadilishe engine oil mpaka rangi ibadilike, hii ilifanya niue engine, na ikabidi kwenda kuweka engine nyingine na ninaifanyia service ndani ya mda na haijasumbua hadi leo. (Engine ikifa sikushauri kufanya overhaul, chukua fundi wako unayemwamini katafute engine nyingine)

Cha msingi weka recomended oils, kwenye engine oil 5w30 ndo nzuri, usije kumsikiliza fundi anakuambia sijui SAE-40 au nyingineyo.

Kingine jiandae kwa gharama ya spare zake, zipo juu kidogo, ila ukiweka unasahau.

Shida yake nyingine ni vitambaa vya kwenye paa na milango kutoka, ili wapo wanaorudishia.

Vitu vingine nilivyowahi kubadilisha tangia nianze kuitumia; (Inaenda miaka miwili sasa)
1. CV Joint na rubber boot
2. Brake pads
3. Sensor ya ABS
4. Bushes
Asante kwa kutupatia uzoefu wako, mkuu.

Wengi tutafaidika!
 
Mbina husem mambo mengine ya ndan zaud kuhusu hii gar?
Eg. Ukipata matatizo ukataka kuiuza Resale Value yake ipo chini hivyo kuuzika nako inasumbua bciz watu wanhofu na kampun ya Nissan.
Nimeshuhudia moja imeuzwa hapa kitaa chetu kwa 10M na modelbya 2008
Mpango wangu ni kuinunua ili niitumie.

Kwenye mipango yangu huwa sijitabirii kukwama,..

Lakini ikinitotokea dharura, na option pekee ya kunivusha ikawa ni kuuza mali yangu; nitaangalia ukubwa wa dharura yangu tu!

Mwenyezi Mungu atuepushe na mabalaa na mitihani ya kuturudisha nyuma kimaisha... aamiyn!
 
Ulishaona gari ina muonekano mzuri, iko comfortable halafu wamiliki wake wanakimbilia kutaka kuiuza haraka haraka, tena kwa bei ndogo, basi wewe jua tu kuna kitu hakiko sawa kiuchumi kuhusu hiyo gari.
Hizi hapa chini ni mojawapo ya gari zenye hiyo tabia.
1. Nissan Dualis
2. Nissan Xtrail
3. BMW
Tatizo la kiuchumi tusiilaumu gari ...

Tutafute hela!
 
Tz tuna umaskini sana hakuna gari mbaya kikubwa service hizo subaru unazoshauriwa kununua nazo zinahitaji service kwa wakati ww ukiona mtu anahoji sana kwenye kutaka kununua chuma bas hana hela na ushauri ni kwamba bora atumie usafiri wa uma binafsi hatoweza
Tutafute hela!

Tuache kulaumu magari!
 
Gari nzuri hautojutia. Sasa kilometers 25 za rough road wewe unaishije huko halafu upeleke gari kama hii huko?! Huko kuna gari zake. Hii gari haitaki mikiki ya makusudi.

Kwa dharula haina shida ila kama unataka kuisumbua kwa makusudi utakutana na gharam za service.

Kuhusu gear box na engine sio kweli. Hii gari ipo vema sana tu. Shida ni watu kuchanganya oili kuweka oil tofauti ya zile pendekezwa.

Hii gari ina oil yake special ambayo inawekwa kwenye gear box na special ya engine na zina nembo ya kampuni ya Nissan kabisa.

Sasa wengi wanaoziita mbovu sijui pasua kichwa. Mawili. Amenunua kwa mtu ambaye aliikosea adabu au yeye mwenyewe alikuwa hayupo makini ndio imemharibikia.

Ila yote kwa yote ni gari nzuri. Nadhani inafanya vema sana kimauzo zimenunuliwa sana kipindi hiki yaani katika gari utakutana nazo sana barabarani ni hii Nissan Dualis, IST, Subaru Forester XT kwa kutaja chache.
Shukrani sana mkuu, ubarikiwe!
 
CVT ni gear box ambazo hazitaki kuchanganyiwa oil. Oil zake ni specific. Kuna CVT oil kwaajiri ya Toyota brands kama Toyota Lumion, Vits, Wish, Vanguard etc. Na ipo CVT ya Nissan Dualis, Nissan Xtrail, etc ambayo ipo specific kwaajiri ya gari husika.

Sasa zingatia kutochanganya oil ili uwe salama.
Shukrani sana.

Wengi tunafaidika hapa!
 
Nunua Ila hakikisha kipindi chote unachokua unaimiliki uwe na paracetamol kopo 3 zile za kizamani moja unatembea nayo kwenye gar nyngne nyumban nyngne kazin
 
Nunua Ila hakikisha kipindi chote unachokua unaimiliki uwe na paracetamol kopo 3 zile za kizamani moja unatembea nayo kwenye gar nyngne nyumban nyngne kazin
Kwanini..?

Ina makelele sana yanaumiza kichwa au..?!
 
Mbina husem mambo mengine ya ndan zaud kuhusu hii gar?
Eg. Ukipata matatizo ukataka kuiuza Resale Value yake ipo chini hivyo kuuzika nako inasumbua bciz watu wanhofu na kampun ya Nissan.
Nimeshuhudia moja imeuzwa hapa kitaa chetu kwa 10M na modelbya 2008

Shida kubwa inakuja ukiwa umepata fundi ambaye sio mzoefu na gari za Nissan. Hapo atakuharibia gari na utaona gari ni mbaya.

Kwa upande wangu pindi ilipokufa engine kuna fundi alishauri kufanya overhaul, ila hakuwa mzoefu na aliweka vifaa duni, tatizo halikupona, nilianza kuichukia gari. Ilifika mda nikatamani hadi kuiuza.

Na mara nyingi ukitaka kuuza kitu pindi una shida mnunuzi atakulalia tu, maana anajua unahitaji pesa.

Ila nikampata fundi mzoefu na tukarekebisha, na ikatulia.

Cha msingi uwe na hela ya kuihudumia, uweke vifaa original na ufanye service kwa wakati.

Tatizo kubwa nililopata ni hilo la engine, mengine madogo ni kama rubber boots, ABS sensor, taa za breki kuungua, bushes. Na nadhani hii ni kawaida hata kwa gari nyinginezo.
 
Ndio. Hata mimi natumia.
Gearbox yake mbovu kishenzi
Toleo gani na ulinunua kwa bei gani ?

Umenunua na kuitumia muda gani?!

Wewe ndie uliinunua na kutumia kwanza ama ulichukua mikononi mwa mtumiaji aliyeinunua, yaani swali langu ni gari imepita mikononi mwa watu wangapi kabla yako tokea iwe imported?!

Nipe history fupi ya service ya hiyo Nissan Dualis yako, ni lini ulianza experience shida ya gear box?!

Umefanya vipi diagnosis na kujua inashida?!

Ni muda gani umepita tokea ugundue tatizo na ni hatua gani umechukua hadi sasa?!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom