Waterlemon
Senior Member
- Sep 2, 2016
- 143
- 199
- Thread starter
- #21
Unaishije na mama mkwe?!kila mtu akae kwake utashindwa hata kuangalia tv kifua wazi nyumbani kwako
Mkuu nahisi hukunifahamu vizuri. Hatukai nyumba moja na mama mkwe!
Unaishije na mama mkwe?!kila mtu akae kwake utashindwa hata kuangalia tv kifua wazi nyumbani kwako
Chukua wadogo zake mkeo wa kike uwalete. usikilize tena kama mama mkwe analalamika. Maana kama ni tamaa wao watakusumbua wewe....Mkuu nahisi hukunifahamu vizuri. Hatukai nyumba moja na mama mkwe!
Mkuu kama nimekusoma vizuri, umesema mnakaa miji tofauti na familia za pande zote mbili, kama ni kweli...mamamkwe anapataje taarifa kuwa wadogo zako wapo hapo kwako?
Inawezekana wife anamueleza mamake baadhi ya vitu ambavyo havimpendezi na hawezi kukwambia wewe kuogopa atakufitinisha na ndugu zako. Na ndio maana mamamkwe anakataa wao kukaa hapo. Lizungumze na wife ujue ana msimamo gani juu ya uwepo wa wadogo zako hapo nyumbani.
Ushauri, kama hali ya maisha inaruhusu kwa maana kwamba una nyumba yenye nafasi chukua ndugu wa kike wa mkeo muishi nae hapo nyumbani. Uwepo wake na wadogo zako unaweza kuepusha fitna ya wadogo zako na mkeo kipindi haupo.