Waterlemon
Senior Member
- Sep 2, 2016
- 137
- 178
Salamu wana JF,
Nimeamua kuja kupata maoni yenu wakuu kuhusu hili jambo ambalo linanikereketa moyoni.
Ni hivi waungwana, niko kwenye ndoa na mke wangu karibia mwaka wa pili huu. Nakaa mji wa mbali na wazazi na family wa pande zote mbili, na huku tulipo mie na mke wote tunafanya kazi. Mungu amejaalia ya kuwa amepata ujauzito tunatarajia kupata mtoto mwezi wa sita mwaka huu. Familia nzima limelifurahia hili.
Jambo la kukereketa ni kuwa mimi huwa napata safari nyingi za nje ya nchi kikazi mara kwa mara ambazo kawaida huwa zinanitoa huko kwa mda wa siku tatu mpaka wiki. Mara nyingi tukiwa sisi wawili tu nikiondoka kikazi kumuacha mke peke yake nyumbani huwa hamna tatizo. Tunaaminiana na tunaishi kwa harmony sana yaani hakuna ugomvi wala nini.
Tatizo kuna vipindi huwa ndugu zangu huwa wanakuja kukaa nami hapo nyumbani pamoja na mke wangu. Tena la zaidi wakija huwa wako katika harakati za kimaisha yaani mfano wamepata kazi karibu na nyumbani hivyo kujianzisha kimaisha huniomba kuja kukaa na mimi hapo nyumbani kwangu na mke wangu kipindi fulani ili wapate kujipanga na kutafuta mahala kwao. Tatizo katika harakati zangu za kikazi kipindi wakiwepo hapo nyumbani huwa naweza kupata safari ya kikazi na kuondoka.
Kiufupi nawaamini sana wadogo zangu wa kiume. Tumelelewa na kukuzwa kiheshima kwa desturi za kiislamu, na vile vile namuamini mke wangu. Tumepitia mengi kimaisha kiasi kwamba sidhani kama anaweza kutupa tulilonalo kirahisi rahisi. Hivyo hata nikiondoka kuwaacha, huwa hata sina wasi wasi kama jambo lolote baya linaweza kutokea huko nyumbani wakati sipo. Imani 100%
Tatizo ni mama mkwe. Kipindi hiki nasafiri kama ndugu yangu yupo nyumbani huleta malalamiko mengi sana na uchochezi mkubwa. Huwa analeta headache sana kama eti binti yake yaani mke wangu husukumwa kimaamuzi. Husema nafanya mambo bila kuangalia athari na ni kinyume na dini yetu ya kiislamu. Hataki ndugu zangu wakae nyumbani. Na kweli yako mafunzo ya dini yaliyogusia kuhusu swala hili na ni kweli mafunzo yanasema sio vyema maana shetani linaweza kuwa kati, lakini nami nimelipima ya namna gani nawajibika nifanye kulingana na hali halisi ilivyo.
Lakini kwa jinsi hili swala lilivyonishika inabidi nichukue maamuzi mazito. Maamuzi ambayo yanaweza kuleta kuchafuana na mama mkwe au kufanya mambo yatakayoletea kuonyesha sitoi msaada kwa ndugu zangu kama ninavyowajibika.
Sasa wakuu, mnalionaje nyinyi hili?
Shukrani waungwana.