Ushauri kuhusu kuwa DJ

Fext

Member
Dec 26, 2016
47
49
Naanza kwa kuwashukuru wana JF wote kwa ushirikiano mnaonipa na kwa kunifunza vitu vingi ambavyo sikuvijua na kwa kweli sijutii kujiunga na wanafamilia wa JF.

Kwa leo ninaomba ushauri kuhusiana na kua DJ, kwa mda mrefu nimekua na ndoto za kua DJ ndoto ambazo nimezitimiza kwa kiasi fulani kwani sasa hivi natumia Virtual DJ kwenye laptop na kazi inaenda vizuri sana kwani naweza kwenda hata kwenye shughuli na kisiharibike kitu.

Swali langu ni kwamba kuna tofauti gani kati ya program ya Virtual DJ ya kwenye laptop na pioneer mixer (mashine ya kumixia muziki) na je kujua sana kutumia program ya virtual DJ kunaweza kunirahisishia kiasi gani kutumia mashine yenyewe ya kuchanganyia muziki?

Nitashukuru kwa ushauri wenu
 
Ni vizuri sema Virtual Dj na Mashine za mixing kama Denon na Pioneer tofauti kabisa, ila cha muhimu ni kutafuta sehemu ambapo hivyo vifaa vya mixing wanavyo ukawa unajifunza taratibu

coz CUE kwenye Virtual Dj ni tofauti na kwenye real pioneer or Denon
 
Ni vizuri sema Virtual Dj na Mashine za mixing kama Denon na Pioneer tofauti kabisa, ila cha muhimu ni kutafuta sehemu ambapo hivyo vifaa vya mixing wanavyo ukawa unajifunza taratibu

coz CUE kwenye Virtual Dj ni tofauti na kwenye real pioneer or Denon
Ahsante mkuu kwahiyo inawezekana kwa mara ya kwanza nikipewa pioneer inaweza ikanitoa out hundred percent na kuangusha maembe sana tuuu
 
Kuangusha maembe kawaida kama ndo mara ya kwanza kutumia SERATO ila cha muhimu kujiamini tu kijana, kwa sababu CUE na LOOP za SERATO ni tofauti na VIRTUAL DJ
 
Virtual dj, ni nzuri kwa beginner's kwa Sababu ya haina buttons nyingi. Pia Ina auto beat synth tofauti na machine km vile numark88 pioneer, au ns6.
 
Back
Top Bottom